Waziri Mkuu ashtushwa na taarifa ya Madereva wa Serikali kulogana ili wapate kazi

Black Butterfly

Senior Member
Joined
Aug 31, 2022
Posts
130
Reaction score
368
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameshtushwa na madai ya madereva wa Serikali kulogana ili wapate magari ya kufanyia kazi.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Juma Mtanda kwenye kongamano la tatu la madereva wa Serikali la mwaka 2024 linaloendelea jijini Arusha kwa siku nne mfululizo.

Mtanda amesema baadhi ya madereva wamekuwa wakilogana ili wapate magari ya kuendesha kutokana na vyombo vyao kuharibika na kuishia kukaa kwenye ajira wakilipwa mishahara bila kupangiwa majukumu, hivyo baadhi hufanya mambo hayo wapangiwe kazi.

Akizungumzia leo Agosti 20, 2024, Waziri Mkuu Majaliwa amewataka wakuu wote wa taasisi na waajiri kuhakikisha wanafanya tathimini ya magari yote ya Serikali yaliyoharibika na yatengenezwe, kuhakikisha madereva wote walioajiriwa wanapata vyombo vya kufanyia kazi.

"Mmh! hili la kulogana limenishtua sana, sijawahi kujua kwamba madereva mnafikia hatua ya kulogana ili mpate vyombo vya kufanyia kazi.”

"Hivyo sasa nitumie nafasi hii, kuwaagiza wakuu wote wa taasisi na waajiri waanze kufanya tathimini mapema sana ya kufufua magari ya Serikali yaliyoharibika ili madereva wapangiwe kazi wasilogane kugombea machache yaliyopo," amesema.

Mbali na hilo, amewataka waajiri kubainisha madereva waliopo kwenye taasisi zao ambao hawana vyombo vya kufanyia kazi au hawajapangiwa majukumu, ili Serikali iwatambue na kuwapangia kazi.

MWANANCHI
 
Ukute yeye mwenye ana dude linapua mfukoni hapo na ana namba ya 'mtaalam' wake kwenye speed dial halafu anajifanya kushangaa kuhusu kurogana.

1724165610119.png
1724165610119.png
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameshtushwa na madai ya madereva wa Serikali kulogana ili wapate magari ya kufanyia kazi.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Juma Mtanda kwenye kongamano la tatu la madereva wa Serikali la mwaka 2024 linaloendelea jijini Arusha kwa siku nne mfululizo.

Mtanda amesema baadhi ya madereva wamekuwa wakilogana ili wapate magari ya kuendesha kutokana na vyombo vyao kuharibika na kuishia kukaa kwenye ajira wakilipwa mishahara bila kupangiwa majukumu, hivyo baadhi hufanya mambo hayo wapangiwe kazi.

Akizungumzia leo Agosti 20, 2024, Waziri Mkuu Majaliwa amewataka wakuu wote wa taasisi na waajiri kuhakikisha wanafanya tathimini ya magari yote ya Serikali yaliyoharibika na yatengenezwe, kuhakikisha madereva wote walioajiriwa wanapata vyombo vya kufanyia kazi.

"Mmh! hili la kulogana limenishtua sana, sijawahi kujua kwamba madereva mnafikia hatua ya kulogana ili mpate vyombo vya kufanyia kazi.”

"Hivyo sasa nitumie nafasi hii, kuwaagiza wakuu wote wa taasisi na waajiri waanze kufanya tathimini mapema sana ya kufufua magari ya Serikali yaliyoharibika ili madereva wapangiwe kazi wasilogane kugombea machache yaliyopo," amesema.

Mbali na hilo, amewataka waajiri kubainisha madereva waliopo kwenye taasisi zao ambao hawana vyombo vya kufanyia kazi au hawajapangiwa majukumu, ili Serikali iwatambue na kuwapangia kazi.

MWANANCHI
Yeye anashangaa hili?
Kashtushwa yaani! Majaliwa Bhana! Yaani hakumbuki kwamba kule kwao ulitokea moshi wa ajabu hadi Jiwe akakimbizwa Bakwata!
Inashangaza Sana.

Mbona hata huko CCM Watu wamekuwa wakifanyiana uovu mbaya sana ikiwemo na kuwekeana sumu ili kugombea Vyeo na Madaraka, kwa nini hili halimshangazi?
 
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Juma Mtanda kwenye kongamano la tatu la madereva wa Serikali la mwaka 2024 linaloendelea jijini Arusha kwa siku nne mfululizo.
Serikali ina mambo ya kishamba sana. Kumbe kuna kongamano la madereva wa serikali.

Na ni kila mwaka.

Na linafanyika kwa siku nne.

Na wanatoka sehemu mbalimbali wanaenda kukusanyika sehemu moja.

Na Waziri Mkuu anaenda kuhutubia. Akiwepo mkuu wa mkoa wa Mwanza, wakiwa Arusha maana yake na mkuu wa mkoa wa Arusha yupo. Si ajabu na wakuu wengine wa mikoa.

Na anaambiwa wanarogana, anashangaa.
 
Back
Top Bottom