Waziri Mkumbo: Tumekusanya maoni ya vyama vyote vya Siasa Dira ya Taifa ya maendeleo 2050

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo akizungumza katika mkutano wake na wahariri wa vyombo vya habari kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, uliofanyika katika Hoteli ya Serena Ijumaa, mkoani Dar es Salaam tarehe 6 Disemba 2024, amesema:

"Tumekusanya vilevile maoni ya wadau wa vyama vya siasa vyote, kwasababu hii ilikuwa ni muhimu kama ambavyo nimekuwa nikisema siku zote kwamba tunaandika Dira ya Taifa ya Maendeleo, siyo dira ya serikali kwahiyo wadau wote, wananchi wote lazima wahudhurie. Lakini pia tulipata nafasi katika makundi, wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walipata nafasi mahususi ya kuweza kutoa maoni yao katika hatua hii. Kwahiyo mchakato umekuwa jumuishi sana, na tumepokea maoni mengi, na wananchi wamejitokeza kwa wingi sana kwenye zoezi hili"

1733471660571.png
 
Machadema hayakususia kweli?
 
Back
Top Bottom