Waziri Mkuu apokea orodha ya majina 453 ya wananchi wa Ngorongoro waliokubali kuhama kwa hiyari yao

Toka jamaa adanganye kuhusu hali ya Mkuu mmoja kiafya, inatuwia vigumu wengi wetu kuamini ayasemayo.
 
...Bilioni Tatu na ... Karibia Nne!
 
Itoshe kujua kuwa wamasai walioko hifadhini Ngorongoro wametengewa eneo katika wilaya ya Handeni. Hayo manamba mtu yeyote anaweza akakosea. Binafsi huwa sielewi wanaposema kilomita za mraba maana yake ni nini na ni graduate.

Wamasai wapishe eneo tuboreshe hifadhi kwa maslahi mapana ya Taifa.


JESUS is CHRIST
 

Aisee
 
Tangu alipodanganya kuhusu kifo cha Jiwe sijawahi kumuamini huyu PM.

Na hicho pia kikanifanya walau nifatilie rekodi za hotuba zake na mishe zake nikaja kujua kua huyu mwamba ni muongo pro max.

Ni kama vile serikali au wakuu wake humtupia zigo la nnya na yeye hawezi kulimudu anaishia kudanganya tu.
 
Hizi pesa2 jamani.waachien watu mji wao mana hapo ndo ilipo asili ya wao
 
PM alifanya kosa kubwa sana kudanganya umma wa watanzania kuhusu kifo cha JPM

Hii dhambi itamtafuna mpaka kiama chake kimfike

Tangia wakati huo nimeshindwa kabisa kuwa na Imani nae
 
🤣🤣🤣🤣🤣 Nimecheka sana. Chakushangaza utawaona mpakani kwako wananyoosha vidole kuelekezana mpk unajiuliza Hawa watu wanaelekezana Nini mpakani kwangu? Kumbe fundi anaelekezwa nyumba itajengwa maeneo Gani na nyumba yako inatakiwa ivunjwe kabla ya ujenzi. Hii Dunia iache tu hasahasa ukiwa mnyonge
 
Haki ya nani asee...

Hebu fikilia, kumbe kuna jamaa masai 'inasemekana' haishi Ngorongoro na yupo mbele all ways PM akija Arusha but, ndiye anaongoza kutaka kuhamia huko handeni na masai wa Ngorongoro na Loliondo wanasema mbona kama hatuelewi 😂.

But wanatakiwa waelewe maana nyumba za kuamia tayari zinawekwa milango, ahahahaaaa aseee!.
 
Katika watu siwezi kuwaamini ni huyo majaliwa namba moja aliwai kutudanganya kua jpm yupo anachapa kazi kumbe mzee aliishakata Moto.
 
Yaani mtu uamke, uamue kuomba kuhamishwa kwa Hiari kutoka Boma lako?

Haya
 
Haijawahi kutokea kuwa watu wanajengewa nyumba kabisa ndipo wanahamishwa. Ubavu huu ni wa Oman kwa mjomba!
 
Katika watu siwezi kuwaamini ni huyo majaliwa namba moja aliwai kutudanganya kua jpm yupo anachapa kazi kumbe mzee aliishakata Moto.
Usitukumbushe machungu!! Kipindi hicho wanakata mbuga kwenye ziara kumbe msiba unatarajiwa muda wowote utangazwe! Watu wana roho ngumu!!!
 
Hayo majina 453 kati ya majina zaidi ya laki moja ni kama hakuna kitu, ni asilimia 0.42% ya wakazi 110,000 wa eneo linalotaka kutengwa!! Hata asilimia 1% haijafika!! SWerikali sikivu itafakari. ANGALIZO: Tujihadhari na kenya! maana wanashabikia sana!! Elimu zaidi itolewe na muda zaidi utolewe!! Waliokubali kuhama waanze hao kisha na wengine watafuata. Tujiwekee malengo ya miaka kama mitano hivi ili tuepuke vurugu zisizo za lazima!!
 

Huyu kiumbe ni muongo sana. Ni vigumu kuamini chochote anachosema. Afadhali angewaachia watu wengine waseme!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…