Uchaguzi 2020 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa apasua ngome ya Mbowe Hai

Wanasheria nisaidieni sielewi vizuri ,hivi mpaka mda huu bado baraza la mawziri lipo? najua kidogo rais bdo yupo may be bado na waziri mkuu akwa yupo vipi mawaziri wengine ? nauliza hivi nikimanisha majuzi nilimuona waziri flani kwenye mambo ya ajira
 
Wanafaidika vp kwa kumkubali Mbowe au ndio yaleyale ya ushabiki wa vyama tu kama tunavyoshabikia simba na yanga? Au ndio kuwakomoa CCM?

Yani siasa za bongo Mtu unaweza ukawa na uhakika wa kuchaguliwa kila uchaguzi hata kama hufanyi maendeleo yeyote kwenye jimbo lako.
 
Yaani reli , meli, madaraja viwanja vya ndege mpeleke lake Kisha mlete treni bovu na reli mbovu K'njaro.
 
Mbona walizomea kwenye mkutano wake mpaka polisi wakamsaidia kutoka mkutanoni? Au alikuwa Mbowe mwingine??
 
Wanasiasa bwana! Hivi Ruangwa Kuna maendeleo?

Hata barabara ya kuunganisha Ruangwa na Lindi haipo, lakini ukiwasikiliza utafikiri majimbo yote ya CCM yana maendeleo.
 
Bwashee kwa mbowe ninavyomfahamu na Hai ninavyoifahamu labda wakimbie na masanduku ya kura maana nimeishi Bomang'ombe kwa miaka 3, ninapafahamu vizuri MCC pale haitakiwi, labda kwa mbinu zile zingine za kimedani za CCM ndio watatoboa.
 
Namwamini Mbowe katika kuendesha kampeni za Ubunge wa Hai, Lakini nitamuamini zaidi kama atashinda uchaguzi wa 2020. Ni mgumu sana hapa Hai mwaka huu.

Na sababu ni moja tuu, Uongozi wote wa Kata, Tarafa na vijiji karibu vyote jimbo la Hai ni CCM na 90% ya Viongozi wote walikuwa wana chama wa Chadema.

Wanaogombea mwaka huu Hai ni Chadema na Chadema walioasi ambao wamejiunga na wana CCM kutaka kuchukua Jimbo. Kuna mtifuano. Tusubiri tuone.
 
Mbowe arudi kwenye kazi yake ya udj.
"kwaheri Mbowe,,,kwaheri Mbowe"
 
Ccm imefanya maendeleo gani kwa miaka karibia 60 ??
 
Ccm imefanya maendeleo gani kwa miaka karibia 60 ??
Sizungumzii vyama,hata ccm wapo watu ambao kila uchaguzi wanapita ila hakuna ambacho wananchi wanafaidika katika maendeleo,ndio maana nikahoji pia kwa Mbowe hao watu wanaomkubali ni kipi wananchofaidika?
 
Kuna vichwa vingi ambavyo siyo vya wapiga kura

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…