mkiluvya
JF-Expert Member
- May 23, 2019
- 809
- 729
WAZIRI MKUU AFURAHISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI WA MRADI WA UMEME MTO RUFIJI:
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewahakikishia Watanzania kuwa kazi ya Ujenzi wa Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) wa megawatts 2115 inayofanyika katika eneo la Bonde la Mto Rufiji ni kazi ya uhakika na inakwenda kwa kasi kama ilivyopangwa.
Majaliwa ameyasema hayo leo, Alhamisi, Mei 14, alipokuwa kwenye ziara ya kukagua hatua za utekelezaji wa mradi huo.
“Nimetembelea eneo la mradi na kujionea shughuli zote zinazoendelea, Kazi inayofanyika ni ya uhakika huku matumaini ni makubwa ya kukamilisha mradi mapema kabla ya muda uliopangwa” Waziri mkuu Kassim Majaliwa.
Aidha, ameeleza kuridhishwa na hatua za utekelezaji ambazo mradi umefikiwa na kueleza kuwa mradi huo wa Julius Nyerere ni mradi mkubwa na wa kimkakati na kutoa pongezi kwa TANESCO na usimamizi wa Wakandarasi kwa kazi nzuri.