ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Serikali imesaini kuanza Ujenzi wa Barabara za Mitaa ya Jiji la Dar Zenye urefu wa km 250 Kwa zaidi ya Shilingi Trilioni 1.2.
Pamoja na kwamba Jiji la Dar ndio kitovu Cha Uchumi wa Nchi ila upendeleo umezidi.
Kwa jini la Dar peke yake Kuna miradi yenye zaidi ya km 600 kama Ifuatavyo. Pia soma Miaka Zaidi ya 60 Baada ya Uhuru,Tanzania Imeshindwa Kuondoa Mizizi ya Ukoloni Kwa Nchi kuwa tegemezi wa Uchumi na Mapato Kwa Jiji Moja tuu la Dar
1.DMDP-II km 250
2.TanRoads km 120
3.TARURA km 30
4.Manispaa za Jiji km 12
Waziri OR-TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa leo tarehe
24 Oktoba, 2024 ameshuhudia
utiaji saini wa mikataba ya awali ya ujenzi wa zaidi ya kilomita 250 za barabara za Mkoa wa Dar es Salaam zitakazojengwa na mradi wa DMDP awamu ya 2
Mradi wa DMDP-II utatekelezwa kwa gharama ya Dola za Marekani milioni 438 sawa na shilingi trillion 1.182 katika fedha hizi, kiasi cha Shilingi trillioni 1.03 ni fedha za mkopo kutoka Benki ya Dunia na Shilingi billioni 143 ni fedha ya ruzuku kutoka Serikali ya Uholanzi
Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu na Mratibu wa Miradi-TARURA, Mhandisi Humprey Kanyenye amesema katika awamu ya kwanza ya mradi, Halmashauri za Manispaa ya Kinondoni, Ilala na Temeke zilinufaika ambapo takribani kilomita 207 za barabara zilijengwa kwa kiwango cha lami.
Kilomita 75.2 za mifereji ya maji ya mvua iliboreshwa. Mradi pia ulijenga kituo kimoja cha afya, masoko kumi ya kisasa, maeneo sita ya wazi (open spaces) na viwanja viwili vya michezo. Aidha, DMDP-1 zilijengwa stendi za mabasi (4), madaraja ya waenda kwa miguu (28).
My Take
Jiji Moja km 612? Wakati Kuna Mikoa haijaunganishwa na Lami achilia mbali Barabara za Mitaa.
Hii sio sawa na Wala sio Afya ila Hongereni watu wa Dar. Pia soma Shilingi Trilioni 1 kutoka World Bank kuigeuza Dar kuwa kama Dubai. Ni mkopo wa mradi wa DMDP-II
Tanzania sio Dar peke yake David Kafulila: Kampuni ya COVEC ya China kumwaga Tsh. Trilioni 2.7 kujenga barabara 10 za kulipia Jijini Dar kwa njia ya PPP
View: https://www.instagram.com/p/DBhCl8_NsfR/?igsh=MW81bTV3aGd2OTZoMg==