Waziri Mkenda: Tunaendelea na zoezi la kumwaga sumu kuua nzige ambao sasa wameelekea Monduli pia Simanjiro!

Waziri Mkenda: Tunaendelea na zoezi la kumwaga sumu kuua nzige ambao sasa wameelekea Monduli pia Simanjiro!

Kiuatilifu kinachotumika ni photo and biodegradable; easily degrades into harmless metabolites ndani ya muda mfupi kwenye mazingira. Kwa hiyo uwezekano wa kuingia kwenye food chain haupo. Siyo aina ya organochlorides ambayo hukaa kwenye mazingira for days/months and years.
Kinaitwaje?
 
India haooo
IMG_6048.jpg
 
Nchi haina ndege ya kilimo wakati kilimo ndiyo uti wa mgongo mnaenda kukodi Kenya shem on my country
 
Kundi jipya la Nzige limeingia Mkomazi Hilo lisipodhibitiwa litasambaa milima ya usambara yote na kuathiri mazao mengi
 
Waziri wa Kilimo Prof Mkenda amesema kesho zoezi la kumwaga sumu ya kuua nzige litaendelea baada ya rubani aliyetelekeza ndege pale Kilimanjaro kurejea.

Mkenda amesema kuna kundi la nzige wadogo wameelekea Monduli hivyo wanawafuatilia ili wawatekeze.

Pia Simanjiro zoezi halikukamilika kutokana na mazingira ya huko ambayo yana vichaka na miiba hivyo kuna nzige ambao hawakufikiwa na timu ya wataalamu imetumwa kuwateketeza kwa kutumia ndege ya fao.

Katika hatua nyingine waziri Mkenda amemlaumu CEO wa oganaizesheni ya kupambana na nzige Afrika mashariki kwa kutotoa ushirikiano na hata kutopokea simu zake huku akijua wazi sehemu ya mshahara wake inatokana na kodi za watanzania.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
Hivi si gwajima na mzee wa upako walituhakikishia kuwa wamewazuia nzige wasiingie tanzania?
 
Nchi haina ndege ya kilimo wakati kilimo ndiyo uti wa mgongo mnaenda kukodi Kenya shem on my country
Haijakodiwa ni ndege ya shirika la nzige wa jangwani kila nchi inahudumiwa na izo ndege japo kwa tahadhari inatakiwa tuwe nazo
 
Back
Top Bottom