Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atembelea Chuo Kikuu cha Kilimo Belarus

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708
WhatsApp Image 2025-07-23 at 16.10.57_fb9a7dc5.jpg
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea Chuo Kikuu cha Kilimo cha Belarus (Belarusian State Agrarian Technical University - BSATU) na kufanya mazungumzo na viongozi wa chuo hicho wakiongozwa na Mkuu wa Chuo, Romaniuk Nikolai.

Mazungumzo hayo yamefanyika leo (Jumatano, Julai 23, 2025) kwenye ukumbi wa mikutano wa chuo hicho jijini Minsk ambapo masuala ya ushirikiano baina ya vyuo vikuu vya Tanzania vikiwemo vya Sokoine na DIT yalijadiliwa.

WhatsApp Image 2025-07-23 at 16.10.58_d7ebf423.jpg

WhatsApp Image 2025-07-23 at 16.11.00_92678ac7.jpg

WhatsApp Image 2025-07-23 at 16.11.00_748b651b.jpg
Waziri Mkuu aliwaeleza viongozi wa chuo kikuu hicho jinsi Serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ilivyoboresha sera ya elimu ambayo inataka elimu ya amali na stadi za ufundi ziwe sehemu muhimu katika mitaala ya mafunzo yanayotolewa nchini kote.

Aliwaeleza viongozi hao juu ya hati ya makubaliano kwenye sekta ya elimu iliyosainiwa jana mbele ya Waziri Mkuu wa Belarus na kwamba sasa ni wakati muafaka wa kuangalia namna ya kuandaa ziara za mafunzo, kubadilishana wanafunzi na wahadhiri ili kujengeana uwezo kwa pande zote mbili.

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo Kikuu cha BSATU, Bw. Romaniuk Nikolai alimhakikishia Waziri Mkuu kwamba chuo hicho kipo tayari kuanza majadiliano na viongozi kutoka Wizara ya Elimu ambao wamefuatana na Mheshimiwa Waziri Mkuu ili waone ni kwa namna gani wanaweza kuanza kutekeleza mambo yaliyojadiliwa.

Alimweleza Waziri Mkuu kwamba Chuo Kikuu hicho ambacho kilianzishwa mwaka 1954, kinaongoza nchini humo kwa kutoa mafunzo kwenye fani za uhandisi, uchumi na utawala na kinashirikiana na taasisi na mashirika rafiki 39 (affiliate organisations) yanayojihusisha na masuala ya kilimo na uundaji wa mitambo ya kilimo na zana za kisasa.
WhatsApp Image 2025-07-23 at 16.11.02_53cf5cd1.jpg

Alisema wanalenga zaidi fani za kitaalamu kwenye ufugaji wa wanyama na mitambo ya kilimo (animal husbandry and agricultural mechanisation) ambapo asilimia 70 ya mafunzo yanayotolewa chuoni hapo, hufanyika kwa vitendo (practicals) na kisha mwanafunzi anapewa wiki 28 za kwenda nje ya chuo kufanya mafunzo kwa vitendo (internship).

Mapema leo asubuhi, Waziri Mkuu alikutana na Wawakilishi wa Muungano wa Kampuni za Belarus zinazofanya biashara na mataifa ya Afrika (AFTRADE) kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli ya President.

Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Waziri Mkuu ameambatana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji wa SMZ, Bw. Shariff Ali Sharriff, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika wa Afrika Mashariki, Cosato Chumi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Khatibu Kazungu, Naibu Katibu Mkuu Kilimo, Dkt. Stephen Nindi na Balozi wa Tanzania nchini Urusi na Belarus, Balozi Fredrick Kibuta.
WhatsApp Image 2025-07-23 at 16.11.04_c987bdfa.jpg
 
watu Belarus wanaweza kuwa sirious wakidhani mgeni wao nae yuko serious kumbe yeye anatania, convoy ya ugeni wao wako bize na posho tu. Angetembea na wataalam wa kilimo ili akigeuza mgongo wao wanabaki kuendelea kuchota utaalam.
Bure kabisa.
 
Kile chuo kikuu chake cha Rwangwa kimeishia wapi
 
SERA YA MAMBO YA NJE YA TANZANIA

Kutoka Maktaba :

Tanzania yazidi kuvutia nchi za Ulaya ya Mashariki

24 October 2024

Tanzania yaigeukia mshirika mkuu wa Russia, nchi ya Belarus

1753282589253.jpeg

Waziri mkuu mheshimiwa Kassim Majaliwa amekutana na Balozi wa Belarus nchini Tanzania Pavel Vziatkin mwenye makazi yake Nairobi nchini Kenya kwa mazungumzo ya pande mbili kuhusu uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Katika kikao cha Alhamisi kilichofanyika katika Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam, Majaliwa aeleza dhamira ya Tanzania ya kuendeleza uhusiano wa nchi hizo mbili na Belarus kwa manufaa ya pande zote.

"Tanzania itaendelea kushirikiana na Belarus katika sekta ya madini, afya, utalii, kilimo na biashara kwa manufaa ya nchi zote mbili," ilisoma taarifa kutoka ukurasa rasmi wa Instagram wa Waziri Mkuu.

Mkutano huo unakuja siku mbili baada ya Balozi Vziatkin kufanya kikao cha maelewano na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Cosato Chumi, katika mji mkuu wa Dodoma.

Wawili hao walipendekeza kusaini Mkataba wa Maelewano (MoUs) na kubadilishana ziara ili kuimarisha kwa kiasi kikubwa uhusiano baina ya nchi hizo huku wakizingatia mienendo ya kimataifa.

Uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Belarus ulianza mwaka 1996 na kufikia kilele mwaka 2016 ambapo Oktoba 31, nchi hizo mbili zilifanya Kongamano la Biashara la Belarusi na Tanzania mjini Minsk, ambapo Mkataba wa Ushirikiano ulitiwa saini kati ya Kituo cha Taifa cha Masoko cha Belarus. Chemba ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA).

Mnamo mwaka wa 2017, Belarus iliwasilisha rasimu mbalimbali za Makubaliano kwa serikali ya Tanzania ili kuzingatiwa katika maeneo yanayohusiana na uhusiano wa nje, elimu na biashara. Walakini, hakuna habari inayoonyesha kuwa serikali hizo mbili zilikamilisha Makubaliano haya kuanzia leo.

Mnamo Januari mwaka huu, ujumbe wa wafanyabiashara kutoka Belarusi na wawakilishi kutoka Chemba ya Wafanyabiashara wa Belarusi waliitembelea Tanzania. Walikutana na wenzao kutoka Chemba ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA). Ujumbe huo ulionyesha nia ya kushirikiana na wafanyabiashara wa Tanzania.

Kiwango cha biashara kati ya nchi hizo mbili bado ni cha kawaida. Ilifikia kilele mwaka 2017 wakati Tanzania ilipouza nje bidhaa zenye thamani ya dola milioni 46.6 na kuagiza takriban dola za Marekani milioni 1.3 kutoka Belarus. Hata hivyo, uhusiano wa kibiashara unaonekana kupungua, ambapo Tanzania iliuza nje dola za Marekani milioni 4.8 na kuagiza dola milioni 4 mwaka 2021
 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea Chuo Kikuu cha Kilimo cha Belarus (Belarusian State Agrarian Technical University - BSATU) na kufanya mazungumzo na viongozi wa chuo hicho wakiongozwa na Mkuu wa Chuo, Romaniuk Nikolai.

Mazungumzo hayo yamefanyika leo (Jumatano, Julai 23, 2025) kwenye ukumbi wa mikutano wa chuo hicho jijini Minsk ambapo masuala ya ushirikiano baina ya vyuo vikuu vya Tanzania vikiwemo vya Sokoine na DIT yalijadiliwa.
Waziri Mkuu aliwaeleza viongozi wa chuo kikuu hicho jinsi Serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ilivyoboresha sera ya elimu ambayo inataka elimu ya amali na stadi za ufundi ziwe sehemu muhimu katika mitaala ya mafunzo yanayotolewa nchini kote.

Aliwaeleza viongozi hao juu ya hati ya makubaliano kwenye sekta ya elimu iliyosainiwa jana mbele ya Waziri Mkuu wa Belarus na kwamba sasa ni wakati muafaka wa kuangalia namna ya kuandaa ziara za mafunzo, kubadilishana wanafunzi na wahadhiri ili kujengeana uwezo kwa pande zote mbili.

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo Kikuu cha BSATU, Bw. Romaniuk Nikolai alimhakikishia Waziri Mkuu kwamba chuo hicho kipo tayari kuanza majadiliano na viongozi kutoka Wizara ya Elimu ambao wamefuatana na Mheshimiwa Waziri Mkuu ili waone ni kwa namna gani wanaweza kuanza kutekeleza mambo yaliyojadiliwa.

Alimweleza Waziri Mkuu kwamba Chuo Kikuu hicho ambacho kilianzishwa mwaka 1954, kinaongoza nchini humo kwa kutoa mafunzo kwenye fani za uhandisi, uchumi na utawala na kinashirikiana na taasisi na mashirika rafiki 39 (affiliate organisations) yanayojihusisha na masuala ya kilimo na uundaji wa mitambo ya kilimo na zana za kisasa.

Alisema wanalenga zaidi fani za kitaalamu kwenye ufugaji wa wanyama na mitambo ya kilimo (animal husbandry and agricultural mechanisation) ambapo asilimia 70 ya mafunzo yanayotolewa chuoni hapo, hufanyika kwa vitendo (practicals) na kisha mwanafunzi anapewa wiki 28 za kwenda nje ya chuo kufanya mafunzo kwa vitendo (internship).

Mapema leo asubuhi, Waziri Mkuu alikutana na Wawakilishi wa Muungano wa Kampuni za Belarus zinazofanya biashara na mataifa ya Afrika (AFTRADE) kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli ya President.

Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Waziri Mkuu ameambatana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji wa SMZ, Bw. Shariff Ali Sharriff, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika wa Afrika Mashariki, Cosato Chumi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Khatibu Kazungu, Naibu Katibu Mkuu Kilimo, Dkt. Stephen Nindi na Balozi wa Tanzania nchini Urusi na Belarus, Balozi Fredrick Kibuta.
Mwendo wa perdiem tu hamna chochote
 
Kuna watu matumbo yanauma na kuunguruma wakisikia jina la Dr Samia Suluhu Hassan, The Mother of Modern Tanzania
 
..huu ni WIZI.

..ziara hiyo ilipaswa kufanywa na Waziri Mkuu mpya, sio huyu aliyetangaza kujiuzulu.
 
ugomvi mwingine ni wa kujitakia tu, belarus imewekewa sanctions na kutengwa na dunia nzima isipokuwa urusi halafu tanzagiza wanakwenda huko ? …
 
Mama samia anazidi kuifungua nchi. Rais ajaye baada ya Samia atakuta nchi imefunguliwa kila sehemu.

Back
Top Bottom