KUTATABHETAKULE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 5,159
- 5,070
Toka jamaa adanganye kuhusu hali ya Mkuu mmoja kiafya, inatuwia vigumu wengi wetu kuamini ayasemayo.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
...Bilioni Tatu na ... Karibia Nne!Binafsi yangu, na toka siku nyingi sijawahi ona PM mwenye uelewa kidogo kama huyu ndugu. Kama kiongozi hesabu na takwimu zinakupiga chenga jua kuwa huwezi kuongoza hata kidogo. Kujua hesabu na takwimu ni muhimu mno.
Alisema msiba waliangalia watu bilioni sijui ngapi!!
Itoshe kujua kuwa wamasai walioko hifadhini Ngorongoro wametengewa eneo katika wilaya ya Handeni. Hayo manamba mtu yeyote anaweza akakosea. Binafsi huwa sielewi wanaposema kilomita za mraba maana yake ni nini na ni graduate.
Wamasai wapishe eneo tuboreshe hifadhi kwa maslahi mapana ya Taifa.
JESUS is CHRIST
mwezi watu na ijumaa nyingine kama ilivyokuwa mwaka jana tunaaminishwa mambo yasiyopo.Kwi Kwi Kwi
🤣🤣🤣🤣🤣 Nimecheka sana. Chakushangaza utawaona mpakani kwako wananyoosha vidole kuelekezana mpk unajiuliza Hawa watu wanaelekezana Nini mpakani kwangu? Kumbe fundi anaelekezwa nyumba itajengwa maeneo Gani na nyumba yako inatakiwa ivunjwe kabla ya ujenzi. Hii Dunia iache tu hasahasa ukiwa mnyongeNa unaweza shangaa serikali ilishaanza ujenzi wa nyumba kwenye eneo ambalo wataenda kuishi hata kabla ya makubaliano kuwa wataondoka au hawaindoki 😂!.
Yaani nimecheka sana, mtu anataka eneo lako hata kabla ya kuja mfanye bargain yeye anakuja na fundi wakiwa na ramani mpya jinsi ya kujenga asee, dunia simama nishuke 🤣!
Haki ya nani asee...🤣🤣🤣🤣🤣 Nimecheka sana. Chakushangaza utawaona mpakani kwako wananyoosha vidole kuelekezana mpk unajiuliza Hawa watu wanaelekezana Nini mpakani kwangu? Kumbe fundi anaelekezwa nyumba itajengwa maeneo Gani na nyumba yako inatakiwa ivunjwe kabla ya ujenzi. Hii Dunia iache tu hasahasa ukiwa mnyonge
Usitukumbushe machungu!! Kipindi hicho wanakata mbuga kwenye ziara kumbe msiba unatarajiwa muda wowote utangazwe! Watu wana roho ngumu!!!Katika watu siwezi kuwaamini ni huyo majaliwa namba moja aliwai kutudanganya kua jpm yupo anachapa kazi kumbe mzee aliishakata Moto.
Hayo majina 453 kati ya majina zaidi ya laki moja ni kama hakuna kitu, ni asilimia 0.42% ya wakazi 110,000 wa eneo linalotaka kutengwa!! Hata asilimia 1% haijafika!! SWerikali sikivu itafakari. ANGALIZO: Tujihadhari na kenya! maana wanashabikia sana!! Elimu zaidi itolewe na muda zaidi utolewe!! Waliokubali kuhama waanze hao kisha na wengine watafuata. Tujiwekee malengo ya miaka kama mitano hivi ili tuepuke vurugu zisizo za lazima!!Waziri mkuu mh Majaliwa leo amepokea orodha ya awali ya wananchi 453 walioomba kuhama kwa hiyari katika hifafhi ya Ngorongori.
Waziri mkuu amewaahidi wamasai hao kwamba serikali itawapeleka kuishi sehemu yoyote watakayoichagua wao wenyewe.
Source: ITV habari!
=====
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amepokea orodha ya majina ya awali ya kaya 86 zenye watu 453 ambao wamekubali kuondoka kwenye hifadhi ya Ngorongoro kwa hiari yao huku wengine wakiendelea kujiandikisha.
View attachment 2146074
View attachment 2146075
--
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amepokea orodha ya majina ya awali ya kaya 86 zenye watu 453 ambao wamekubali kuondoka kwenye hifadhi ya Ngorongoro kwa hiari huku wengine wakiendelea kujiandikisha.
Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi, Machi 10, 2022 na Ofisi ya Waziri Mkuu imesema kuwa, Majaliwa amepokea majina hayo baada ya kumaliza kikao na viongozi wa kimila wa jamii ya Kimasai (Laigwanak) kwenye mkutano uliofanyika eneo la Oretei Loongaik-Marya, kwenye Chuo cha Ufundi Arusha, jijini Arusha.
Hatua hiyo ni utekelezaji wa mazungumzo ambayo Waziri Mkuu aliyafanya na wadau wa uhifadhi kwenye vikao vilivyofanyika Februari 14 na 17 mwaka huu kwenye tarafa za Loliondo na Ngorongoro, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
Majina hayo yamekabidhiwa kwa Waziri Mkuu na Mkuu wa Mkoa wa Arusha (DC), John Mongela amesema majina hayo ni ya awali na tayari yalishahakikiwa mara baada ya wakazi hao kujiandikisha.
“Tutawasimamia vizuri hadi waende kule wapate hati za mashamba, nyumba na maeneo ya kulisha mifugo yao.”
Akizungumza na Malaigwanak hao zaidi ya 350, Waziri Mkuu amesema Rais Samia Suluhu Hassan alipofanya ziara mkoani humo aliliambia Taifa iko hatari ya kutoweka kwa hifadhi ya Ngorongoro ndani ya muda mfupi na akatoa maagizo viongozi waende kuwasikiliza wananchi juu ya hatua za kuchukua ili tunu hiyo isipotee.
“Ile hatari aliyosema Rais ni ipi? Zamani watu waliweza kuishi na wanyama bila tatizo kwa sababu kulikuwa na wakazi 8,000 tu wenye ng’ombe 20 hadi 30. Leo hii kuna wakazi 110,000 na mifugo zaidi ya 813,000 wakiwemo ng’ombe, mbuzi na kondoo.
“Zamani maboma yalikuwa yamesambaa lakini leo hii nyumba zimejaa, tena za bati na tofali. Idadi ya watu imeongezeka, idadi ya mifugo imeongezeka na makazi yameongezeka. Hakuna huduma za afya au shule wakati ni hitaji muhimu kwa wananchi.” imesema taarifa hiyo
Amewaeleza viongozi hao kwamba Serikali imetenga eneo la ekari 400,000 wilayani Handeni ambalo kati ya hizo, ekari 220,000 zimeshapimwa.
“Tumepima viwanja 2,406 ambapo kati ya hivyo, viwanja 2,070 tumeandaa kwa ajili ya makazi na kila kimoja kina ukubwa wa ekari tatu. Tumeanza na nyumba za kuanzia 101 za vyumba vitatu vya kulala kwa wale wanaotaka. Tuna viwanja 336 kwa ajili ya huduma kama shule za msingi na sekondari, zahanati na vituo vya afya. Ujenzi wa mifumo ya maji kazi inaendelea
“Umeme wa REA pia utakuwepo. Huku mlipo hakuna umeme. Haya tutayafanya na Mheshimiwa Rais Samia amesisitiza tuyafanye ili wananchi msipate bugudha,” imesema taarifa hiyo.
Taarifa hiyo imesema kuwa Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Wamasai Tanzania, Isack Ole Kisongo alisema kwa nafasi yao viongozi wa kimila wako tayari kushirikiana na Serikali kuhakikisha rasilimali za nchi zinawanufaisha Watanzania wote.
"Kwa kunyanyua rungu zetu tumekula kiapo kwa kukubali kuwa Ngorongoro na hifadhi nyingine nchini zilindwe kwa nguvu zote ili hadhi yake irudi kama zamani” imesema taarifa hiyo ikimnukuu kiongozi wa Wamasai nchini
Taarifa hiyo imesema kuwa Laigwanani wa Malaigwanani wa Ngorongoro, mzee Matengway Ole Tauwo alimweleza Waziri Mkuu kwamba anasubiri tarehe ya kuhamia huko kwa sababu ameenda hadi Handeni na ameona kwa macho yake kwamba mipango ya Serikali ina lengo zuri.
Waziri mkuu mh Majaliwa leo amepokea orodha ya awali ya wananchi 453 walioomba kuhama kwa hiyari katika hifafhi ya Ngorongori.