Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,413
- 23,592
Halafu mbaya zaidi aliongopa akiwa ndani ya nyumba ya ibada!!
Kuna dini moja tu ambayo athari zake si kwa waumini wake tu bali kwa taifa zima la Tanzania na watu wake wote. Dini hiyo si Ukristo wala Uislaam, ni UCCM!
Ukishakuwa muumini wa hii dini hisia, fahamu na mantiki hupotea...ingawa unayo macho utatazama lakini hutaona, ingawa una masikio utasikiliza lakini hutaelewa!
Tunajenga taifa la ajabu ambapo hakuna tofauti kati ya wema na ubaya, hekima na uovu, ukweli na uongo ...vyote vimekumbatiwa kitaifa kwa vifijo, vigelegele na makofi!