Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akutana na Waziri Mkuu wa Morocco

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akutana na Waziri Mkuu wa Morocco

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Julai 13, 2021 kwa nyakati tofauti amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Africa wa Morocco Nasser Bourita na Waziri Mkuu wa Morocco Saad Dine El Otmani.

Katika Mzungumzo hayo Waziri Mkuu alizungumzia kuimarisha ushirikiano mzuri na wa kihistoria kati ya Tanzania na Morocco ulioasisiwa na kujengwa na wasasisi wa nchi hizi mbili Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mfalme Mohammed V.

Waziri Mkuu alisisitiza umuhimu wa nchi hizi kuendelea kushirikiana katika sekta mbalimbali ikiwemo Elimu, Kilimo, Utalii, Nishati na Uvuvi.

Katika mazungumzo hayo, Waziri Mkuu aliambatana na Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda, Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Zanzibar Leila Muhamed Mussa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk.
 
... sera ya Tanzania kwa sasa kuhusu Western Sahara (Saharawi) ni ipi?
 
Nchi masikini zote zimekutana
Ukikaa karibu na waridi hukosi harufu yake Chief. Morocco wakichungulia north mida ya jioni wanaona taa za jiji la Barcelona Mkuu.
 
Hahaha masikini tunaamini iliufanikiwe lazima utoe kafara, masikini kwa masikini hakuna mawazo positive zaidi ya kujadili namna ya kuongezewa ulinzi.
Kuamini kwamba kuna siku mzungu ndio atakaekuja kukujaza mihela ya maendeleo ni utahira mkubwa!

Jiulize wao walijazwa na nani mpaka wakafika hapo walipo?
 
Kuamini kwamba kuna siku mzungu ndio atakaekuja kukujaza mihela ya maendeleo ni utahira mkubwa!

Jiulize wao walijazwa na nani mpaka wakafika hapo walipo?
Hakuna sehemu nimetaja mzugu hayo yatakuwa mawazo yako tu ya kijinga
 
Back
Top Bottom