Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa: Tunaboresha maslahi ya Wafanyakazi, sio lazima tuseme hadharani

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa: Tunaboresha maslahi ya Wafanyakazi, sio lazima tuseme hadharani

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imejifunza kuwa inapotangaza hadharani kuhusu kupandishwa mishahara, kumekuwa kunatengeneza gharama kubwa na kusababisha ugumu wa maisha ya wengine....
Hapajawahi kuwa na PM wa hovyo kama huyu. Ndiyo maana shangazi zake aliwatoa sadaka.
 
Aisee kama ni mchezo wa karata basi watumishi walilamba dume, lazima tumuongezee mitano mingine atake asitake🤣
 
Nnaona kapiga porojo wala hajajibu swali aliloulizwa, kimsingi kuna wanasiasa wanatuonaga kama mazwazwa na hatuna akili, nnashauri tuendako tusije kuthubutu kuwapa walimu nafasi ya kuongoza nchi hii tena maana roho zao mbaya
 
Kwa muda mrefu tangu mwaka 2016, nimekuwa nafuatilia nafuatilia kauli za PM kuhusu hiyo mishahara ya wafanyakazi, mara utamsikia akisema hivi sasa serikali imetengeneza mfumo wa kielekroniki wa lawson, ni mfumo unaobainisha wenyewe watumishi wanaostahili kupandishwa madaraja, hivyo tatizo hilo limepatiwa ufumbuzi wa kudumu! Haya ilipofika 2018, akaja na kauli mpya OOH! Serikali imeunda Tume ya kupitia upya viwango vya mishahara na kwa tunasubiri ikamilishe kazi na kutoa mapendekezo! Tume hiyo mpaka leo kimyaa! Na sasa leo bado anasema serikali ikipandisha mishahara gharama nyingine zitaongezeka! Hapa serikali iache uvivu!

Hivi si hiyohiyo serikali ndio inayotoa bei elekezi ya huduma?

Kwani wakiwapandishia wafanyakazi mishahara alafu wakatoa bei elekezia za nauli za mabasi na huduma nyingine ni nani atapinga???
Ikumbukwe kwamba ongezeko la mishahara kwa wafanyakazi lina mchango sana katika kuchangamsha mzunguko wa fedha na ukuwaji wa uchumi kwa ujumla!

Ukipandisha mishahara na madaraja kwa watumishi utawezesha watumishi hawa kukopa mamilioni kwenye mabenk, Ni haohao watumishi watalipa fedha hizo kufanya manununuzi, kulipia huduma na mambo mbali mbali, humo mote serikali itakusanya kodi na kutunisha mfuko, uchumi unapaa, Lakini kuendelea kuzuia mishahara isipande kunadumaza mzunguko wa fedha na ucumi kwa ujumla.
Nashauri serikali ishirikishe wataalam wake wa masuala uchumi kupata ushauri muafaka kwenye jambo hili, lakini tukiendelea kulibeba kisiasa tutaendelea kuimiza nchi yetu kiuchumi.
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imejifunza kuwa inapotangaza hadharani kuhusu kupandishwa mishahara, kumekuwa kunatengeneza gharama kubwa na kusababisha ugumu wa maisha ya wengine...
Jibu zuri la mh.swali la nyongeza: je katika kuwasilisha budget ya sirikali ongezeko la kiasi Cha Mishahara, litafichwa kutajwa?Au litapewa kasima bandia? Mishahara ya watumishi ni component kubwa haiwezi kufichika kirahisi ni vema kuwa na serikali transparent kujenga Imani kwa watu wake
 
Kwa ujumla walimu wana roho ngumu, omba usiongozwe nao. wamezoea maisha ya kujibana.
Kabisa watu wengi waliounga maisha wana roho mbaya, nakumbuka lecture wangu chuo alijiendeleza toka ualimu wa upe alifanya somo lake lionekane gumu makusudi watu wateseke.
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imejifunza kuwa inapotangaza hadharani kuhusu kupandishwa mishahara, kumekuwa kunatengeneza gharama kubwa na kusababisha ugumu wa maisha ya wengine...
Huyu naye tulimtetea sana kumbe tungeacha tu Anko Magu akawadunde shangazi zake.
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imejifunza kuwa inapotangaza hadharani kuhusu kupandishwa mishahara, kumekuwa kunatengeneza gharama kubwa na kusababisha ugumu wa maisha ya wengine.

