Kwa muda mrefu tangu mwaka 2016, nimekuwa nafuatilia nafuatilia kauli za PM kuhusu hiyo mishahara ya wafanyakazi, mara utamsikia akisema hivi sasa serikali imetengeneza mfumo wa kielekroniki wa lawson, ni mfumo unaobainisha wenyewe watumishi wanaostahili kupandishwa madaraja, hivyo tatizo hilo limepatiwa ufumbuzi wa kudumu! Haya ilipofika 2018, akaja na kauli mpya OOH! Serikali imeunda Tume ya kupitia upya viwango vya mishahara na kwa tunasubiri ikamilishe kazi na kutoa mapendekezo! Tume hiyo mpaka leo kimyaa! Na sasa leo bado anasema serikali ikipandisha mishahara gharama nyingine zitaongezeka! Hapa serikali iache uvivu!
Hivi si hiyohiyo serikali ndio inayotoa bei elekezi ya huduma?
Kwani wakiwapandishia wafanyakazi mishahara alafu wakatoa bei elekezia za nauli za mabasi na huduma nyingine ni nani atapinga???
Ikumbukwe kwamba ongezeko la mishahara kwa wafanyakazi lina mchango sana katika kuchangamsha mzunguko wa fedha na ukuwaji wa uchumi kwa ujumla!
Ukipandisha mishahara na madaraja kwa watumishi utawezesha watumishi hawa kukopa mamilioni kwenye mabenk, Ni haohao watumishi watalipa fedha hizo kufanya manununuzi, kulipia huduma na mambo mbali mbali, humo mote serikali itakusanya kodi na kutunisha mfuko, uchumi unapaa, Lakini kuendelea kuzuia mishahara isipande kunadumaza mzunguko wa fedha na ucumi kwa ujumla.
Nashauri serikali ishirikishe wataalam wake wa masuala uchumi kupata ushauri muafaka kwenye jambo hili, lakini tukiendelea kulibeba kisiasa tutaendelea kuimiza nchi yetu kiuchumi.