Waziri Mkuu apokea orodha ya majina 453 ya wananchi wa Ngorongoro waliokubali kuhama kwa hiyari yao

Waziri Mkuu apokea orodha ya majina 453 ya wananchi wa Ngorongoro waliokubali kuhama kwa hiyari yao

Labda nichangie tena mada hii serikali iharakishe kuwaondoa binadamu wote ndani ya ngoro ngoro crater sio wamasai tu hapana. Asibakie mtu yoyote ndani ya crater baada ya saa 11 jioni kila siku, yaani wafanyakazi wa NCCA na wa mahoteli na watalii wawe wanaingia ndani ya crater asubuhi na kuondoka jioni.

Hoteli zote na ofisi za NCCA zijengwe nje ya crater huko Karatu. Hoteli zote na maofisi na kituo cha polisi zivunjwe mara moja. Mabasi yanayoenda Musoma iruhusiwe basi moja tu kwa siku. Watalii wanaoingia crater wasizidi watu 200 kwa siku. Nitarudi tena siku nyingine na ushauri mwingine.
 
Nilikuwa naandika kwenye thread mbalimbali zilizohusu hii scandal kuwa kama wao walihamia pale bahada ya kutoka Serengeti how come ngorongoro?, but now kweli wanaondoka, hii ni nchi yetu sote.
 
Waziri mkuu kwaambia wamasai watakaohamishwa Ngirongoro kuwa serikali imewatengea kilometa za mraba 400,000 eneo la Handeni. Na kilimeta za mraba 240,000 zimpimwa viwanja.
Ninachojiuliza. Tamzania nzima ina kilometa za mraba 945,000. Hizo ni pamoja ma maziwa, mbuga za wanyama n.k.
Mbona wamasai wanapendelewa kupewa nusu karibu nusu ya ardhi ya nchi hii?
 
400 kati ya laki 1 ni peanut tu
Waziri mkuu mh Majaliwa leo amepokea orodha ya awali ya wananchi 453 walioomba kuhama kwa hiyari katika hifafhi ya Ngorongori.

Waziri mkuu amewaahidi wamasai hao kwamba serikali itawapeleka kuishi sehemu yoyote watakayoichagua wao wenyewe.

Source: ITV habari!

=====

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amepokea orodha ya majina ya awali ya kaya 86 zenye watu 453 ambao wamekubali kuondoka kwenye hifadhi ya Ngorongoro kwa hiari yao huku wengine wakiendelea kujiandikisha.

View attachment 2146074
View attachment 2146075

--
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amepokea orodha ya majina ya awali ya kaya 86 zenye watu 453 ambao wamekubali kuondoka kwenye hifadhi ya Ngorongoro kwa hiari huku wengine wakiendelea kujiandikisha.

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi, Machi 10, 2022 na Ofisi ya Waziri Mkuu imesema kuwa, Majaliwa amepokea majina hayo baada ya kumaliza kikao na viongozi wa kimila wa jamii ya Kimasai (Laigwanak) kwenye mkutano uliofanyika eneo la Oretei Loongaik-Marya, kwenye Chuo cha Ufundi Arusha, jijini Arusha.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa mazungumzo ambayo Waziri Mkuu aliyafanya na wadau wa uhifadhi kwenye vikao vilivyofanyika Februari 14 na 17 mwaka huu kwenye tarafa za Loliondo na Ngorongoro, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.

Majina hayo yamekabidhiwa kwa Waziri Mkuu na Mkuu wa Mkoa wa Arusha (DC), John Mongela amesema majina hayo ni ya awali na tayari yalishahakikiwa mara baada ya wakazi hao kujiandikisha.

“Tutawasimamia vizuri hadi waende kule wapate hati za mashamba, nyumba na maeneo ya kulisha mifugo yao.”


Akizungumza na Malaigwanak hao zaidi ya 350, Waziri Mkuu amesema Rais Samia Suluhu Hassan alipofanya ziara mkoani humo aliliambia Taifa iko hatari ya kutoweka kwa hifadhi ya Ngorongoro ndani ya muda mfupi na akatoa maagizo viongozi waende kuwasikiliza wananchi juu ya hatua za kuchukua ili tunu hiyo isipotee.

“Ile hatari aliyosema Rais ni ipi? Zamani watu waliweza kuishi na wanyama bila tatizo kwa sababu kulikuwa na wakazi 8,000 tu wenye ng’ombe 20 hadi 30. Leo hii kuna wakazi 110,000 na mifugo zaidi ya 813,000 wakiwemo ng’ombe, mbuzi na kondoo.

