Mlezi wa Kikundi cha Marsho Manufacturing Company kinachojishughulisha na shughuli za ujasiriamali kupitia zao la ndizi ambae pia ni Mbunge wa Rombo Prof. Adolf Mkenda, Jumanne ya March 11,2025 amekikabidhi hundi ya Shilingi Milioni 5 ikiwa kama sehemu ya ahadi yake yakukisaidia kikundi hicho.
Kikundi hicho chenye ofisi zake Kata ya Makidi Wilaya ya Rombo kimekuwa kikijihusisha na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali ikiwemo za vyakula kupitia zao la ndizi.