Waziri Mkuu Kassim Majaliwa avamia mwendokasi, ahoji mapato yalipo kama wanashindwa kununua mabasi. Mkurugenzi wa fedha atumbuliwa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa avamia mwendokasi, ahoji mapato yalipo kama wanashindwa kununua mabasi. Mkurugenzi wa fedha atumbuliwa

Waziri Mkuu hapo anaenda hii sijui mara ya tatu kila siku changamoto haziishi na anataka kutatua kwa makamera kazi ipo...Kuna kitu kimejificha hapo apeleke Timu ya ukaguzi tupate majibu ya kitaalamu sio haya ya kisiasa.
Na Wizara ya TAMISEMI inayomiliki huo mradi, Katibu Mkuu yupo, Waziri yupo sasa hivi kabadilishiwa tu wizara ili nako akavuruge kama alivyovurunda TAMISEMI.

Nchi haina kuwajibishana, ni matukio tu baada ya matukio bila matokeo na yanajadiliwa kama SOGA tu vijiweni.
 
Hii yote ni kwa sababu hatuna mfumo maalumu wa kuendesha nchi,rejea Asskofu Gwajima bungeni last week.

Waziri mkuu anajaribu kufata nyayo za boss wake wa zamani ili kuonyesha watanzania bado wanafanya kazi.

Sikatai ni jambo jema lakini bado tupo nyuma sana sana kama mambo yenyewe ndiyo haya.

Nilitegemea Rais Samia aje na ajenda yake ya kiutendaji kuliko haya mambo ya kujaribu kokopi na kupesti ili kuridhisha wananchi
bado sana.

Si kweli kuwa Hayati Rais Magufuli alianzisha huu mtindo. Nyerere na Kawawa walikuwa wakifanya hivyo mara kwa mara, sema tu wakati ule ufisadi na ubadilifu wa mli za umma ulikuwa bado haujatamalaki.

Waziri mkuu Moringe Sokoine ndiye aliye jitokeza sana katika hii ya kusaka walanguzi. Maneno kama ufisadi na ubadilifu wa mali za umma hakutumika bado. Tulikuwa tunauita ulanguza. Na watendaji walikuwa walanguzi. Ndiyo slogan yetu wakati ule.
 
Huyo eng lwakatare anakunywa chai tuu hapo, hadi mwendo kasi unakatibia kuwa sehemu ya taka za jiji.

Hadi leo kwnye vituo vya mabasi hakuna TV wala matangazo ya biashara.

Vyoo vichafu utadhani hakuna Director,

Uzio kimara umeharibika jamaa anacheka tuu

Kituo cha kikara kilitakiwa kukamilishwa kwa kujengwa kituo cha daladala kama ilivyo morocco na katiakaoo lakini hadi leo hollaaaa.

Aondolewe tuu, awekwe mtu ambaye ji business minded
 
Hayo mabasi 100 yanafanya kazi barabara zipi aisee?? Abiria wanajazana kituoni mabasi hayaji halafu mnasema mabasi yaliyo barabarani ni 100,aah wapi?

Mwendokasi ubabaishaji ni mkubwa sana, mfumo wa kuonesha tiketi kwenye mashine umekufa zaidi ya miaka 2 sasa na hakuna hatua zinazochukuliwa.

Mabasi yanayofanya kazi ni machache na hayo machache madereva wanapaki wanavyotaka..utasikia derava anakunywa chai, mara anapumzika nk
Sidhani hata 50 yanafika hayo mabasi yanayofanya kazi,ushenzi mtupu!
 
Pale Mwanza kwenye kivuko cha Busisi/Kigongo tikeni huwa zipo nyingi sana mezani wanachukua na kumpa abiria, nina wasiwasi kama tiketi zile hazina magumashi.
 
Tunarudi kule kule. Haya mambo si ya kuulizana jukwaani. Angemwita yeye na viongozi wake ili wakae waone tatizo liko wapi. Kama ni uongozi lingeonekana tu.

Na kama ni serikali ingeonekana tu maana Meneja angeweza kusema kweli yake bila kuonekana kuwa anamdhalilisha WM hadharani. Inabidi viongozi wakuu wabadilike.

Amandla...
Usiri wa nini? Sisi ndio walipa kodi,lazima tujue kinachoendelea,staha kumfanyia mwizi ni dhambi sana.
 
Yale yaliyokwama sababu ya ushuru vipi kulikoni walishayakomboa?
 
Tunarudi kule kule. Haya mambo si ya kuulizana jukwaani. Angemwita yeye na viongozi wake ili wakae waone tatizo liko wapi. Kama ni uongozi lingeonekana tu.

Na kama ni serikali ingeonekana tu maana Meneja angeweza kusema kweli yake bila kuonekana kuwa anamdhalilisha WM hadharani. Inabidi viongozi wakuu wabadilike.

Amandla...
Wewe ndo unakosea.. Waziri amefanya "Surprise Visiti" ina maana atakuwa na taatifa za awali, hapo n kwenda kuhakikisha tu. Yote aliyoyasema ni kweli tupu. Mfano mashine zilikuwa nzima sasa zimekufa na hakuna hatua yoyote
 
Tatizo la huyu anakopitaga huwa hamna impact yoyote. Kama kiki tu.
 
