Very clear bila hata chenga, mmepata picha kamili kuna upendo mkubwa sana dhidi ya Rais na serikali yetu.Ukweli utabaki kuwa rais na serikali inapendwa sana, inapendwa na wanafunzi wanaosoma bure bila ada,wapo wanaoshukuru hospitali mpya zilizojengwa na huduma Bora za afya.
Wapo ambao hawakuweza kufanya shughuli zao za usafirishaji ila sasa miundombinu iliyoboreshwa wanafanya vyema shughuli zao za usafirishaji. Wapo ambao walidhulumiwa haki zao na mafisadi na vigogo na walionyimwa haki zao mbalimbali Mh rais ameacha alama mioyoni mwao.
Ukweli ni kuwa serikali inapendwa sana. Msidhani ni upendo wa walio nje ya nchi tu. Bali wengi walio ndani hapa Tanzania wanawapenda sana.
Mbaya zaidi wale wanyonge na wanaotambua yale mazuri waliyofanyiwa na serikali hawana muda na mitandao ya kijamii Bali wale waliotumbuliwa,waliotaka kufanya ufisadi,madawa ya kulevya,utakatishaji,uchu wa madaraka n.k ndio wamegeuka kuisema serikali ya Mh rais.
Viva Magufuli, viva Tanzania.