Waziri Mkuu Kassim Majaliwa avamia mwendokasi, ahoji mapato yalipo kama wanashindwa kununua mabasi. Mkurugenzi wa fedha atumbuliwa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa avamia mwendokasi, ahoji mapato yalipo kama wanashindwa kununua mabasi. Mkurugenzi wa fedha atumbuliwa

Maskini hujui usemalo. Mwendokasi tangu mwanzo ulikuwa mradi uliokufa kabla ya kuanza kazi hasa ikizingatiwa kuwa akina SImon Kisena waliopoka UDA waliishauua. Magufuli amesaidia hata kufikia hapo ulipo baada ya kuwakamata na kuwasweka ndani akina Kisena. Kama hujui uliza ujuzwe badala ya kuja na mambo ya ajabu ajabu yaliyojaa ujinga na uongo.
Kama ulikuwa umekufa tangu mwanzo Mbona mwanzoni hakukuwa na shida na mradi ulikuwa unaenda vizuri?
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo amefanya ziara ya kushtukiza kituo cha mwendokasi eneo la gerezani na kukuta mfumo wa kusoma tiketi haufanyi kazi, mtendaji mkuu alisema mfumo haufanyi kazi baada ya kutokea mgogoro kati ya supplier na alieununua. Meneja huyo amesema mfumo mpya unajengwa na waziri mkuu kumuhoji inatumia miaka mingapi kukamilika?

Majaliwa amesema wanaibiwa mapato kwani wao wanatumia mtambo na wengine wanatumia mtambo mwingine na hawana namna ya ku-check.

Pia Meneja amehojiwa tangu aingie amenunua mabasi mangapi baada ya serikali kununua mabasi 140 huku mabasi yanayokadiriwa kuwa barabarani ni wastani wa 100.

Mtoa huduma ya mwendokasi aliagiza mabasi 70 ambayo yamekwama kuingia barabarani kutokana na mgogoro na waziri mkuu akasema anaenda kuyaona. Majaliwa amesema wananchi wanalalamika mabasi hayatoshi akitolea mfano Kimara watu wanaingilia dirishani na kuhoji mapato wanayokusanya wanapeleka wapi kama wanashindwa kununua mabasi.

Pia waziri mkuu amepita karakana ya Jangwani na sasa anaelekea Ubungo kuangalia mabasi yenye mgogoro


Namsikia mtangazaji wa kike kwa sauti ya kulembua nahisi anamkoga PM kuwa huduma zipo sawa bila kujua mwenzao anataarifa zao zote kuhusu madudu yao
 
Hujui kuwa wanatumia ticket na zinakatwa?? Hujui mwanzoni kulikuwa na kadi na watu walikuwa wanaswap na mapato yanasoma???

Uko chato au Burundi?
Hakuna kukatavtiketi kama daladala, hakuna konda UDART. Mwongo mkubwa.
 
Ufisadi upi ulikuwepo?? Acheni kuchukia matajiri ndo mana mnakuwa masikini na makapuku milele!
Umejuaje mimi ni maskini? Umejuaje nachukia matajiri? Kusema huu mradi ulikuwa wa kifisadi ndiyo nimechukia matajiri? Nachukia mafisadi siyo matajiri.
 
Nilikuwa siamini kwamba kwenye kila analogusa Magufuli huwa ana haribu Ila kwenye Mwendokasi ndo sehemu niliyokuja kuamini kwa Mara ya kwanza!

Kwanza inabidi wote tujiulize mwendokasi ilianzia wapi?

Mradi wa mabasi ya mwendokasi ukianzishwa na kuasisiwa na Rais wa Awamu ya nne. Kwa Jinsi mradi ulivyokuwa umeandaliwa ulitakiwa kusimamiwa na kampuni binafsi na tangu mwanzo ulisimamiwa kwenye mfumo huo. Mradi huu ulikuwa chini ya Kampuni na Kisena na wakati unaanza kila kitu kilikuwa kinaendeshwa katika dunia ya kisasa. Ticket zilikatwa kielectronic na watu waliweka hadi kuwa na kadi ya kutumia mwezi mzima.

