Waziri Mkuu Kassim Majaliwa yuko wapi? Kimya sana, kulikoni?

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa yuko wapi? Kimya sana, kulikoni?

PM yuko ofisini anachapa kazi. Unataka kiongozi mkuu wa serikali azurure tu Magomeni au Kariakoo?
Hapana tunataka wawe na 'Machawa' wao...kam Wasanii wanavyowakilishwa na wale kina mikwaju, baba lovo n.k.
 
Salaam Wakuu;

Waziri Mkuu kawa kimya sana miezi ya karibuni, tatizo ni Nini? Hii Hali ni tofauti na mwanzo alikua akitoa ushirikiano na kila wakati tutamsikia kwenye media akieleza mambo kadhaa na kukagua miradi ya serikali, sasa haonekani Tena!

Nini shida?
Nyakati zimebadilika mkuu. Ila kuna ile kauli ya mama alipozungumza na Baraza la Mawaziri tarehe 13 ya mwezi huu wakati anatoa ufafanuzi wa msamiati MUHALI.

Akamtolea mfano PM kwamba "kwa mfano PM hafanyi vizuri halafu simwambii ukweli, huo ndiyo muhali". Mimi nilijiuliza why mfano uwe kwa PM?

Lkn siku za nyuma alipomchamba Spika alisema "huko bungeni kwa kina Kassim...". Mtu wa cheo cha PM unatajwa kwa jina lako tena your first name!

Aidha, kitendo cha Lukuvi kupewa kazi ya uratibu wa Wizara zote pia kilinitafakarisha sana kwasababu kuratibu mawizara ni kazi ya PM.

Mimi nadhani kwa PM mambo hayako kama zamani. Ni swala la muda tu.
 
Kassim Majaliwa ndie PM ambae amekaa madarakani muda mrefu zaid ukimto Mh.Fredrick Sumaye na Mzee Kayanza Pinda na pia ameingia kwny list ya Cleop Msuya kuwa PM kwa ma Rais tofauti

Lakin kubwa zaid ndie PM ambae hajapata Msukosuko wa kisiasa katika Mawaziri wengi waliotawala…

Ma Rais wa Zamani katika mambo mengi ya Maamuzi magumu walikuwa wanatanguliza Ma PM wao matokeo yake wakawa wanashambuliwa zaid wao kuliko Rais katika hilo mf.Kawawa, Lowassa, Malecela…lakin kuanzia Utawala wa JPM na SSH wao ma Rais ndio wanaingia front na PM anabaki nyuma na matokeo yake ma Rais hawa wanakabiliwa na mashambulizi ya moja kwa moja Mf.issue ya michango ya rambirambi za tetemeko kule Kagera ilipaswa atangaze PM, au suala la kupandisha bei ya Umeme ilipaswa atangaze PM

Pia PM kajiweka mbali sana na mbio za Urais tofauti na PM waliomtamgulia matokeo yake kajikuta hajatengeneza Kambi kama z kina Msuya, Lowassa na Malecela kwny kusaka Urais timu ambazo zikajikuta zinakabiliana na kambi hasimu na matokeo yake kuzaa majungu na makashfa ya kutengenezeana
 
kumbukizi kabla ya uchaguzi wafipa walivyokua wanapanga baraza lao kwenye vijiwe vya kijitali.
Rais Lisu.
waziri mkuu Mbowe.
wanawake jinsia na watoto Halima Mdee.
waziri wa sheria Lema.
waziri wa ulinzi John Heche.
sanaa ajira na michezo Sugu a.k.a Rais wa Mbeya.
waziri wa maliasili Nyarandu.
kitengo cha habari kigogo2014.

baada ya uchaguzi sasa:

Rais Lisu kakimbilia Ubalozini.
Mbowe waziri mkuu yupo jela.

waziri wa jinsia Mdee kang'ang'ania Bungeni.
Sugu waziri wa sanaa kapewa sifa ya uwekezaji Mbeya.
nabii Lema waziri wa sheria kajikita tweeter uko.

waziri wa utalii kakamatwa mpaka wa Kenya anatoroka.
Ally Bananga anasema familia kwanza chama baadae.
Kigogo yupo na chif Hangaya.

hii nchi ngumu sana ndugu zangu.
 
Salaam Wakuu;

Waziri Mkuu kawa kimya sana miezi ya karibuni, tatizo ni Nini? Hii Hali ni tofauti na mwanzo alikua akitoa ushirikiano na kila wakati tutamsikia kwenye media akieleza mambo kadhaa na kukagua miradi ya serikali, sasa haonekani Tena!

Nini shida?
Akikagua miradi kwa sasa itakuwa ni aibu, maana hakuna kinachoendelea
 
Back
Top Bottom