“Zamani maboma yalikuwa yamesambaa lakini leo hii nyumba zimejaa, tena za bati na tofali. Idadi ya watu imeongezeka, idadi ya mifugo imeongezeka na makazi yameongezeka. Hakuna huduma za afya au shule wakati ni hitaji muhimu kwa wananchi.” imesema taarifa hiyo

Amewaeleza viongozi hao kwamba Serikali imetenga eneo la kilometa za mraba 400,000 wilayani Handeni ambalo kati ya hizo, kilometa za mraba 220,000 zilitumika kwa kujenga nyumba, kupima viwanja na kutenga maeneo ya malisho.

“Tumepima viwanja 2,406 ambapo kati ya hivyo, viwanja 2,070 tumeandaa kwa ajili ya makazi na kila kimoja kina ukubwa wa ekari tatu. Tumeanza na nyumba za kuanzia 101 za vyumba vitatu vya kulala kwa wale wanaotaka. Tuna viwanja 336 kwa ajili ya huduma kama shule za msingi na sekondari, zahanati na vituo vya afya. Ujenzi wa mifumo ya maji kazi inaendelea

“Umeme wa REA pia utakuwepo. Huku mlipo hakuna umeme. Haya tutayafanya na Mheshimiwa Rais Samia amesisitiza tuyafanye ili wananchi msipate bugudha,” imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imesema kuwa Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Wamasai Tanzania, Isack Ole Kisongo alisema kwa nafasi yao viongozi wa kimila wako tayari kushirikiana na Serikali kuhakikisha rasilimali za nchi zinawanufaisha Watanzania wote.

"Kwa kunyanyua rungu zetu tumekula kiapo kwa kukubali kuwa Ngorongoro na hifadhi nyingine nchini zilindwe kwa nguvu zote ili hadhi yake irudi kama zamani” imesema taarifa hiyo ikimnukuu kiongozi wa Wamasai nchini

Taarifa hiyo imesema kuwa Laigwanani wa Malaigwanani wa Ngorongoro, mzee Matengway Ole Tauwo alimweleza Waziri Mkuu kwamba anasubiri tarehe ya kuhamia huko kwa sababu ameenda hadi Handeni na ameona kwa macho yake kwamba mipango ya Serikali ina lengo zuri.

CHANZO : MWANANCHI
 
WAZIRI MKUU WA TANZANIA APOKEA MAJINA 453 YA AWALIYA WALIO TAYARI KUHAMA NGORONGORO

Malaigwanak wala kiapo kuilinda Hifadhi ya Ngorongoro kwa maslahi ya Taifa.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea orodha ya majina ya awali ya kaya 86 zenye watu 453 ambao wamekubali kuondoka kwenye hifadhi ya Ngorongoro kwa hiari yao huku wengine wakiendelea kujiandikisha. Hatua hiyo ni utekelezaji wa mazungumzo ambayo Waziri Mkuu aliyafanya na wadau wa uhifadhi kwenye vikao vilivyofanyika Februari 14 na 17, mwaka huu kwenye tarafa za Loliondo na Ngorongoro, wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha.

Waziri Mkuu amepokea majina hayo leo (Alhamisi, Machi 10, 2022) mara baada ya kumaliza kikao na viongozi wa kimila wa jamii ya Kimasai (Laigwanak) kwenye mkutano uliofanyika eneo la Oretei Loongaik – Marya, kwenye Chuo cha Ufundi Arusha, jijini Arusha. Eneo hilo hufanyika Bunge la viongozi hao na hutumika pia kufanyia ibada za kimila. Akikabidhi orodha hiyo kwa Waziri Mkuu, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Bw. John Mongela amesema majina hayo ni ya awali na tayari yalishahakikiwa mara baada ya wakazi hao kujiandikisha. “Tutawasimamia vizuri hadi waende kule wapate hati za mashamba, nyumba na maeneo ya kulisha mifugo yao.”

Akizungumza na Malaigwanak hao zaidi ya 350, Waziri Mkuu amesema Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan alipofanya ziara mkoani humo aliliambia Taifa iko hatari ya kutoweka kwa hifadhi ya Ngorongoro ndani ya muda mfupi na akatoa maagizo viongozi waende kuwasikiliza wananchi juu ya hatua za kuchukua ili tunu hiyo isipotee. “Ile hatari aliyosema Mheshimiwa Rais ni ipi? Zamani watu waliweza kuishi na wanyama bila tatizo kwa sababu kulikuwa na wakazi 8,000 tu wenye ng’ombe 20 hadi 30. Leo hii kuna wakazi 110,000 na mifugo zaidi ya 813,000 wakiwemo ng’ombe, mbuzi na kondoo.

