Waziri Mkuu apokea taarifa ya nyongeza ya mishahara, kuiwasilisha kwa Rais ambaye ataitangaza hivi karibuni

Waziri Mkuu apokea taarifa ya nyongeza ya mishahara, kuiwasilisha kwa Rais ambaye ataitangaza hivi karibuni

Mr Q

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
18,046
Reaction score
38,598
UPDATES. TAREHE 23/72022
WATUMISHI WALICHOKUTANA NACHO HAWATAKUJA KUSAHAU HIZI NGONJERA ZA KUPOKEA TAARIFA KWA MBWEMBWE MPAKA SERIKALI INATAKA KUTOA UFAFANUZI UPYA


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


WAZIRI MKUU APOKEA TAARIFA YA NYONGEZA YA MISHAHARA

*Aahidi kuikabidhi kwa Mheshimiwa Rais Samia wakati wowote

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea taarifa ya mapendekezo ya ongezeko la mishahara ya watumishi kutoka kwa timu ya wataalamu iliyokuwa ikiyaandaa kwa ajili ya kuiwasilisha kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Amepokea taarifa hiyo leo usiku (Jumanne, Mei 10, 2022) katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma. Kikao hicho kiliwahusisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba.

Viongozi wengine waliohudhuria kikao hicho ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Hamad Hassan Chande, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi pamoja na Makatibu Wakuu wa wizara hizo.

Mheshimiwa Majaliwa amesema taarifa hiyo imeonesha kwamba maandalizi ya mapendekezo ya ongezeko la mishahara yameshakamilika na kwamba wakati wowote atayawasilisha kwa Mheshimiwa Rais Samia ambaye atautangazia umma mabadiliko hayo yanayotarajiwa Julai mwaka huu.

Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia wananchi katika sherehe za maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani Jumapili Mei Mosi 2022 aliwahikikishia wafanyakazi nchini kuwa Serikali katika mwaka wa fedha 2022/2023 itaongeza mishahara kwa watumishi wake.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

S. L. P. 980,

41193 – DODOMA

JUMANNE, MEI 10, 2022.
 
Ni taarifa ya kipuuzi, haina maana wala mantiki, ni kuwachezea akili wafanyakazi. It is pure poor government propaganda.
Wafanyakazi wanataka nyongeza ya mishahara, hizo blah blah wawapelekee wake zao.
Wafanyakazi wenyewe hawana akili acha wachezewe
 
Kuwasilisha taarifa kutokea wapi? Kwani serikali haikua ina details za inachotaka kufanya?

Watu wa utumishi na fedha si wanajua plan ni ipi kwa asilimia gani ya kuongeza?

Taarifa ilivyokaa ni as if kulikua na utafiti wa kujua kiongezwe kipi?

Tabia ya kufanya kila kitu ni siasa kwa kutafuta political mileage ndio itatuondoa kwenye list ya nchi zinazojitambua. Too much politics!
 
Ina maana Mh Rais alivyoahidi mwaka jana hakuna hatua zilizofuata kwa watendaji kufanya utafiti wa nyongeza HADI IMESUBIRIWA JUZI BAADA YA TAMKO LA MAMA NDIO WAKAONA WAKAE. NILITEGEMEA TAARIFA HIYO INGESHAFANYIWA KAZI NA KUWASILISHWA KWA RAIS KABLA YA MEIMOSI.

RAIS WETU NI MZURI SANA LAKINI HILI KUNDI LA WASAIDIZI WAKE KWA KWELI KWA KWELI....
 
Najiuliza shida iko wapi mpaka nyongeza za wafanyakazi zikokotolewe as its kitu very special and confidential.
Tatizo lipo kwenye kibubu. Je kina pesa za kutosha?
 
Wafanyabiashara msituchukie bure....hatununui kwa sababu hatuna pesa
 
Hili eneo la ajira za Serikali linachangia Wizi wa fedha na Mali za nchi Kwa asilimia 80.

Kwanza ajira zimegubikwa na ujanja ujanja,udugu,urafiki,rushwa na a kila Aina ya upendeleo dhambi hiyo inaendelea mpaka kwenye post na kupandisha vyeo.

Tija ya wafanyakazi inazidi kufifia kungekuwa na vipimo vya Utendaji kazi Kwa kila mtumishi ni wazi ingebainika asilimia 60 wanalipwa mshahara na marupurupu ya bure.

Jambo la nyongeza ya mshahara halijaanza mei mosi na linajulikana kitaifa na kimataifa na ni sheria cha ajabu Leo inaundwa tume Kwa ghalama za nchi kujadili namna ya kupandisha mshahara Pia ni hisani!

Pamoja na kwamba nilikosa ajira lakini sijutii kabisa.
 
Back
Top Bottom