Waziri Mhagama awajulia hali Mama Janeth Magufuli na Mama Asina Kawawa

Waziri Mhagama awajulia hali Mama Janeth Magufuli na Mama Asina Kawawa

“Watu wazuri hawafi”

Jenista ameenda kuwaomba hawa wajane wasisusie mialiko ya serikali baada ya kushambuliwa kwa maneno na kina Mzee Makamba kwenye mkutano wa Kamati Kuu ya CCM.
 
View attachment 2495808

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama akifurahia jambo na Mama Janeth Magufuli mjane wa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, mara baada ya kuwasilisha salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Mama Janeth Magufuli, alipoenda kumjulia hali nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.

View attachment 2495809

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama akiwasilisha salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Mama Asina Kawawa, mjane wa Waziri Mkuu Mstaafu, Hayati Rashid Mfaume Kawawa, alipoenda kumjulia hali nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.
Pozi la mama Kawawaa kama anashangaa shangaa tu mnamsumbua tu
 
Back
Top Bottom