Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo amefanya ziara ya kushtukiza kituo cha mwendokasi eneo la gerezani na kukuta mfumo wa kusoma tiketi haufanyi kazi, mtendaji mkuu alisema mfumo haufanyi kazi baada ya kutokea mgogoro kati ya supplier na alieununua. Meneja huyo amesema mfumo mpya unajengwa na waziri mkuu kumuhoji inatumia miaka mingapi kukamilika?
Majaliwa amesema wanaibiwa mapato kwani wao wanatumia mtambo na wengine wanatumia mtambo mwingine na hawana namna ya ku-check.
Pia Meneja amehojiwa tangu aingie amenunua mabasi mangapi baada ya serikali kununua mabasi 140 huku mabasi yanayokadiriwa kuwa barabarani ni wastani wa 100.
Mtoa huduma ya mwendokasi aliagiza mabasi 70 ambayo yamekwama kuingia barabarani kutokana na mgogoro na waziri mkuu akasema anaenda kuyaona. Majaliwa amesema wananchi wanalalamika mabasi hayatoshi akitolea mfano Kimara watu wanaingilia dirishani na kuhoji mapato wanayokusanya wanapeleka wapi kama wanashindwa kununua mabasi.
Pia waziri mkuu amepita karakana ya Jangwani na sasa anaelekea Ubungo kuangalia mabasi yenye mgogoro