Waziri Mchengerwa: Tirioni moja kutumika kuboresha Miundombunu Dar

Waziri Mchengerwa: Tirioni moja kutumika kuboresha Miundombunu Dar

Barabara ya Mbezi Victoria kwenda Bunju via Mpigi Magoe nayo ikumbukwe sasa.

Tunajua hii ni barabara ya TANROADS na tenda ilitangazwa mwezi June 2024 lakini mpaka sasa kimya. Taratibu za tenda zote hufanyikia kwenye mfumo wa NEST na kila hatua ni rahisi kuijua kwa kuona tenda imefikia wapi. Lakini baada ya hii tenda kufunguliwa, imepotea kabisa hata kwenye mfumo.

Tunaomba kujua utaratibu umefikia wapi au ndo imeisha tena??

Kwa saaa barabara inafanyiwa maintanance ya kukwanguliwa ila haina hata kifusi. TANROADS mtusaidie jamani.
 
Nakubaliana na wewe kuhusu DSM kupendelewa barabara za "rami" za mitaa,tena kwa gharama kubwa zaidi ya uhalisia( nisiambiwe eti mifereji ya maji, taa, matuta ndivyo vimeongeza gharama), wakati mikoani huku hatuna barabara hizo, ila si kweli kuwa mambo kama haya ndiyo yanafanya watu wasijiandikishe na kupiga kura, kwani tumeambiwa na Waziri wa TAMISEMI kuwa, Watz 31 milioni wamejiandikisha, na hata kama si kweli,sababu ya msingi kwenye kutojiandikisha ni mchakato mzima wa uchaguzi kutothamini kura zetu.
Kwa kweli hata Mimi binafsi kusema nitakuja kusimama kwenye line nikaoige kura hapana Hadi hapo wa Mikoani tutakapothaminiwa.

Ona wenzetu hapa ni Botswana na huu sio Mji Mkuu Gaborone Bali Mji wa huko Mkoani 👇👇

View: https://x.com/AfricaViewFacts/status/1849699165518860759?t=wHEhPgJFNmETwDf7FJYvVQ&s=19
 
Kwa kweli hata Mimi binafsi kusema nitakuja kusimama kwenye line nikaoige kura hapana Hadi hapo wa Mikoani tutakapothaminiwa.

Ona wenzetu hapa ni Botswana na huu sio Mji Mkuu Gaborone Bali Mji wa huko Mkoani 👇👇

View: https://x.com/AfricaViewFacts/status/1849699165518860759?t=wHEhPgJFNmETwDf7FJYvVQ&s=19

Watanzania tuache uchawa wa mtu au chama bali tuwe machawa wa maendeleo.
Kwenye upangaji wa mgawanyo wa miradi kufanywa wapi,hii mikoa yetu inapunjwa mno mno.
 
Serikali imesaini kuanza Ujenzi wa Barabara za Mitaa ya Jiji la Dar Zenye urefu wa km 250 Kwa zaidi ya Shilingi Trilioni 1.2.

Pamoja na kwamba Jiji la Dar ndio kitovu Cha Uchumi wa Nchi ila upendeleo umezidi.

Kwa jini la Dar peke yake Kuna miradi yenye zaidi ya km 600 kama Ifuatavyo. Pia soma Miaka Zaidi ya 60 Baada ya Uhuru,Tanzania Imeshindwa Kuondoa Mizizi ya Ukoloni Kwa Nchi kuwa tegemezi wa Uchumi na Mapato Kwa Jiji Moja tuu la Dar

1.DMDP-II km 250
2.TanRoads km 120
3.TARURA km 30
4.Manispaa za Jiji km 12

Waziri OR-TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa leo tarehe
24 Oktoba, 2024 ameshuhudia
utiaji saini wa mikataba ya awali ya ujenzi wa zaidi ya kilomita 250 za barabara za Mkoa wa Dar es Salaam zitakazojengwa na mradi wa DMDP awamu ya 2

Mradi wa DMDP-II utatekelezwa kwa gharama ya Dola za Marekani milioni 438 sawa na shilingi trillion 1.182 katika fedha hizi, kiasi cha Shilingi trillioni 1.03 ni fedha za mkopo kutoka Benki ya Dunia na Shilingi billioni 143 ni fedha ya ruzuku kutoka Serikali ya Uholanzi

Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu na Mratibu wa Miradi-TARURA, Mhandisi Humprey Kanyenye amesema katika awamu ya kwanza ya mradi, Halmashauri za Manispaa ya Kinondoni, Ilala na Temeke zilinufaika ambapo takribani kilomita 207 za barabara zilijengwa kwa kiwango cha lami.

Kilomita 75.2 za mifereji ya maji ya mvua iliboreshwa. Mradi pia ulijenga kituo kimoja cha afya, masoko kumi ya kisasa, maeneo sita ya wazi (open spaces) na viwanja viwili vya michezo. Aidha, DMDP-1 zilijengwa stendi za mabasi (4), madaraja ya waenda kwa miguu (28).

My Take
Jiji Moja km 612? Wakati Kuna Mikoa haijaunganishwa na Lami achilia mbali Barabara za Mitaa.

Hii sio sawa na Wala sio Afya ila Hongereni watu wa Dar. Pia soma Shilingi Trilioni 1 kutoka World Bank kuigeuza Dar kuwa kama Dubai. Ni mkopo wa mradi wa DMDP-II

Tanzania sio Dar peke yake David Kafulila: Kampuni ya COVEC ya China kumwaga Tsh. Trilioni 2.7 kujenga barabara 10 za kulipia Jijini Dar kwa njia ya PPP

View: https://www.instagram.com/p/DBhCl8_NsfR/?igsh=MW81bTV3aGd2OTZoMg==

Jamani kumbukeni Kuna Mikoa mingine pia sio daily Dar 👇👇

View: https://www.instagram.com/p/DCMAPdJtOl8/?igsh=MTFuZHlwYXR6NnlkNw==
 
Back
Top Bottom