Waziri Mhagama: Tanzania Inakuja na Mifumo Imara ya Bima ya Afya kwa Wote Nchini

Waziri Mhagama: Tanzania Inakuja na Mifumo Imara ya Bima ya Afya kwa Wote Nchini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Screenshot 2024-12-10 at 15-20-23 Zainab Athman Katimba (@zainabkatimba) • Instagram photos an...png

Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagamana na ujumbe wake akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Bw. Ismail Rumatila, Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu pamoja na wataalam wengine Desemba 09, 2024 wamefanya ziara ya mafunzo ya jinsi mfumo wa uendeshaji wa masuala ya afya unavyofanya kazi chini ya Wizara ya Afya Uingereza.

Hatua hii ni muhimu kuelekea utekelezaji wa sheria ya Bima ya Afya kwa wote nchini Tanzania kwa kuhakikisha kuwa tunakuwa na mifumo imara katika usimamiaji wa huduma za afya.

Soma Pia: Jenista Mhagama afika Mji wa London, azungumza na Watanzania waishio Uingereza

Screenshot 2024-12-10 at 15-20-27 Zainab Athman Katimba (@zainabkatimba) • Instagram photos an...png

"Miongoni mwa mambo tuliyojifunza kutoka kwa wenzetu wakiongozwa na Mkurugenzi msaidizi wa Ushirikiano wa Kimataifa kutoka Wizara ya Afya ya Uingereza Dkt. Kevin Miles ni pamoja na jinsi huduma za afya kupitia Bima ya Afya zinavyotolewa kwa wanachama, mifumo ya utoaji wa huduma kupitia Bima ya Afya jinsi inavyofanya kazi pamoja na namna ambavyo wanalipwa watoa huduma hao," amesema Waziri Mhagama.

GebsmmhWsAAWp2_.jpg
GebsmmgXAAAU8lt.jpg
 

Attachments

  • GebsmmoWIAAAMdm.jpg
    GebsmmoWIAAAMdm.jpg
    154.1 KB · Views: 5
  • GebsmmpXEAA78AR.jpg
    GebsmmpXEAA78AR.jpg
    148.2 KB · Views: 5
Back
Top Bottom