PostGE2025 Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu akutana na katibu mkuu wa TEC Padri Charles Kitima

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Hao hao, au hujasikia ishu ya EU kuzuia misaada?
Kwa nchi yenye nakisi "deficit" ya bajeti kwa 40% kitendo cha EU kupiga kura kuzuia misaada/mikopo ni pigo.
Kwani ni mara ya kwanza kufanya hilo?

Nukuu hili, siku zote hao wanacho jali ni interests zao si haki wala watu.
 
Kwani ni mara ya kwanza kufanya hilo?

Nukuu hili, siku zote hao wanacho jali ni interests zao si haki wala watu.

Lakini kuna fedha zinalenga kuimarisha utawala bora wanazitoa pia. EU hawatatoa ruzuku/misaada/mikopo kwa tukio la jana la upigaji kura. Msitegemee vitu hivyo toka kwa wanachama wao pia.
 
Lakini kuna fedha zinalenga kuimarisha utawala bora wanazitoa pia. EU hawatatoa ruzuku/misaada/mikopo kwa tukio la jana la upigaji kura. Msitegemee vitu hivyo toka kwa wanachama wao pia.
Siasa za dunia ziko hivyo, diplomasia itachukua nafasi.

Kama wangekasirika kabisa wangetoa balozi zao hapa nchini. Hizo ni hatua za kuonesha kuchukizwa na yalotokea, mpaka sasa EU wana taarifa za upande mmoja, serikali itawafikia na kuzungumza nao (kujieleza au kukiri udhaifu).

Jambo la muhimu, tuweze pata suluhu ya siasa zetu hapa ndani na maridhiano wenyewe, hayo mengine kama yatadumu sana sijui kama miaka miwili itaisha.
 
Deficit ni 28%

28% Deficit hiyo ni "tentative" ya mwaka huu yaani 2025-2026 yaani "kabla" ya mikopo/ruzuku/misaada na utekelezaji.
40% kwa 2024-2025 ni actual "baada" hiyo ni actual Deficit ya mwaka jana iliyoshindwa kufikiwa. Ipo miradi haikukamilika mwaka jana na imekuwa "forwarded" mwaka huu kama kiporo. Yaani maji yalizidi unga au pesa haikupatikana maana haitoki ndani. 😊
Ushauri: Japo sijajua naongea na mtu mwenye uelewa wa kiasi gani, lakini uwe unafuatilia taarifa ya utekelezaji wa bajeti kwa mwaka uliopita kabla bajeti mpya haijaanza kusomwa, na utajifunza juu ya actual and tentative Deficit.
 
Watamuua huyu father, aache tamaa za kuitwa ikulu.

Bora ajifiche huko alikokuwa.
 
Binadamu ni wasaaulifu, Mwigulu ni muuwaji mkubwa nchi hii.

Wakati akiwa waziri wa mambo ya ndani alikuwa akivaa mavazi ya jeshi, na ndicho kipindi aliuwa watu waliosemekana magaidi kule MKWIRU.

Hata kina Azori Gwanda walipitezwa na Mwugulu, huko mkuranga, kibiti, na lindi.
 
Kitima achana na WAHUNI hao watakuvunjia heshima ,walitaka kukuua then unawasogelea? Hakuna maridhiano baada ya uchaguzi ,walipewa muda wafanye reforms then ndiyo waitishe uchaguzi ,wakakaza MAFUVU.

Tumepoteza maelfu ya wazalendo kuanzia Mo29 hadi Nov 3 ,nani ataponye majeraha ya waliopoteza wapendwa wao? Toto Baya zuri kwa mama.

"Hakuna maridhiano baada ya uchaguzi ni uhuni" -Balozi Polepole
 
Wala sijamsahau huyu ndio mtu wa kwanza kuvaa kama Che Guevara kama anavyojifanya sasa Mchengerwa list ya matukio yao ipo na wala hawajasahaulika maana jinai haiozi.

Ambacho kwa sasa sikitambui ni huo uwaziri mkuu.
 
Si walishasema eti alikua tungi wakati anatekwa?
 
Na Wachina wamefika hapo baada ya kukataa kuendekeza dini za kuletewa kutoka kwa Wazungu na Waarabu. China mambo ya dini yanaishia kwenye nyumba za ibada hakuna cha mikutano ya injili wala mihadhara. Wao kazi ndiyo kipaumbele na utamaduni wao. Mambo ya kukuta mtu katega spika yake na kipaza sauti anahubiri mtaani kama ilivyo hapa kwetu huo ujinga hawautaki, nadhani ndiyo siri ya mafaniko yao.
 
... hata mimi sikubali kabisa mjadala wa mustakabal wa Taifa ujumuishe tu TEC na Serikali!
Inabidi jumuia zote zilizo na nyongo ziruhusiwe kuzitema ili muafaka utakaopatikana uwe JUMUISHI!
"Jumuia zote" Zilizobaki zimejaa wapumbavu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…