Waziri Mkuu: Hadi Februari, 2026 ajira 625,275 zimezalishwa

Waziri Mkuu: Hadi Februari, 2026 ajira 625,275 zimezalishwa

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema hadi kufikia Februari, 2026, fursa za ajira 625,273 zimezalishwa Tanzania ambapo kati ya ajira zilizozalishwa, ajira 242,656 za wazawa zilitokana na vibali 12,549 vilivyotolewa kwa wageni.

Mwigulu amesema hayo April 01, 2026 Bungeni Jijini Dodoma wakati akiwasilisha hotuba kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2026/2027.

Mwigulu amesema “Serikali imeendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ya kuratibu uzalishaji wa fursa za ajira nchini, mikakati hiyo ni pamoja na kubaini fursa kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali, kujenga mazingira wezeshi kwa Wawekezaji na kuimarisha ushirikiano baina ya Serikali na sekta binafsi”

“Hadi February, 2026, fursa za ajira 625,273 zilizalishwa, kati ya ajira zilizozalishwa, ajira 242,656 za wazawa zilitokana na vibali 12,549 vilivyotolewa kwa wageni sawa na uwiano wa mgeni 1 kwa wazawa 19 ikilinganishwa na uwiano wa mgeni 1 kwa wazawa 10 kama ilivyoainishwa katika Sheria ya kuratibu Ajira za Wageni, Sura 436”
 
Nikionaga neno "waziri mkuu" jina linalokuja kichwani mwangu ni "Kasimu majaliwa" ila nikisoma content nakuta majina ya ajabu ajabu sijui ni kushiba kwangu makande muda huu
 
Hakuna kiongozi hata Mmoja nchi hii aliye mkweli,
Mafisadi wote
 
Back
Top Bottom