“Zamani maboma yalikuwa yamesambaa lakini leo hii nyumba zimejaa, tena za bati na tofali. Idadi ya watu imeongezeka, idadi ya mifugo imeongezeka na makazi yameongezeka. Hakuna huduma za afya au shule wakati ni hitaji muhimu kwa wananchi.” Aliwaeleza viongozi hao kwamba Serikali imetenga eneo la kilometa za mraba 400,000 wilayani Handeni ambalo kati ya hizo, kilometa za mraba 220,000 zilitumika kwa kujenga nyumba, kupima viwanja na kutenga maeneo ya malisho.

“Tumepima viwanja 2,406 ambapo kati ya hivyo, viwanja 2,070 tumeandaa kwa ajili ya makazi na kila kimoja kina ukubwa wa ekari tatu. Tumeanza na nyumba za kuanzia 101 za vyumba vitatu vya kulala kwa wale wanaotaka. Tuna viwanja 336 kwa ajili ya huduma kama shule za msingi na sekondari, zahanati na vituo vya afya. Ujenzi wa mifumo ya maji kazi inaendelea.” “Umeme wa REA pia utakuwepo. Huku mlipo hakuna umeme. Haya tutayafanya na Mheshimiwa Rais Samia amesisitiza tuyafanye ili wananchi msipate bugudha,” amesema Waziri Mkuu.

Aliwaeleza viongozi hao wa kimila kwamba Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia eneo lao la kufanyia ibada za kimila liendelee kutumika kwa sababu ni jambo jema. “Maeneo yote ya kimila, wananchi waruhusiwe kuendesha mila zao. Mkuu wa Mkoa simamia hili, ilimradi Mkuu wa Chuo apewe taarifa mapema kwamba mnakuja lini kufanya shughuli yenu,” amesema. Mapema, Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Wamasai Tanzania, Bw. Isack Ole Kisongo alisema kwa nafasi yao viongozi wa kimila wako tayari kushirikiana na Serikali kuhakikisha rasilimali za nchi zinawanufaisha Watanzania wote. “Kwa kunyanyua rungu zetu tumekula kiapo kwa kukubali kuwa Ngorongoro na hifadhi nyingine nchini zilindwe kwa nguvu zote ili hadhi yake irudi kama zamani.”

Alisema suala la kuhama Ngorongoro halina tofauti na maeneo mengine ambako wananchi waliondoka kwa amani kupisha miradi ya maendeleo kama vile ujenzi wa reli ya kisasa, bomba la Mafuta la kutoka Tanga hadi Uganda na ukuta wa Mererani. Naye Laigwanan wa Malaigwanani wa Ngorongoro, Mzee Matengway Ole Tauwo alimweleza Waziri Mkuu kwamba anasubiri kwa hamu tarehe ya kuhamia huko kwa sababu ameenda hadi Handeni na ameona kwa macho yake kwamba mipango ya Serikali ina lengo zuri.

“Nataka uniambie leo tarehe gani Mkuu wa Mkoa ananipeleka huko, niko tayari kwenda. Mke wangu alipoona ile nyumba alitaka kugoma kurudi tena Ngorongoro. Nataka nijue tarehe ya kwenda sababu hapa sina hatimiliki, siwezi kulima lakini kule naweza,” alisema mzee huyo mwenye umri wa miaka 70. Akisoma risala kwa niaba ya Malaigwanak hao, Katibu Mkuu wa Jamii hiyo, Bw. Amani Lukumay alisema wanayo maeneo ya kimila ambayo yametishiwa kuchukuliwa na akaomba Serikali iingilie kati ili maeneo hayo yakabidhiwe rasmi kwao.


#KaziIendelee
#2022JiandaeKuhesabiwa

IMG-20220310-WA0027.jpg


IMG-20220310-WA0029.jpg
 
Hakuna kama Tanzania! Nikiwa mdogo niliambiwa Tanzania ni ya pili nyuma ya Islael kwa "ujasusi" leo ndio nimeamini. Maulid Kitenge oyeeeee! NGO ziiiiiiiiii!
 
Mungu atawalaani wote wanaofanya hujuma na uonevu kwa jamii ya kimasai.

Amen.

Baada ya kusema hayo. Sitachangia tena hili jambo.
 
Hao wamasai wakisubili pa kwenda wawaulize waliopisha mgodi wa ggm geita na ulyankulu naisi watafulai wenzao wapo kabisa paris ufaransa
 
Itupieni humu hiyo list usije kuta imejaa majina kanyaboya tupu.............
 
Back
Top Bottom