Ameeleza hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Konde (ACT-Wazalendo) Khatib Haji aliyehoji ni lini Wafanyakazi wa Tanzania watapandishiwa mishahara na kuboreshewa maslahi.

Waziri Mkuu amesema, "Eneo la Wafanyakazi peke yake ukitangaza hadharani kwamba tumepandisha mishahara kwenye masoko, vituo vya mabasi na huduma nyingine zote zinapanda".

Amekiri ni kweli wafanyakazi wengi wanasubiri kusikia kupanda kwa mishahara akisema hilo likifanyika linatengeneza ugumu wa maisha, hivyo bado Serikali inaendelea kutafuta njia nzuri ya kuongeza maslahi ya mtumishi.

Aidha, Waziri Mkuu ameeleza kuwa maslahi ya wafanyakazi hayapo kwenye mishahara tu bali pia kwa kuwapandisha daraja na kupunguza kiwango cha kodi.
Kauli ya Majaliwa siyo ya kuichukulia serious hata siku moja. Huyu ni Waziri Mkuu kwa jina. Kama unategemea mshahara utapanda kwa kauli ya Majaliwa unaapoteza muda.
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imejifunza kuwa inapotangaza hadharani kuhusu kupandishwa mishahara, kumekuwa kunatengeneza gharama kubwa na kusababisha ugumu wa maisha ya wengine.

Ameeleza hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Konde (ACT-Wazalendo) Khatib Haji aliyehoji ni lini Wafanyakazi wa Tanzania watapandishiwa mishahara na kuboreshewa maslahi.

Waziri Mkuu amesema, "Eneo la Wafanyakazi peke yake ukitangaza hadharani kwamba tumepandisha mishahara kwenye masoko, vituo vya mabasi na huduma nyingine zote zinapanda".

Amekiri ni kweli wafanyakazi wengi wanasubiri kusikia kupanda kwa mishahara akisema hilo likifanyika linatengeneza ugumu wa maisha, hivyo bado Serikali inaendelea kutafuta njia nzuri ya kuongeza maslahi ya mtumishi.

Aidha, Waziri Mkuu ameeleza kuwa maslahi ya wafanyakazi hayapo kwenye mishahara tu bali pia kwa kuwapandisha daraja na kupunguza kiwango cha kodi.
Viongozi wa Serikali wote toka juu mpaka chini ni matatizo matatupu wanakuwa wametolowa toka mapango ya Stone Age hawajui taratibu za msingi za kuendesha Serikali ya Kisasa, wao wanaendesha jinsi wanavyoamka au wanavyofikiri ilitakiwa iwe. Taratibu za utendaji kazi na watendaji wenyewe ziko wazi kabisa lakini zisipofuatwa matokeo yake yanafika mbali haraka sana na madhara yanakuwa makubwa. Awamu ya Tano ilipoingia madarakani iliingia na matatizo mengi ikiwa ni pamoja na maslahi ya wafanyakazi kama kupandishwa vyeo, nyongeza za mwaka, marupurupu ya uhamisho na likizo nk yaliwekwa pembeni kimyakimya bila hata kutoa sababu. Miaka 5 yote Wafanyakazi walidai haki zao na kulalamika sana mpaka malalamiko yakafika nchi nzima mpaka kwa machinga na mamantilie nao wakisaidia kusinikiza Serikali itekeleze wajibu wake lakini haikusadia. Awamu zilizopita walitumia Sikukuu yao ya Mei Mosi kutangaza malipo yoyote ya muda mrefu ya wafanyakazi wote bila madhara yoyote. Waziri Mkuu ni walewale!
 
Back
Top Bottom