Waziri Mhagama: Maambukizi ya VVU Kutoka kwa Mama Kwenda kwa Mtoto yamepungua Nchini

Waziri Mhagama: Maambukizi ya VVU Kutoka kwa Mama Kwenda kwa Mtoto yamepungua Nchini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

Screenshot 2024-11-29 at 19-10-04 Nchi Kwanza (@nchikwanza) • Instagram photos and videos.png

Na WAF - Ruvuma

Waziri wa Afya Mhe. Jesnista Mhagama amesema kiwango cha maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto yamepungua kutoka asilimia 18 mwaka 2010 hadi asilimia 8.1 mwaka 2023.

Waziri Mhagama amesema hayo Novemba 29, 2024 wakati wa ufunguzi wa kongamano la kitaifa la kisayansi la masuala ya UKIMWI pamoja uzinduzi na usambazaji wa ripoti ya utafiti wa viashiria na matokeo ya UKIMWI mwaka 2022 - 2023 uliofanyika Songea mkoani Ruvuma.

Screenshot 2024-11-29 at 19-10-36 Nchi Kwanza (@nchikwanza) • Instagram photos and videos.png

Waziri Mhagama amesema usalama wa watoto wanaozaliwa kutopata maambukizi ya VVU hivi sasa ni mkubwa kutokana na jitihada za Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo kuwekeza na kutekeleza afua mbalimbali za masuala ya VVU na UKIMWI.

"Nishukuru sana kwa juhudi za wadau wote ambao wanajielekeza katika kuhakikisha maisha yanaendelea kwa WAVIU na watoto wanaozaliwa katika mahusiano mbalimbali hapa nchini wanakua salama," amesema Waziri Mhagama.

Screenshot 2024-11-29 at 19-11-08 Nchi Kwanza (@nchikwanza) • Instagram photos and videos.png

Aidha, Waziri Mhagama ameishukuru Tume ya Taifa Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) kwa kuendelea kuratibu suala zima la mapambano ya VVU na UKIMWI kwa kutengeneza mikakati unganishi na shirikishi ambayo itasaidia katika kufikia mafanikio na mikakati iliyowekwa.

Waziri Mhagama ametoa wito kwa kila mmoja kushiriki katika kulinda na kuthamini mafanikio yaliyofikiwa ikiwa ni pamoja na kuondoa unyanyapaa kwa watu wanaishi na maambukizi ya VVU.

Screenshot 2024-11-29 at 19-11-40 Nchi Kwanza (@nchikwanza) • Instagram photos and videos.png

Naye Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe. Kapenjama Ndile ambaye amemuwakilisha Mkuu wa Mkoa huo amesema Mkoa huo umepata mafanikio ya kupambana na maambukizi mapya ya VVU kutoka asilimia 5.6 mwaka 2017 hadi 4.9 mwaka 2022 ikiwa sawa na asilimia 0.7 huku viwango vya kitaifa ikiwa na asilimia 2.8.

Wiki ya maadhimisho ya kitaifa ya siku ya UKIMWI duniani yanaendelea mkoani Ruvuma ambapo yanatarajiwa kufikia kilele tarehe 1 Disemba 2024 ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akitarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Screenshot 2024-11-29 at 19-11-28 Nchi Kwanza (@nchikwanza) • Instagram photos and videos.png
 

Attachments

  • Gdj1b8WWMAALtNF.jpg
    Gdj1b8WWMAALtNF.jpg
    148.1 KB · Views: 5
  • Screenshot 2024-11-29 at 19-10-58 Nchi Kwanza (@nchikwanza) • Instagram photos and videos.png
    Screenshot 2024-11-29 at 19-10-58 Nchi Kwanza (@nchikwanza) • Instagram photos and videos.png
    882.2 KB · Views: 3
  • Screenshot 2024-11-29 at 19-11-19 Nchi Kwanza (@nchikwanza) • Instagram photos and videos.png
    Screenshot 2024-11-29 at 19-11-19 Nchi Kwanza (@nchikwanza) • Instagram photos and videos.png
    640.1 KB · Views: 4
  • Screenshot 2024-11-29 at 19-10-48 Nchi Kwanza (@nchikwanza) • Instagram photos and videos.png
    Screenshot 2024-11-29 at 19-10-48 Nchi Kwanza (@nchikwanza) • Instagram photos and videos.png
    543.1 KB · Views: 3
  • Screenshot 2024-11-29 at 19-10-14 Nchi Kwanza (@nchikwanza) • Instagram photos and videos.png
    Screenshot 2024-11-29 at 19-10-14 Nchi Kwanza (@nchikwanza) • Instagram photos and videos.png
    673.6 KB · Views: 4
Back
Top Bottom