Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa: Nataka niwaambie bila amani hatuwezi kupata mafanikio yoyote

Amani mnaitaka nyinyi mkiwa mnakula vizuri,
Bila kuvurugana hakuna maendeleo,
Bora amani isiwepo maisha yakabadilika,
Alafu amani inayosemwa kila siku ni ipi ama mimi sijui maana ya amani?
Sidhani hata kwenye top30 ya nchi zenye amani duniani tumo
 
PM siku hizi huaminiki
Angekuwa ni mtu mwema huu ndio ulikuwa muda mzuri wa kustep down na kuwaachia watu waovu wabakie pekee yao serikalini. Ila sasa mdio hivyo wanakwambia ubinadamu ni kazi sana kwa mtu mnafiki, hawezi kuachia ulaji ili kutenda haki.
 
Amani mnaitaka nyinyi mkiwa mnakula vizuri,
Bila kuvurugana hakuna maendeleo,
Bora amani isiwepo maisha yakabadilika,
Alafu amani inayosemwa kila siku ni ipi ama mimi sijui maana ya amani?
Sidhani hata kwenye top30 ya nchi zenye amani duniani tumo
Wakatazame zile video za waumini wa kanisa la Gwajima halafu watuelezee ni AMANI gani hiyo wanayoielezea kwenye majukwaa ya kuongea as if ni kitu wanachokiheshimu.
 
Hakuna amani hii nchi,porojo tu
Mwaka huu nikipata nafasi ya kuuliza swali kwa diwani ama mbunge watanitafuta waniue,
Nina hakika hatoweza kunijibu na vita itaanzia hapo
 
Na safari hii huo ndio utakuwa mwendo aisee.
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali itaendelea kuweka mkazo katika kulinda na kudumisha amani nchini ili kuhamasisha maendeleo na kuziba mianya ya kuibuka kwa migogoro miongoni mwa wanajamii.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumapili Juni 29, 2025) wakati alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kufunga kongamano la Afrika Mashariki la Amani lililoandaliwa na The Islamic Foundation, katika viwanja vya shule ya msingi Mirongo jijini Mwanza

“Nataka niwaambie bila amani hatuwezi kupata mafanikio yoyote, kupitia kongamano hili mmepata nafasi ya kujadili kuhusu tunu hii ya amani, ambayo wakati wote tumeshuhudia viongozi wa dini mkiwa kwenye majukwaa yenu mkihimiza amani miongoni mwa wanajamii, tuishike tunu hii”.

Kadhalika, amewataka Watanzania kuangalia kwa upana wake suala la mmomonyoko wa maadili katika jamii hasa kwa vijana. “Ni muhimu sana suala hili mkaliweka kama agenda katika mikutano na vikao vyenu, kila kiongozi wa dini anapozungumza, suala la maadili na mmomonyoko wa liwe ni ajenga ya kudumu”

Pia Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa falsafa ya 4R ya Resilience (Ustahimilivu), Reconciliation (Maridhiano) and Reforms (Mageuzi), Rebulding (Kujenga upya) iliyoasisiwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejikita katika misingi imara ya kulinda amani. “Falsafa hii imeifanya Tanzania kuwa tulivu na salama”

amevaa balagashia vizuri inaonekana alienda na kuswali, ila waumini wa gwajima hawataki wapate haki yao ya kuabudu. Mungu atawasaidia lakini.
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali itaendelea kuweka mkazo katika kulinda na kudumisha amani nchini ili kuhamasisha maendeleo na kuziba mianya ya kuibuka kwa migogoro miongoni mwa wanajamii.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumapili Juni 29, 2025) wakati alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kufunga kongamano la Afrika Mashariki la Amani lililoandaliwa na The Islamic Foundation, katika viwanja vya shule ya msingi Mirongo jijini Mwanza

“Nataka niwaambie bila amani hatuwezi kupata mafanikio yoyote, kupitia kongamano hili mmepata nafasi ya kujadili kuhusu tunu hii ya amani, ambayo wakati wote tumeshuhudia viongozi wa dini mkiwa kwenye majukwaa yenu mkihimiza amani miongoni mwa wanajamii, tuishike tunu hii”.

Kadhalika, amewataka Watanzania kuangalia kwa upana wake suala la mmomonyoko wa maadili katika jamii hasa kwa vijana. “Ni muhimu sana suala hili mkaliweka kama agenda katika mikutano na vikao vyenu, kila kiongozi wa dini anapozungumza, suala la maadili na mmomonyoko wa liwe ni ajenga ya kudumu”

Pia Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa falsafa ya 4R ya Resilience (Ustahimilivu), Reconciliation (Maridhiano) and Reforms (Mageuzi), Rebulding (Kujenga upya) iliyoasisiwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejikita katika misingi imara ya kulinda amani. “Falsafa hii imeifanya Tanzania kuwa tulivu na salama”

Ulinzi endelevu wa amani ya nchi unaletwa na kutamalaki kwa haki (sio mabomu na risasi). Amani ni tunda la haki.
 
Yaani kuwe na amani kwenu nyie mnaotuongoza wakati haki zetu sisi ambao hatuko kwenye korido za maamuzi zikivunjwa tunapoonyesha uovu wenu? 😳 🤔:AYOOO:
 
Back
Top Bottom