Waziri Mkuu aitaka Wizara kutoa taarifa haraka kuhusu Mechi ya Simba na Yanga pamoja na Viingilio vya Mashabiki

Waziri Mkuu aitaka Wizara kutoa taarifa haraka kuhusu Mechi ya Simba na Yanga pamoja na Viingilio vya Mashabiki

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoa taarifa haraka sana kwa Watanzania juu ya tarehe ya kuchezwa kwa mchezo huo na pia ieleze utaratibu kuhusu hatima ya waliolipa viingilio ili kushuhudia mchezo huo.

Pia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewasihi Watanzania kuwa wavumulivu ili kuipa muda Wizara kwa kushirikiana na taasisi zinazosimamia mpira wa miguu ikiwemo TFF kuja na taarifa juu ya hatima ya mchezo huo.
 
Tunataka sababu ya kuahirishwa mechi,mbona anakwepa hapo?
Simba ndio waliosababisha.Wachezaji wao wengi wamefunga Ramadhani wakawaambia TFF kuwa watakuwa hawana nguvu sababu ya swaaumu hhivyo wakaomba mchezo uchezwe saa moja usiku baada ya wao kufuturu saa 12 jioni.

Ndipo sisi yanga tukagoma sababu kanuni ya kubadilishwa imekiukwa.
 
yan mpaka hapa mashabiki ni wavumilivu sana na wastarabu, wanachotaka sanaa sanaaa ni tarehe ya mechi itakapo chezwa
 
Akiwa bungeni leo, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa, amewataka TFF kwa kushirikiana na Wizara ya Habari na Michezo kusema lini Simba na Yanga zitacheza.

Pia amewataka Watanzania kuwa wavumilivu kwa usumbufu uliojitokeza siku ya Jumamosi, hasa wale waliolipa viingilio siku ya mchezo ijulikane hatma yao.
 
Hawa watu bado tu wapo ofisini? Yaani hatuna serikali kabisa
 
Mh. Majaliwa alikuwa ni mtendaji na msimamizi mzuri sana ila katika hii hawamu ya 6 naona akikwama na kupoteza vipaji vyake hvyo ..sincerely, haendani na bosi wake kifikra na kimitizamo kabisa
 
Uongozi huu wa TFF tutamkumbuka Wallace kwa uhuni na ubabaishaji wa uendeshaji wa michezo Tanzania. Huyu Msomali anatuletea mambo ya Somalia kwenye michezo.
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoa taarifa haraka sana kwa Watanzania juu ya tarehe ya kuchezwa kwa mchezo huo na pia ieleze utaratibu kuhusu hatima ya waliolipa viingilio ili kushuhudia mchezo huo.

Pia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewasihi Watanzania kuwa kuwa wavumulivu ili kuipa muda Wizara kwa kushirikiana na taasisi zinazosimamia mpira wa miguu ikiwemo TFF kuja na taarifa juu ya hatima ya mchezo huo
Huyu naye ni Mhuni na laghai Mkubwa. Alitwambia Mwendazake anapitia mafaili. Kweli akapitia mafaili jumla.
 
Ukimsikiliza anavyoaddress hii issue unakuwa unafikiri neno linalofuata ndiyo lenye uzito ila mpk mwisho hakuna chochote ametoa tamko rahisi ambalo lingeweza kutolewa na yeyote tu wa chini yake mambo mengine ni petty issues tuwaachie wa chini wayahandle tu hasa kwa aliyoyasema. Labda kama angesimama kuzungumzia nini ilikuwa sababu hasa ya delaying ya kick off kutoka 11 mpk 1 lakini sijui lini itachezwa mara viingilio hata Ndimbo angeweza kusema achilia mbali Karia
 
Back
Top Bottom