Waziri Mkuu Kassim Majaliwa: Rais Magufuli ni mzima na anachapa kazi. Wanataka atoke, atoke aende wapi? Kariakoo au Magomeni?

Hili linchi limeoza! Yaani mko serious mnaamini huu uzushi! Ujue msikute mkuu anawasoma anawashangaa tu! I believe, he is very cool and safe! Acheni kuamini kila uzushi! Kuna wanasiasa akiwemo Tundu Lissu wataumbuka! Save this comment!!!

..What?

..R u kidding me?

..Unasema Jiwe yuko mahali anasoma haya?!!

..R u sure?

..Sasa kama anaona haya yanaendelea na hachukui hatua then ana tofauti gani na wanaoneza uzushi huo?
 
Kwanini uamini hapa ndio penyewe? Unatishwa na maneno? Majaliwa ambaye ndio waziri mkuu kasema Rais yupo sawa! Sio tu mgonjwa yupo sawa! Unataka kipi cha ziada?
Mambo ya kuamimiana bila ushahidi hayana tena nafasi kwangu

Nachojua ni kuwa Raisi ni binadamu, katika kuishi kwake lolote linaweza mpata na tetesi kuwa hatupo naye hazipoi zinaongezeka pamoja na kauli ya PM,

kujiandaa kisaikolojia ni muhimu, sina cha kupoteza kama atatokea na kuzungumza maana namuombea mema.
 
Kwahiyo kila ngoma itayopigwa acheze? Kikatiba nini kimevunjwa? Au shida ni political tunes?
 
Kiranga kama Chahali kaandika hivyo tafadhali save ili wakati ukifika usipotezee uwaulize pia! Walizusha 2019 hatukuhoji alipoibuka mh Rais, this time fairly TUTAWAULIZA! No spinning!
Hao kina Chahali sijui Kigogo sikui Tundu Lissu ni wananchi tu.

Chahali hata akikosea si big deal. Atakosa credibility kwa wafuasi wake lakini hana national impact.

Aliye na national impact ni Magufuli. Kwa sababu yeye ni Head of State.

Kama Magufuki yupo mzima, kwa nini inakuwa vigumu sana kujitokeza kusalimia wananchi na kusema yeye ni mzima tu?
 
Sitaki kuamini.

Nataka kujua.

Nataka kumuona Magufuli akisema yupo hai na ni mzima.
Sawa ila nitataka pia kukuona ukizodoa hao wazushi kwa nguvu hii hii siku akijitokeza! Tatizo akijitokeza thread zake hazitozidi hata page 30 na wazee wa mbanga mtapotea [emoji41]
 
Wewe hizo tetesi unazipata wapi zaidi ya same sources? Sources famba!!!
 
Kiukweli, kama Watanzania wenzetu wanaweza kufanya haya alafu wasichukuliwe hatua basi linchi limeoza! Huku ni kuvuka mstari! Aibu! Aibu! Aibu! Kushabikia haya!
Mimi naona rais kujificha wakati watu wanaeneza uongo, kama hizi habari ni uongo, ndiyo uozo wenyewe.

Kama Magufuli ni mzima, kwa nini asijitokeze na kumaliza uvumi kwamba kafa?
 
Sasa mzee kama hao wanachochea hizi tetesi si watu muhimu kwanini ajitokeze kwa influence zao? Kwahiyo kesho Pierelikwidi akisema Rais kafa itabidi JPM amjibu pia?

Alafu narudia wewe unaheshima zako humu, Tundu Lissu ni mtu wa kawaida? Ndiye aliyekuwa mpinzani mkuu wa JPM uchaguzi uliopita hivyo maneno yake yana uzito. Wakikosea jipange kuwazodoa pia! No double standards.
 
Mimi nashangaa watu mpaka leo wanakwenda kwa kuamini wanasiasa, katika jambo ambalo kulimaliza hatuhitaji experiment itakayogharimu fedha za kigeni!

Kama Magufuli yupo hai na ni mzima, kwa nini asijitokeze kumaliza mjadala watu waendelee na shughuli zao nyingine badala ya kubishana kuhusu hili?
 
Wewe hizo tetesi unazipata wapi zaidi ya same sources? Sources famba!!!
Sawa kama ni famba itapendeza sana. Hivi ni kweli raisi wa Zanzibar kasitisha shughuli zake? Au nayo ni famba?
 
Mimi naona rais kujificha wakati watu wanaeneza uongo, kama hizi habari ni uongo, ndiyo uozo wenyewe.

Kama Magufuli ni mzima, kwa nini asijitokeze na kumaliza uvumi kwamba kafa?
Mfano kesho akijitokeza alafu baada ya wiki Pierelikwidi akazusha tena ajitokeze tu?? Let's be fair!

Nimesoma vyombo vyote vya kimataifa vilivyoripoti hii habari wame quote taarifa ya Lissu au opposition in general!
 
Jua kusoma kwa ufahamu. Hakuna nilipoandika kwamba kuna mtu asiye muhimu.

Kila mtu ni mtu muhimu. Nimesema hao kina Tundu Lissu na Chahali ni wananchi wa kawaida kwa maana si Heads of State. Ni muhimu kwenye upinzani, kwa wafuasi wao etc. Magufuli ni Head of State, ni muhimu kwa nchi nzima.

Rais ana wajibika kuwa transparent.

Rais ni muajiriwa wa wananchi. Moja ya kazi yake ni kuonekana anaongoza nchi. Nchi iko katika pandemic, watu wanakufa left right and center. Rais hajulikani alipo, wiki mbili nzima.

Wewe unaona hapo hamna tatizo?

Kwako wewe rais kukaa bila kuonekana hadharani in the middle of a pandemic kwa muda gani kunakubalika?

Wiki mbili? Mwezi mmoja? Miezi sita? Mwaka mmoja? Miaka miwili? Miaka mitano?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…