Waziri Mkuu apokea orodha ya majina 453 ya wananchi wa Ngorongoro waliokubali kuhama kwa hiyari yao

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Waziri mkuu mh Majaliwa leo amepokea orodha ya awali ya wananchi 453 walioomba kuhama kwa hiyari katika hifafhi ya Ngorongori.

Waziri mkuu amewaahidi wamasai hao kwamba serikali itawapeleka kuishi sehemu yoyote watakayoichagua wao wenyewe.

Source: ITV habari!

=====

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amepokea orodha ya majina ya awali ya kaya 86 zenye watu 453 ambao wamekubali kuondoka kwenye hifadhi ya Ngorongoro kwa hiari yao huku wengine wakiendelea kujiandikisha.

--
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amepokea orodha ya majina ya awali ya kaya 86 zenye watu 453 ambao wamekubali kuondoka kwenye hifadhi ya Ngorongoro kwa hiari huku wengine wakiendelea kujiandikisha.

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi, Machi 10, 2022 na Ofisi ya Waziri Mkuu imesema kuwa, Majaliwa amepokea majina hayo baada ya kumaliza kikao na viongozi wa kimila wa jamii ya Kimasai (Laigwanak) kwenye mkutano uliofanyika eneo la Oretei Loongaik-Marya, kwenye Chuo cha Ufundi Arusha, jijini Arusha.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa mazungumzo ambayo Waziri Mkuu aliyafanya na wadau wa uhifadhi kwenye vikao vilivyofanyika Februari 14 na 17 mwaka huu kwenye tarafa za Loliondo na Ngorongoro, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.

Majina hayo yamekabidhiwa kwa Waziri Mkuu na Mkuu wa Mkoa wa Arusha (DC), John Mongela amesema majina hayo ni ya awali na tayari yalishahakikiwa mara baada ya wakazi hao kujiandikisha.

“Tutawasimamia vizuri hadi waende kule wapate hati za mashamba, nyumba na maeneo ya kulisha mifugo yao.”

Akizungumza na Malaigwanak hao zaidi ya 350, Waziri Mkuu amesema Rais Samia Suluhu Hassan alipofanya ziara mkoani humo aliliambia Taifa iko hatari ya kutoweka kwa hifadhi ya Ngorongoro ndani ya muda mfupi na akatoa maagizo viongozi waende kuwasikiliza wananchi juu ya hatua za kuchukua ili tunu hiyo isipotee.

“Ile hatari aliyosema Rais ni ipi? Zamani watu waliweza kuishi na wanyama bila tatizo kwa sababu kulikuwa na wakazi 8,000 tu wenye ng’ombe 20 hadi 30. Leo hii kuna wakazi 110,000 na mifugo zaidi ya 813,000 wakiwemo ng’ombe, mbuzi na kondoo.

“Zamani maboma yalikuwa yamesambaa lakini leo hii nyumba zimejaa, tena za bati na tofali. Idadi ya watu imeongezeka, idadi ya mifugo imeongezeka na makazi yameongezeka. Hakuna huduma za afya au shule wakati ni hitaji muhimu kwa wananchi.” imesema taarifa hiyo

Amewaeleza viongozi hao kwamba Serikali imetenga eneo la ekari 400,000 wilayani Handeni ambalo kati ya hizo, ekari 220,000 zimeshapimwa.

“Tumepima viwanja 2,406 ambapo kati ya hivyo, viwanja 2,070 tumeandaa kwa ajili ya makazi na kila kimoja kina ukubwa wa ekari tatu. Tumeanza na nyumba za kuanzia 101 za vyumba vitatu vya kulala kwa wale wanaotaka. Tuna viwanja 336 kwa ajili ya huduma kama shule za msingi na sekondari, zahanati na vituo vya afya. Ujenzi wa mifumo ya maji kazi inaendelea

“Umeme wa REA pia utakuwepo. Huku mlipo hakuna umeme. Haya tutayafanya na Mheshimiwa Rais Samia amesisitiza tuyafanye ili wananchi msipate bugudha,” imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imesema kuwa Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Wamasai Tanzania, Isack Ole Kisongo alisema kwa nafasi yao viongozi wa kimila wako tayari kushirikiana na Serikali kuhakikisha rasilimali za nchi zinawanufaisha Watanzania wote.

