PreGE2025 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa: Mapato ya ATCL yameongezeka kutoka Tsh Bilion 254 hadi TSh. Trilioni 1.5

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kwani mamlaka inayotakiwa kufanya kazi ya ukaguzi wa mahesabu imehamishiwa ofisi ya waziri mkuu?

Yaani waziri mkuu anasimama kutoa habari za ofisi inayotakiwa kuwa huru?

Sasa kama hii ofisi imeandikwa kisheria ni huru sasa hiki ni nini?

"The Tanzanian constitution ensures the CAG's independence, stating that they are not subject to any orders or directions from any government department or person regarding their audit work. "
 
Kuamin takwimu zinazotolewa na nchi hii ni ujinga ambao sitakuja kuufanya.

Imagine hata takwimu za sensa tu tulidanganywa, sasa hizo financial reports sindo watakuwa wanafuta decimal points afu wanaongeza zero..!
 
Hata mimi kipato changu kwa mwaka bila makato nikitaja hapa mtakimbia.....

Sasa baada ya makato na matumizi yaani nabakia na negative.

Waziri usitudanganye sema wazi Net profit yao hawa jamaa inasoma ngapi?
 
Shirika la Ndege Tanzania ATCL limeongeza mapato yake kutoka Shilingi Bilioni 254 mwaka 2021 hadi kufikia Shilingi Trilioni 1.5 Februari mwaka 2025, ikichangiwa na Ongezeko la Ndege na safari za ndege kwenda nje ya nchi, kulikofanywa na Serikali ya awamu ya sita ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akitoa Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Bunge kwa mwaka 2025/2026, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameliambia Bunge la Tanzania leo Aprili 09, 2025 kuwa katika kipindi cha Februari mwaka 2025 jumla ya abiria 3, 818, 567 walisafirishwa kutoka abiria 822, 232 waliokuwepo mwaka 2021.

"Mheshimiwa Spika, ongezeko la ndege limechangia pia kuongezeka kwa idadi ya abiria wanaohudumiwa kutoka abiria 822,232 mwaka 2021 hadi abiria 3,818,567 Februari, 2025; mizigo kutoka tani 2,567 mwaka 2021 hadi tani 5,730.48 Februari, 2025. Kadhalika, mapato yameongezeka kutoka shilingi bilioni 254 mwaka 2021 hadi shilingi trilioni 1.5 Februari, 2025." Amekaririwa Mhe. Majaliwa.

Waziri Mkuu Majaliwa pia ameeleza kuwa ATCL imeongeza safari zake kwenda nje ya nchi ambapo ndege zake zinasafiri kwenda Johanesburg Afrika kusini, Guangzhou China, Mumbai India, Lubumbasi DRC, Lusaka na Ndola Zambia, Harare Zimbabwe na Dubai, Falme za Kiarabu.

Kulingana na Mhe. Majaliwa, Jumla ya Trilioni 1.49 zimetumika kununua ndege saba, sita zikiwa za abiria na moja ya mizigo suala ambalo limewezesha Ndege za ATCL pia kufanya safari zake kwenda Nairobi Kenya, Entebbe Uganda, Bujumbura Burundi, Moroni Comoro, na Hivi karibuni shirika hilo linatarajiwa kufanya safari za moja kwa moja kutoka Dar Es salaam hadi Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kwa maana hiyo CAG alitudanganya kuwa ATCL ilipata hasara ya billion 91.8 yaani elfu tisini na moja mia nane million (91,800,000,000) kwa 2023/24? Tangu siku ile 12/03/2021 Majaliwa alivyotudanganya kuwa rais yupo ofisini anachapa kazi wakati mambo yalikuwa yashaharibika simuamini tena.
 
Shirika la Ndege Tanzania ATCL limeongeza mapato yake kutoka Shilingi Bilioni 254 mwaka 2021 hadi kufikia Shilingi Trilioni 1.5 Februari mwaka 2025, ikichangiwa na Ongezeko la Ndege na safari za ndege kwenda nje ya nchi, kulikofanywa na Serikali ya awamu ya sita ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akitoa Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Bunge kwa mwaka 2025/2026, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameliambia Bunge la Tanzania leo Aprili 09, 2025 kuwa katika kipindi cha Februari mwaka 2025 jumla ya abiria 3, 818, 567 walisafirishwa kutoka abiria 822, 232 waliokuwepo mwaka 2021.

"Mheshimiwa Spika, ongezeko la ndege limechangia pia kuongezeka kwa idadi ya abiria wanaohudumiwa kutoka abiria 822,232 mwaka 2021 hadi abiria 3,818,567 Februari, 2025; mizigo kutoka tani 2,567 mwaka 2021 hadi tani 5,730.48 Februari, 2025. Kadhalika, mapato yameongezeka kutoka shilingi bilioni 254 mwaka 2021 hadi shilingi trilioni 1.5 Februari, 2025." Amekaririwa Mhe. Majaliwa.

Waziri Mkuu Majaliwa pia ameeleza kuwa ATCL imeongeza safari zake kwenda nje ya nchi ambapo ndege zake zinasafiri kwenda Johanesburg Afrika kusini, Guangzhou China, Mumbai India, Lubumbasi DRC, Lusaka na Ndola Zambia, Harare Zimbabwe na Dubai, Falme za Kiarabu.

Kulingana na Mhe. Majaliwa, Jumla ya Trilioni 1.49 zimetumika kununua ndege saba, sita zikiwa za abiria na moja ya mizigo suala ambalo limewezesha Ndege za ATCL pia kufanya safari zake kwenda Nairobi Kenya, Entebbe Uganda, Bujumbura Burundi, Moroni Comoro, na Hivi karibuni shirika hilo linatarajiwa kufanya safari za moja kwa moja kutoka Dar Es salaam hadi Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Pato ghafi hilo. Nikiingiza TZS 1 million kwa gharama ya TZS 2 million, biashara yangu sio sustainable! Wao wameingiza TZS 1.5 trillion kwa gharama kiasi gani?
 
Back
Top Bottom