PreGE2025 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa: Mapato ya ATCL yameongezeka kutoka Tsh Bilion 254 hadi TSh. Trilioni 1.5

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kwani mamlaka inayotakiwa kufanya kazi ya ukaguzi wa mahesabu imehamishiwa ofisi ya waziri mkuu?

Yaani waziri mkuu anasimama kutoa habari za ofisi inayotakiwa kuwa huru?

Sasa kama hii ofisi imeandikwa kisheria ni huru sasa hiki ni nini?


"The Tanzanian constitution ensures the CAG's independence, stating that they are not subject to any orders or directions from any government department or person regarding their audit work. "
 
Kuamin takwimu zinazotolewa na nchi hii ni ujinga ambao sitakuja kuufanya.

Imagine hata takwimu za sensa tu tulidanganywa, sasa hizo financial reports sindo watakuwa wanafuta decimal points afu wanaongeza zero..!
 
Hata mimi kipato changu kwa mwaka bila makato nikitaja hapa mtakimbia.....

Sasa baada ya makato na matumizi yaani nabakia na negative.

Waziri usitudanganye sema wazi Net profit yao hawa jamaa inasoma ngapi?
 
Kwa maana hiyo CAG alitudanganya kuwa ATCL ilipata hasara ya billion 91.8 yaani elfu tisini na moja mia nane million (91,800,000,000) kwa 2023/24? Tangu siku ile 12/03/2021 Majaliwa alivyotudanganya kuwa rais yupo ofisini anachapa kazi wakati mambo yalikuwa yashaharibika simuamini tena.
 
Pato ghafi hilo. Nikiingiza TZS 1 million kwa gharama ya TZS 2 million, biashara yangu sio sustainable! Wao wameingiza TZS 1.5 trillion kwa gharama kiasi gani?
 
Hapo utakuta matumizi ni 1.8t.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…