"Kwa kunyanyua rungu zetu tumekula kiapo kwa kukubali kuwa Ngorongoro na hifadhi nyingine nchini zilindwe kwa nguvu zote ili hadhi yake irudi kama zamani” imesema taarifa hiyo ikimnukuu kiongozi wa Wamasai nchini

Taarifa hiyo imesema kuwa Laigwanani wa Malaigwanani wa Ngorongoro, mzee Matengway Ole Tauwo alimweleza Waziri Mkuu kwamba anasubiri tarehe ya kuhamia huko kwa sababu ameenda hadi Handeni na ameona kwa macho yake kwamba mipango ya Serikali ina lengo zuri.
 
Habari zako nyingine zina Source zingine huwa ni Propaganda za Chama.
 
Hiyo ni janja janja tu, ki fupi ni kuwa hao Wamaasai wote hawatakiwi eneo hilo, na lazima tu wataondolewa!!ni suala la muda tu, kwani leo nimemsikia waziri wa mali asili na utalii, kupitia DW, ni kuwa lazima waondoke tu kwani mbona sehemu nyingine watu wanahamishwa?
 
Imepigwa Fitna Mpaka Maasai Hoi

Haya Ya Kuhama Niliwahi Kuyaona Kigoma Wakimbizi Wakirudi Kwao Rwanda, Congo, Burundi

Leo Sasa Ni Ndani Kwa Ndani
 
Hapo kama serikali ina mpango wa kuwaondoa kwa nguvu hao wamasai bora ifanye hivyo tu, kuwatengeneza hao 450 ili kuwahamasisha wengine wanaojielewa waondoke haitakuwa kazi rahisi.
 
Kunamambo serekali ikishaamua hakuna njia ya kuyakwepa. Walianza kimasiara kutekenya Sasa taratiiibu watu wanainua makwapa. Yaan kwa kifupi suala la Masai kuondoka kwenye hiyo hifadhi ni lazima ni Jambo la taratibu tu
 
Watu wanavamia maeneo na kuyaendeleza Serikali ikiona. Ni wakati sasa Serikali iache kufanya kazi kama zima moto.
 
Hivi Malisho ya mifugo yao itakuwa ni wapi vile tukiletewa hao jamaa huku mtaani na makundi yao ya mbuzi na ng'ombe

Kuna baadhi ya vijiji vya Wamasai vimejitokeza kati yetu lakini bado imekuwa kero kwa mazao yetu na wizi wa mifugo yetu pia
sasa je ukienda kuhamisha ngome nzima ya maasai itakuwaje hapo
 
Hapa serikali imetumia akili. Imecheza kama Pele.

Wapinga kuhama walikuwa wachache ila wenye sauti sababu walikuwa backed na wanaharakati na international NGO’s zilizofanikiwa kutengeneza picha ya uonevu, unyanyasaji na uporaji haki kupitia vyombo vya habari.

Serikali ilibonyea na kujifanya wapole wakati move ya kuconvince wahame ikiendelea chini kwa chini. Hii ndiyo faida ya ’divide and rule’ . Kwa hiyo hapo serikali imefanikiwa kuvunja umoja ambayo ni silaha kubwa, na kuionyesha dunia kwamba wanahamishwa kwa hiari yao baada ya kupokea elimu. Waliobaki ni suala la mudatu, wote wataondoka.
 
Wamasai wahame ,mbuga zingine raia hawatakiwi kwenye eneo la hifadhi,je Masai wao ni nani
 
Ngorongoro.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amepokea orodha ya majina ya awali ya kaya 86 zenye watu 453 ambao wamekubali kuondoka kwenye hifadhi ya Ngorongoro kwa hiari huku wengine wakiendelea kujiandikisha.

