Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,147
- 2,008
Akichangia hoja ya Utoshelevu wa Watumishi wa Umma na mifumo ya ajira nchini Bungeni leo, Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ameagiza Sekretarieti ya Ajira kutangaza vijana waliofaulu usaili wa ajira za utumishi wa Umma na Julai 1, ajira zote mpya zianze kufanya kazi.
Vile vile ameelekeza Mfumo wa usaili kuwezeshwa katika Mikoa yote nchini,ili hatua ya awali ya usaili ifanyike Mikoani na hatua nyingine kufanyika ngazi ya Kanda na hata Taifa ili kupunguza kero ya Vijana ya usafiri kufuata vituo vya usaili Jijini Dodoma.
Aidha ameagiza Sekretarieti ya Ajira kutunza kumbukumbu za wanaofaulu usaili katika nafasi zinazofanana ili vijana wasihangaike kurudia kufanya usaili na badala yake database hiyo itumike kuajiri.