Waziri Mkuu: Dodoma itaendelea kuwa Makao Makuu ya Nchi. Ujenzi utaendelea

Tuache matusi njooni na hoja. Kuhamia Dodoma ulikua ujinga wa karne na umegharimu sana uchumi wa nchi.
Dodoma hakuna kitu kabisa mji umekufa na watu wake wote ni wachovu kabisa.
 
Dodoma ni marehemu hafufuki hata mumpake mafuta ya karsma.
Majumba mengi ya taasisi yapo Dar with high property values. Rudisha vitu Dar achana na maiti Dodoma.
Uwezo wako mdogo Sana wa kuona Mambo watanzania Kama nyinyi ndo hasara kwa taifa hili
 
Serikali ulikua na malengo mazuri mkuu kusogeza huduma karibu na wananchi Tanzania ni kubwa Dodoma ni katikati lakini pia kutawanya maendeleo sio kila kitu iwe Dar kwaio ondoa issue personal kwenye hili swala no mpango mzuri was kitaifa
 
Hakuwa na namna naye alikuwa anapokea tu, asingeweza kusema boss wake hatunaye kirahisi rahisi tu
 
Kwa iyo Ile miundo mbinu ibomolewe!?

Ifanyeni kuwa madarasa kuanzia chekechea mpaka vyuo vikuu. Dodoma liweni jiji la uwekezaji wa kielimu, utafiti wa Kisanyansi na Kitechnologia. Na centre ya kibiashara ya kanda ya kati.

Acheni kutapanya raslimali za nchi hovyo hovyo. Hili nilimpinga hata mwendazake akiwa hai na akanifokoe kwa njia ambayo nikaona niache maana nilisemea vya kutosha hakuwa wakubadili msimamo wake. Rejea ile hotuba yake pale kwenye uzinduzi wa ujenzi wa Ubungo flyover.

Dodoma ni kutapanya raslimali za nchi ambazo ni chache. Wapeleke fedha hizo kwenye mambo ya msingi boresheni huduma za afya, maji, umeme, kilimo, mifugo, uvuvi, mishahara ya Watumishi wa umma nk nk.

Huwezi kucreate soko kwa wakandarasi kwa staili hii ya kujenga Dodoma ukiacha majengo DSM ya kiishi popo na mijusi ukuta. Dodoma ndio hasara ya nchi ambayo Ndungai anatakiwa alete hoja iendelee ama isiendelee si ndege.

Nina hakika tunaosema Dodoma isiendelee tutakuwa wengi. Watakao sema iendelee wengi utakuta ni wakware wa kunyemelea ndoa za watu basi. Hivyo tu.
 
Huyu PM yuko vizuri sana,anafaa sana kwa urais,Mungu amjalie aweze kutimiza ndoto zake.Majaliwa is just a man of actions.

Huyu akiukwaa urais lazima mafisadi yasalimu amri,
 
Hahaha sasa akiomba radhi si ndiyo atakuwa kajitia kitanzi kabisa? Siasa za nchi hii ni ubabe ubabe tu!
 
Tunakosa vipaumbele kama taifa!! Majengo mazuri tunayaacha dar es salaam, tunaenda wekeza majengo mengine Dodoma!! Watoto wanakaa chini hakuna madarasa ya kutosha nchi nzima!! Naikumbusha serekali itambue baba was taifa alihitaji centralized government kwa kipindi kile na sio sasa dunia ya utandawazi!! Kalagabaho
 
Serikali ulikua na malengo mazuri mkuu kusogeza huduma karibu na wananchi Tanzania ni kubwa Dodoma ni katikati lakini pia kutawanya maendeleo sio kila kitu iwe Dar kwaio ondoa issue personal kwenye hili swala no mpango mzuri was kitaifa
point!
 
Serikali ulikua na malengo mazuri mkuu kusogeza huduma karibu na wananchi Tanzania ni kubwa Dodoma ni katikati lakini pia kutawanya maendeleo sio kila kitu iwe Dar kwaio ondoa issue personal kwenye hili swala no mpango mzuri was kitaifa
Yes ulikuwa mpango mzuri kwa miaka ile ya 70s kwani wakati ule sayansi na teknolojia ilikuwa haijaendelea. Wakati ule mawasiliano yalikuwa ya barua ambayo ilisafirishwa kwa gari kwa siku kadhaa wakati sasa kuna email na scanning ya barua ambapo kwa dakika chache mtu atatuma na kujibiwa, viongozi ilikuwa lazima wakutane kwa kuonana physically lakini sasa kuna simu mpaka za kiganjani ambapo mtu hata akiwa mahali popote atawasiliana kwa kuongea na mkutano wa video. Hiyo ni mifano michache lakini kwa ujumla dunia imekuwa kijiji na ipo kiganjani. Makao makuu hata yangekuwa Tunduma ni sawa tu kama mawasiliano yakiboreshwa vizuri zaidi.
 
Mama hataki kumuapiasha pm mwingine anamkubali sana pm wake

Ulitaka shughuli za bunge asimamie mama Samia

Pole Ila ndio uvumilie
Mama anamvumilia tu huku akijipanga for 2025 au akijistabilize kwenye throne
 
Huyu jamaa yuko busy na kutafuta urais. Hajajua kama tunae Rais. Nataka Mama amuapishe Pm wake.. Huyu jamaa kaapa kwa marehemu.
Wewe unataka kama nani?

Mama kashamuacha. Mtakufa mwaka huu kwa kihoro. Yupo hadi 2025.
 
Unaongea ukkiwa wapi maana mji wa serikali na majengo mengine bado vinajengwa.
Kwa hiyo pale Mtumba mnapoita Mji wa Serikali zile nazo nyumba? Kweli karne ya 21 tunajenga nyumba na mafundi washi na tunaziita nyumba.

Yale ni mabanda ya emergency yakiyojengwa kwenye vichaka vilivyo tapakaa vumbi.

Utakuwa ni UHAYAWANI kuendelea kuwekeza kwenye ule mji kwa majengo na barabara wakati kuna maofisi ya kisasa Dar es Salaam yanakaliwa na popo na mijusi tu.

Ushauri:
Waziri Mkuu, Wizara Kilimo, Wizara ya Mifugo na TAMISEMI ziendelee kubakia Dodoma. Zingine zirudi DSM

Wakati wa cabinet meeting Waziri na watendaji watakwenda DSM au inapobidi.
 
Huyu jamaa anachofanya nikumuekea mama maneno mdomoni sasa ili hashindwe kwenda atakavo mama badala ya kuongelea mambo ya wizara na mawaziri wake anaongelea kuhusu kubaki dodoma irrelevant. Hopeless kabsa.

Sent from my 601SO using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…