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi, Machi 10, 2022 na Ofisi ya Waziri Mkuu imesema kuwa, Majaliwa amepokea majina hayo baada ya kumaliza kikao na viongozi wa kimila wa jamii ya Kimasai (Laigwanak) kwenye mkutano uliofanyika eneo la Oretei Loongaik-Marya, kwenye Chuo cha Ufundi Arusha, jijini Arusha.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa mazungumzo ambayo Waziri Mkuu aliyafanya na wadau wa uhifadhi kwenye vikao vilivyofanyika Februari 14 na 17 mwaka huu kwenye tarafa za Loliondo na Ngorongoro, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.

Majina hayo yamekabidhiwa kwa Waziri Mkuu na Mkuu wa Mkoa wa Arusha (DC), John Mongela amesema majina hayo ni ya awali na tayari yalishahakikiwa mara baada ya wakazi hao kujiandikisha.

“Tutawasimamia vizuri hadi waende kule wapate hati za mashamba, nyumba na maeneo ya kulisha mifugo yao.”

Akizungumza na Malaigwanak hao zaidi ya 350, Waziri Mkuu amesema Rais Samia Suluhu Hassan alipofanya ziara mkoani humo aliliambia Taifa iko hatari ya kutoweka kwa hifadhi ya Ngorongoro ndani ya muda mfupi na akatoa maagizo viongozi waende kuwasikiliza wananchi juu ya hatua za kuchukua ili tunu hiyo isipotee.

“Ile hatari aliyosema Rais ni ipi? Zamani watu waliweza kuishi na wanyama bila tatizo kwa sababu kulikuwa na wakazi 8,000 tu wenye ng’ombe 20 hadi 30. Leo hii kuna wakazi 110,000 na mifugo zaidi ya 813,000 wakiwemo ng’ombe, mbuzi na kondoo.

“Zamani maboma yalikuwa yamesambaa lakini leo hii nyumba zimejaa, tena za bati na tofali. Idadi ya watu imeongezeka, idadi ya mifugo imeongezeka na makazi yameongezeka. Hakuna huduma za afya au shule wakati ni hitaji muhimu kwa wananchi.” imesema taarifa hiyo

Amewaeleza viongozi hao kwamba Serikali imetenga eneo la kilometa za mraba 400,000 wilayani Handeni ambalo kati ya hizo, kilometa za mraba 220,000 zilitumika kwa kujenga nyumba, kupima viwanja na kutenga maeneo ya malisho.

“Tumepima viwanja 2,406 ambapo kati ya hivyo, viwanja 2,070 tumeandaa kwa ajili ya makazi na kila kimoja kina ukubwa wa ekari tatu. Tumeanza na nyumba za kuanzia 101 za vyumba vitatu vya kulala kwa wale wanaotaka. Tuna viwanja 336 kwa ajili ya huduma kama shule za msingi na sekondari, zahanati na vituo vya afya. Ujenzi wa mifumo ya maji kazi inaendelea

“Umeme wa REA pia utakuwepo. Huku mlipo hakuna umeme. Haya tutayafanya na Mheshimiwa Rais Samia amesisitiza tuyafanye ili wananchi msipate bugudha,” imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imesema kuwa Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Wamasai Tanzania, Isack Ole Kisongo alisema kwa nafasi yao viongozi wa kimila wako tayari kushirikiana na Serikali kuhakikisha rasilimali za nchi zinawanufaisha Watanzania wote.

"Kwa kunyanyua rungu zetu tumekula kiapo kwa kukubali kuwa Ngorongoro na hifadhi nyingine nchini zilindwe kwa nguvu zote ili hadhi yake irudi kama zamani” imesema taarifa hiyo ikimnukuu kiongozi wa Wamasai nchini

Taarifa hiyo imesema kuwa Laigwanani wa Malaigwanani wa Ngorongoro, mzee Matengway Ole Tauwo alimweleza Waziri Mkuu kwamba anasubiri tarehe ya kuhamia huko kwa sababu ameenda hadi Handeni na ameona kwa macho yake kwamba mipango ya Serikali ina lengo zuri.

CHANZO : MWANANCHI
 
Wasipokuwa makini wataandikwa hata watu wa mikoa mingine kujaza nafasi.

Serikali inapaswa ihakiki upya Kaya zote kabla ya malipo.
 
Huu ni mradi wa kupiga hela za umma, wananchi tusubiri maumivu!
 
Back
Top Bottom