Waziri Mkuu apokea taarifa ya nyongeza ya mishahara, kuiwasilisha kwa Rais ambaye ataitangaza hivi karibuni

Waziri Mkuu apokea taarifa ya nyongeza ya mishahara, kuiwasilisha kwa Rais ambaye ataitangaza hivi karibuni

Hili eneo la ajira za Serikali linachangia Wizi wa fedha na Mali za nchi Kwa asilimia 80.

Kwanza ajira zimegubikwa na ujanja ujanja,udugu,urafiki,rushwa na a kila Aina ya upendeleo dhambi hiyo inaendelea mpaka kwenye post na kupandisha vyeo...
Mwenyewe niliajiriwa baada ya miezi 8 nikaacha maana niliona ni ujinga mtupu hakuna mwelekeo na utapelitapeli umejaa
 
Kazi kweli kweli!
Kumbe hakuna kilichokuwa kimefanyika? Tulitegemea kuwa tayari iko kwenye bajeti ya 2022/2023 kumbe ndiyo kwanza mapendekezo yanapelekwa kwa Rais?
 
Ni taarifa ya kipuuzi, haina maana wala mantiki, ni kuwachezea akili wafanyakazi. It is pure poor government propaganda.
Wafanyakazi wanataka nyongeza ya mishahara, hizo blah blah wawapelekee wake zao.
Nimecheka balaa ,,,Sasa makona yote hayo ya Nini bongo ina vituko sana
 
Mtadanganywa mpaka mpate akili
tena!wafanyeje sasa.nadhani wa kulaumiwa ni wawakilishi wao.wakiandamana watapigwa risasi.mmesahau ya lissu wala hata hakuandamana lkn maneno yake tu yalitaka kughalimu maisha yake.suluhisho ya haya yote ni katiba tu mfano mzuri kenya.

Ruto anachanja mbuga tu sababu katiba yao iko clear na ingekuwa tz angetolewa umakamu raisi,mfanoNdugai.katoa tu mawazo yake ambayo kimsingi ana haki lkn kilichotokea!tukomae na katiba.
 
Hehehee.......kwa hiyo hadi hiyo taarifa ipitiwe, ichakatwe, ichujwe, isagwe, iparuriwe, ifinyangwe, ichujwe na makorokoro mengine ndo mshahara uongezwe, itakuwa leo hiyo....
 
Hizi siasa hazitatupeleka popote kama taifa.!
 
Hii...ni taarifa mbichi kwa wafanyakazi,taarfa ambayo imekaa kisiasa.

Taarfa iliyoiva haiwezi kuwa ya namna hii.hii taarfa haina Tofauti na ile ya utatuzi wa ongezeko la bei ya mafuta.

Hapa ni Siasa, siasa! siasa!!
yaani tunazungushanaaaaa mara jambo lenu lipo, ooh hesabu zinaendelea, oooh kikao kinafanyika, mara oooh waziri mkuu kapokea hesabu, tena ooh katelefoni atamkabidhi Sam mapendekezo, ooh Sam atawatangazia yaani kama pasi za NETBALL....... wasi wasi tu mwanzo mwisho
 
Aongeze chochote kitu angalau kutuliza nafsi za watu, akili za wafanyakazi hazifanyi kazi tena miaka yote wanawaza ongezeko la mshahara.
 
Lile jambo letu lileeee,
Mahesabu yamekamilika,😋

Mungu awajaalie watumishi wameumia kwa muda mrefu.
 
Back
Top Bottom