Waziri Mkuu Kassim Majaliwa avamia mwendokasi, ahoji mapato yalipo kama wanashindwa kununua mabasi. Mkurugenzi wa fedha atumbuliwa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa avamia mwendokasi, ahoji mapato yalipo kama wanashindwa kununua mabasi. Mkurugenzi wa fedha atumbuliwa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo amefanya ziara ya kushtukiza kituo cha mwendokasi eneo la gerezani na kukuta mfumo wa kusoma tiketi haufanyi kazi, mtendaji mkuu alisema mfumo haufanyi kazi baada ya kutokea mgogoro kati ya supplier na alieununua. Meneja huyo amesema mfumo mpya unajengwa na waziri mkuu kumuhoji inatumia miaka mingapi kukamilika?

Majaliwa amesema wanaibiwa mapato kwani wao wanatumia mtambo na wengine wanatumia mtambo mwingine na hawana namna ya ku-check.

Pia Meneja amehojiwa tangu aingie amenunua mabasi mangapi baada ya serikali kununua mabasi 140 huku mabasi yanayokadiriwa kuwa barabarani ni wastani wa 100.

Mtoa huduma ya mwendokasi aliagiza mabasi 70 ambayo yamekwama kuingia barabarani kutokana na mgogoro na waziri mkuu akasema anaenda kuyaona. Majaliwa amesema wananchi wanalalamika mabasi hayatoshi akitolea mfano Kimara watu wanaingilia dirishani na kuhoji mapato wanayokusanya wanapeleka wapi kama wanashindwa kununua mabasi.

Pia waziri mkuu amepita karakana ya Jangwani na sasa anaelekea Ubungo kuangalia mabasi yenye mgogoro

==========

UBUNGO: Kinachoendelea waziri mkuu anauliza hatua zinazoweza kuchukuliwa kwa mabasi yaliyokwama ambapo mtu TRA anasema sheria inamruhusu kamishna kuya-donate au kuyaharibu na waziri mkuu amesema hawezi kupewa Shabiby kwasababu hayamfai kwenda Dodoma kwani ni kwaajili ya barabara za mwendokasi na sasa anauliziwa mwanasheria

Pia waziri mkuu anawaambia forodha waendelee kufanya minada ya mizigo iliyokaa kupita kiasi mara kwa mara ili kusafisha nafasi ya kuagiza mizigo mingine na kuwataka wabadilike kwani baadhi ya wateja wanalalamika process zinachukua muda mrefu

Kassim Majaliwa anasema pesa zilizotumika zimekopwa world bank na zinalipwa na mabasi yameletwa na mjasiriamali laiki ameshindwa ku-comply na sheria na sheria zimechukua mkondo wake tangu 2018 na kutaka kesho wakae waamue

Majaliwa amesema serikali inao uwezo wa kununua mabasi lakini tatizo ni usimamizi na hawawezi kumsimamia msimamizi ambae hawezi na leo amemuweka pembeni mkurugenzi wa fedha na mwingine anamuachia Rais kwani yuko kwenye mamlaka yake.

Hii ndio Tanzania watu wachache wanayoitaka. Kuiba mali ya umma. Nakupongeza sana PM wetu kwa kuendelea kukazia. Wizi wa mali ya umma unatusononesha sana wananchi wa kawaida. Unajenga chuki na serikali. Wezi wa mali ya umma sasa wawe wanawajibishwa. Sio kuwalea kama watoto wa faru john. Hawana tija na nchi yetu na hawastahili kukamata ofisi za umma
 
Hujui kama jamaa wana mkopo mkubwa....
usirukie vitu usivyojua utapasuka msamba
Tatizo humu jamvini kuna raia mnajiona mnajua everything but they don't know everything! Inaamaana wazir mkuu amekurupuka? Hujasikia akiwalaumu kua wameshindwa hata kununua magari mengine na kampuni inaenda kufa? Kasome vzr maneno ya prime minister ndo urud hapa. Kwamba unamaanisha hata wazir hajui kama wana mkopo??
 
TANZANIA ni ile ile.......tufanye kazi kwa bidii........
 
Amefanya sahihi. Kuhojo hadharani ni sahihi kabisa ila wananchi wajue kinachoendelea.
Kutumbua ndio inapaswa kufuata taratibu za kiutumishi.
Utumbuaji wa hivi haufuati waraka wa utumishi wa umma.