Usiri wa nini ?,sisi ndio walipa kodi,lazima tujue kinachoendelea,staha kumfanyia mwizi ni dhambi sana
Mtajua kinachoendelea kwa kusikiliza upande mmoja?

Mnadhani jamaa alishindwa kujibu kwa sababu tu hakuwa na majibu?

Na wangapi kati yetu wanaweza kuelewa financial report hata tukisomewa?

Kwani ni Mkurugenzi aliyezuia MaxMalipo kukata tiketi?

Na je yeye ana mamlaka gani ya kutafuta vendor mwingine?

Kwani ni Mkurugenzi ndie aliyelazimisha Depo ijengwe Jangwani ( ukiangalia hayo mabasi uharibifu mkubwa umetokana na matope yaliyosababishwa na mafuriko)?

Mabasi 70 yamekamatwa na TRA, serikali ilifanya juhudi gani kuyakwamua ili yatoe huduma?

Nani alipanga hiyo nauli na je inatosha kulipa madeni, kuendesha shirika, kufanyia maintenance mabasi yaliyopo na kununua mapya?

Tiketi ngapi za kufoji zimekamatwa? Na walioshikwa nazo wamechukuliwa hatua gani?

Kweli unategemea maswali yote haya yajibiwe katika ziara ya kustukiza?

Due process ina maana yake. Tunachotaka ni haki itendeke bila upendeleo wowote.

Amandla...
 
Wewe ndo unakosea.. Waziri amefanya "Surprise Visiti" ina maana atakuwa na taatifa za awali, hapo n kwenda kuhakikisha tu. Yote aliyoyasema ni kweli tupu. Mfano mashine zilikuwa nzima sasa zimekufa na hakuna hatua yoyote
Hizi mashine hazikuharibika jana wala juzi. Wote wanajua hilo.

Amandla...
 
Tunarudi kule kule. Haya mambo si ya kuulizana jukwaani. Angemwita yeye na viongozi wake ili wakae waone tatizo liko wapi. Kama ni uongozi lingeonekana tu.

Na kama ni serikali ingeonekana tu maana Meneja angeweza kusema kweli yake bila kuonekana kuwa anamdhalilisha WM hadharani. Inabidi viongozi wakuu wabadilike.

Amandla...
Unatetea ujinga.

Hivi kweli kuosha na kusafisha matope ndani ya mabasi kunahitaji kikao?

Kununua mabasi mapya unahitaji kuuliza?

Hivi kweli kugawa tiketi kunahitaji maamuzi?

Hii ni ujinga ndani ya biashara.

Huyu anazidiwa hata na konda wa daladala anajua wajibu wake.

STD 7 vs PhD manager.
 
Hii miradi wanaiua wenyewe.

kule vivukoni ukiwa mtu wa kitengo unavuka free hulipi hata sent moja.

risiti zinakatwa lakini mashine hazisomi.

mm walipowatoa tu wale maxmalipo nikajua apa tayari tumeinamishwa.

cio bure lzm kuna wanaofaidika na upuuz huu.
 
Hizi ni politicking tu. Walivyowaondoa MaxMalipo na kusema tunawapa kazi TTCL kutengeneza mfumo wa malipo, nilishangaa! Wana huo uwezo?

Leo Waziri Mkuu anakuwa kama ndio kaanza kazi jana! Wakazi wa Kimara wamelalamika mpaka wameamua kukaa kimya, ndio Majaliwa anaenda kuleta siasa. Hayo mabasi yaliyozuiwa na TRA yameleta faida gani huko? Si ni bora yangekuwa yanasaidia wananchi na wakati huo huo yanalipa hiyo kodi.

Tuna safari ndefu sana
 
Unatetea ujinga.

Hivi kweli kuosha na kusafisha matope ndani ya mabasi kunahitaji kikao?

Kununua mabasi mapya unahitaji kuuliza?

Hivi kweli kugawa tiketi kunahitaji maamuzi?

Hii ni ujinga ndani ya biashara.

Huyu anazidiwa hata na konda wa daladala anajua wajibu wake.

STD 7 vs PhD manager.
Ni kweli suala la matope halipendezi lakini kisichopendeza zaidi ni kuwa hayawezi kutembea. Hilo ndio swali la kuulizwa kwenye kikao.

Mabasi mapya yamenunuliwa lakini yameshikwa na TRA. Hivi kweli serikali ilishindwa kukubaliana na shirika ili walipe deni lao taratibu. Kumuachia TRA ayazuie kufanya biashara ni kuwa myopic.

Mfumo ulikuwepo lakini wahusika wakatimuliwa. Mpaka sasa hajapatikana mwengine. Kikao ndio kingeainisha nani aliwajibika kupata vendor mwingine.

Hilo la std 7 siwezi kulisemea maana mimi std 7 na ninajijua kabisa kuna maeneo siwezi kushindana na Ph.D au mtu mwenye MBA.

Amandla...
 
Shida yetu tunatanguliza kumkamata mchawi badala ya kutafuta utatuzi wa tatizo.

Amandla...
 
Back
Top Bottom