Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa: Tunaboresha maslahi ya Wafanyakazi, sio lazima tuseme hadharani

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa: Tunaboresha maslahi ya Wafanyakazi, sio lazima tuseme hadharani

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imejifunza kuwa inapotangaza hadharani kuhusu kupandishwa mishahara, kumekuwa kunatengeneza gharama kubwa na kusababisha ugumu wa maisha ya wengine.

Ameeleza hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Konde (ACT-Wazalendo) Khatib Haji aliyehoji ni lini Wafanyakazi wa Tanzania watapandishiwa mishahara na kuboreshewa maslahi.

Waziri Mkuu amesema, "Eneo la Wafanyakazi peke yake ukitangaza hadharani kwamba tumepandisha mishahara kwenye masoko, vituo vya mabasi na huduma nyingine zote zinapanda".

Amekiri ni kweli wafanyakazi wengi wanasubiri kusikia kupanda kwa mishahara akisema hilo likifanyika linatengeneza ugumu wa maisha, hivyo bado Serikali inaendelea kutafuta njia nzuri ya kuongeza maslahi ya mtumishi.

Aidha, Waziri Mkuu ameeleza kuwa maslahi ya wafanyakazi hayapo kwenye mishahara tu bali pia kwa kuwapandisha daraja na kupunguza kiwango cha kodi.
 
Wasiongeze hiyo mishahara yao! Watupandishe tu madaraja yetu. Huu upuuzi wa kutudhulumu kwa zaidi ya miaka 5, unaleta maudhi yaliyo pitiliza.
 
Hamna mwenye shida ya kutangaziwa ongezeko la mshahara. Ongezeni hata kimya kimya, si wataona wenyewe
 
Acha longo longo amesema Hivi.
 

Attachments

  • IMG_20210211_095814.jpg
    IMG_20210211_095814.jpg
    124.7 KB · Views: 4
Hizo hela ambazo hazijaongezwa kwenye mishahara na madaraja ya watumishi wa serikali,kwanini wasizitumie hata kuajiri wafanyakazi wengine?
Au ajibu tu kua pesa zote zinatupiwa kule Nyerere dam,SGR na kwingineko,tujue.
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imejifunza kuwa inapotangaza hadharani kuhusu kupandishwa mishahara, kumekuwa kunatengeneza gharama kubwa na kusababisha ugumu wa maisha ya wengine...
Swali ni je huku kupanda kwa mafuta,cement,ngano n.k walitangaza nn mpk vikawa hivyo?awamu ya roho mbaya hii
 
Napenda na wao wajue hali huku kitaa kwa Walimu sio khali
Makato ya 35% kwenye gross salary ya mtumishi hasa mwalimu na ile bodi ya mkopo khali ni tete
 
Waziri Mkuu amesema, "Eneo la Wafanyakazi peke yake ukitangaza hadharani kwamba tumepandisha mishahara kwenye masoko, vituo vya mabasi na huduma nyingine zote zinapanda"...
Mwanangu cheza hapahapa nyumbani jioni nitakuletea pipi na biskutiiii... umesikia!!!!
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imejifunza kuwa inapotangaza hadharani kuhusu kupandishwa mishahara, kumekuwa kunatengeneza gharama kubwa na kusababisha ugumu wa maisha ya wengine....
Huyu mzee mwanzo nilikuwa namuona ni bonge la kiongozi kumbe naye ni hovyo kabisa
 
Back
Top Bottom