Amandla...
 
Mràdi ulikosewa tangu awali. Mràdi huo ulitakiwa utumie train za umeme za kuzunguka kwà kutumia barabara hizo hizo. Matokeo yake wakaenda kumtoa mchina shida kwà kununua mabasi ya kichina.pia train ya umeme nauli ingekuwa kidogo, pia uharibifu ni kidogo, kuzitawala ni rahisi pia,
Mradi kama huu unaendeshwa kwa mafanikio sana Latin Amerika. Nao wanatumia mabasi sio treni.

Amandla...
 
Hivi kwa nini tiketi za mwendokasi zisiuzwe kama vocha za simu? Unanua vocha, unakwangua halafu unaipitisha kwenye kitu cha kuisoma ndio unaruhusiwa kuingia kituoni. Wauzaji wanazinunua kutoka kwa wakala wa DART. Nadhani mtindo huu utapunguza wizi na mzigo wa ajira kwa DART.

Amandla....
 
Tunarudi kule kule. Haya mambo si ya kuulizana jukwaani. Angemwita yeye na viongozi wake ili wakae waone tatizo liko wapi. Kama ni uongozi lingeonekana tu.

Na kama ni serikali ingeonekana tu maana Meneja angeweza kusema kweli yake bila kuonekana kuwa anamdhalilisha WM hadharani. Inabidi viongozi wakuu wabadilike.

Amandla...
Tunarudi wapi wewe,mabasi yanajaa lakini hawanunui mapya,tiketi wanatoa kienyeji halafu unataka aulizwe sebuleni huku anakunywa fanta?
 
Waziri mkuu sijawahi kuona mpact yake aliyasema yameishia hapo na kama utasikia kuna jipya
 
Mwendokasi tu tumefeli...
SGR tutaiweza.....

Ova
 
Tunarudi kule kule. Haya mambo si ya kuulizana jukwaani. Angemwita yeye na viongozi wake ili wakae waone tatizo liko wapi. Kama ni uongozi lingeonekana tu.

Na kama ni serikali ingeonekana tu maana Meneja angeweza kusema kweli yake bila kuonekana kuwa anamdhalilisha WM hadharani. Inabidi viongozi wakuu wabadilike.

Amandla...
Hakuna kulemba ni kubomoa hapo hapo
 
Nilikuwa siamini kwamba kwenye kila analogusa Magufuli huwa ana haribu Ila kwenye Mwendokasi ndo sehemu niliyokuja kuamini kwa Mara ya kwanza!

Kwanza inabidi wote tujiulize mwendokasi ilianzia wapi?

Mradi wa mabasi ya mwendokasi ukianzishwa na kuasisiwa na Rais wa Awamu ya nne. Kwa Jinsi mradi ulivyokuwa umeandaliwa ulitakiwa kusimamiwa na kampuni binafsi na tangu mwanzo ulisimamiwa kwenye mfumo huo. Mradi huu ulikuwa chini ya Kampuni na Kisena na wakati unaanza kila kitu kilikuwa kinaendeshwa katika dunia ya kisasa. Ticket zilikatwa kielectronic na watu waliweka hadi kuwa na kadi ya kutumia mwezi mzima.

Alipokuja Magufuli kwanza alianza ku deal na kisena kwa sababu kisena hakuwa kwenye kundi la watu waliomuunga mkono kwenye uchaguzi wa mwaka 2015. Alimtesa kisena kumpa kesi za uhujumu uchumi na mkewe na baadae kumnyang’anya mradi na hatimaye akaondoa utaratibu wote mzuri uliokuwa umewekwa kwa ajiri ya kuendesha mradi.

Matokeo yake akawapa wanajeshi, na hapo ndo Tatizo lilipoanza. Mradi ulianza kuendeshwa kwa tabia za kiswahili na watu wakaanza kukata ticket kama daladala.

Mradi huu hadi kufikia sasa ulitakiwa uwe umeshaanza kujiendesha kwa faida Ila kwa roho mbaya ya magufuli na tabia zake za kuchukia matajiri ndo amefanya mradi ule uwe kituko na usifike popote.

Polee kisena. Buriani Mwendokasi.
 
Back
Top Bottom