Alipokuja Magufuli kwanza alianza ku deal na kisena kwa sababu kisena hakuwa kwenye kundi la watu waliomuunga mkono kwenye uchaguzi wa mwaka 2015. Alimtesa kisena kumpa kesi za uhujumu uchumi na mkewe na baadae kumnyang’anya mradi na hatimaye akaondoa utaratibu wote mzuri uliokuwa umewekwa kwa ajiri ya kuendesha mradi.

Matokeo yake akawapa wanajeshi, na hapo ndo Tatizo lilipoanza. Mradi ulianza kuendeshwa kwa tabia za kiswahili na watu wakaanza kukata ticket kama daladala.

Mradi huu hadi kufikia sasa ulitakiwa uwe umeshaanza kujiendesha kwa faida Ila kwa roho mbaya ya magufuli na tabia zake za kuchukia matajiri ndo amefanya mradi ule uwe kituko na usifike popote.

Polee kisena. Buriani Mwendokasi.
Kuna watu mnaidhalilisha jamii forum kwa kudandia vitu msivyovifahamu au kwa kutumwa kuwasifia watu. Mjitahidi kabla ya kuandika masuala makubwa kama haya ili kuepuka upotoshaji mnatakiwa kufanya utafiti siyo kuandika mkiongozwa na chuki. Zamani niliamini JF ni sehemu ya kuoata habari za kiuchunguzi lakini imegeuka kuwa jukwaa la wambea na wafitishi kwa habari za kutunga kama hizi.
 
Sasa mmemuondoa na mradi umewafia. Hiyo ni akili au matope?
Wewe unaweza kuwa unaongozwa na ujinga. Unataka ku-suggest kuwa watu hata wakiiba ilimradi wanakwenda kufanya vizuri basi tusiwahesabu kuwa wana makosa? Unatumia nini kufiri wewe? Au wewe ndiye huyu mwizi? Au mke wake?
 
Nyuma ya kisena kuna rizi-1, juhudi kubwa sana zinafanyika kuirudisha miradi ya kifisadi ya Kikwete iliyo chinjiwa baharini na Makufuli, kosa kubwa alilofanya Makufuli ni kutowanyonga haraka haraka Kisena, Rugemalila na Sethi
Ehehh

Ova
 
Maskini hujui usemalo. Mwendokasi tangu mwanzo ulikuwa mradi uliokufa kabla ya kuanza kazi hasa ikizingatiwa kuwa akina SImon Kisena waliopoka UDA waliishauua. Magufuli amesaidia hata kufikia hapo ulipo baada ya kuwakamata na kuwasweka ndani akina Kisena. Kama hujui uliza ujuzwe badala ya kuja na mambo ya ajabu ajabu yaliyojaa ujinga na uongo.
Eti anamlaumu jpm,wakati jpm alijaribu kuirudisha mwendokasi kwenye mstari
Sema ndiyo hivyo

Ova
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo amefanya ziara ya kushtukiza kituo cha mwendokasi eneo la gerezani na kukuta mfumo wa kusoma tiketi haufanyi kazi, mtendaji mkuu alisema mfumo haufanyi kazi baada ya kutokea mgogoro kati ya supplier na alieununua. Meneja huyo amesema mfumo mpya unajengwa na waziri mkuu kumuhoji inatumia miaka mingapi kukamilika?
Kaza boot Majaliwa
 
Kuna mtu anasikika anasema mabasi yameharibiwa na corona😀🤣 kiti moto sakafu moto
 
Kazi kazi.

mapigaji yanataka kurudi.

safi sana waziri mkuu
Sijui kama unaelewa.
Upigaji huu upo miaka yote, sio mwendokasi pekee hata vivuko mtindo ni huu huu wa kuchana tiket badala ya ku scan.
 
Back
Top Bottom