Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali itaendelea kuweka mkazo katika kulinda na kudumisha amani nchini ili kuhamasisha maendeleo na kuziba mianya ya kuibuka kwa migogoro miongoni mwa wanajamii.
Ametoa kauli hiyo leo (Jumapili Juni 29, 2025) wakati alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kufunga kongamano la Afrika Mashariki la Amani lililoandaliwa na The Islamic Foundation, katika viwanja vya shule ya msingi Mirongo jijini Mwanza
“Nataka niwaambie bila amani hatuwezi kupata mafanikio yoyote, kupitia kongamano hili mmepata nafasi ya kujadili kuhusu tunu hii ya amani, ambayo wakati wote tumeshuhudia viongozi wa dini mkiwa kwenye majukwaa yenu mkihimiza amani miongoni mwa wanajamii, tuishike tunu hii”.
Kadhalika, amewataka Watanzania kuangalia kwa upana wake suala la mmomonyoko wa maadili katika jamii hasa kwa vijana. “Ni muhimu sana suala hili mkaliweka kama agenda katika mikutano na vikao vyenu, kila kiongozi wa dini anapozungumza, suala la maadili na mmomonyoko wa liwe ni ajenga ya kudumu”
Pia Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa falsafa ya 4R ya Resilience (Ustahimilivu), Reconciliation (Maridhiano) and Reforms (Mageuzi), Rebulding (Kujenga upya) iliyoasisiwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejikita katika misingi imara ya kulinda amani. “Falsafa hii imeifanya Tanzania kuwa tulivu na salama”