Waziri Mkuu Lebanon asema watatekeleza azimio la umoja wa mataifa kwa kupeleka Jeshi mpaka wao wa Kusini kuchukua nafasi ya Hezbollah!

Marekani ni moja ya nchi zilizopigana vita vingi duniani, huwezi sema eti inaogopa vita, nivile tu hujagusa maslahi yake vilivyo.
 
Sio Israel, vita vya ardhini ni vigumu kwa nchi zote hata hiyo marekani ama urusi, kumbuka unapambana na wapiganaji waliofundishwa kutumia silaha ipasavyo
Russia amethibitisha kuwa anaiweza na ameiweza.

Vita wanayopigana wale ma slavic Ukraine na Russia ni ngumu sana ya mtaa kwa mtaa. Anglo-Saxon hawaiwezi ile vita.

Russia ameonyesha anaiweza na ndiyo maana mchina anaifanyia kazi kwa sasa hivi ikiwa kama ataivamia Taiwan.

Kwa upande wa Israel nguvu yake kubwa ni anga: Anafanya mashambulizi kwa kutumia ndege na drones n.k ila ardhini bado ameonyesha hajaiweza.

Hizbullah ni mzuri ardhini ila kwenye anga ni mdebwedo. Kwa kulitambua hili ndiyo maana Israel wamesema operation itakuwa ni limited kwa maana wana test ground force yao ipoje!

Kama wakifanikiwa watatanua zaidi wigo wa malengo yao.
 
Chanzo kingine cha Middle east Observer kinasema.......

Israel has been firing artillery and and phosphorus bombs on the border around the Metula Settlement for the past 3 or 4 hours, but no ground entry recorded yet.
-------------------
Mpaka kesho asubuhi tutapata taarifa kamili.
 
Huwezi kuipa ushindi Urusi kwakuwa vita bado havijaisha na ugumu pia bado unaonekana, ikiwa watu wanadai Urusi inapigana na wanajeshi wa Ukraine wasio na mafunzo na bado Ukraine inahimili vita tena kwenye mji wa Urusi inathibitisha kuwa vita vya ardhini kwa upande wa Urusi pia ni vigumu, Israel inapata wakati mgumu kwakuwa inapigana na adui ambae kwanza Hana sare za kimapigano, pili adui amejichanganya katikati ya raia, eneo la Gaza ni dogo mno lakini lenye wakaazi zaidi ya million lazima operation ya ardhini pia iwe ngumu.
 
Israeli evacuation orders to a whole neighborhood in Beirut.

This is Sayyed Shuhada compound area. They are evacuating this whole area and the area near Al-Qaem mosque (which several assassinations took place in)

This is a big area
 
Sasa kumbe Nchi Ina jeshi, kwanini wakawacha wahuni wajitwalie tu kama wanavyotaka.
Siasa za mashariki ya kati ni kichekesho sana😂😂. Yaani hivi vikundi vinakuwa na intelijensia na nguvu ya kijeshi kuliko serikali
 
Siasa za mashariki ya kati ni kichekesho sana😂😂. Yaani hivi vikundi vinakuwa na intelijensia na nguvu ya kijeshi kuliko serikali
Ndio maana serikali ya Lebanon haipingi Israel ikiwapiga Hezbollah yaani hao Hezbollah wanaweza kwenda Bank wakachukua hela kwa nguvu au wakachapa mtaa mzima na hakuna Mahali utawashitaki sababu Wana Makombora
 
Brother, kwanza kabla ya yote unaifahamu vita?

Unatuma Infantry soldier wakiwa na vifaru na magari mengineyo ya vita. Unatengeneza perimeter ku repel attacks from any direction. Kwa namna hiyo umbali wa mita kadhaa utaweka vikosi vya mizinga vikusaidie na ukumbuke lengo lako ni kufanya sweeping.

Kumbuka unayepigana naye ana nyenzo kama za kwako! Anafuatilia mwenendo wako kwa satellite za kijeshi au drones za kijasusi ili atume coordination labda kwa kikosi cha mizinga ili asambaratishe kikosi cha adui.

Huku mapambano yakizidi kwa askari wa miguu waombe msaada kwa watu wa mizinga au wenzao wenye vifaru au jeshi la anga. Ukumbuke haupo peke yako mnapigana hiyo ni vita.

Wakati una deal na sweeping ni urban warfare unapita mtaa ambao haujui adui kajifichia wapi! Unaingia nyumba ambayo haujui adui kajifichia chumba gani. Usafishe chumba kwa chumba mpaka nyumba mpaka kijiji mpaka jiji.

Kwa ufupi tu chukua hiyo picha.
Wakati huku mnaomba sapoti kutoka kikosi cha mizinga kumbe adui ana wa zoom, anawapa raha analipua kikosi cha mizinga cha kwenu.

Unapigana na adui wa namna hiyo ambaye ana jeshi kamili la kamandi ya anga, majini, ardhini n.k ana viwanda vya kutengeneza silaha. Ana meli vita, ndege vita, helicopter, mavifaru. Ana jeshi lenye mafunzo na askari wa kutosha na Ukraine ipo kwenye rank ya majeshi bora 20 duniani kabla ya kuvamiwa na Russia.

Russia anapambana na hili jeshi na kateka miji tangu mwaka 2022 mpaka leo hola Ukraine hajarudisha. Kachukua miji kama Donetsk, Kharkiv, Kherson, Luhansk, Mykolayiv, and Zaporizhzhya Oblasts na sasa hivi anachukua Odessa. Amechukua takribani asilimia 20 plus ya nchi.

Unasema Israel inapitia wakati mgumu kwa kupigana na Hizbullah? Wanamgambo ambao wana share kambi na jeshi la nchi na kambi zao zingine zinafahamika?

Wanamgambo ambao hawana ndege vita hawana vifaru, hawana air defensive system. Hawana meli vita, hawana helicopter wao wana jeshi tu la ardhini. Wanamgambo ambao anga lao lipo uchi Israel anapiga anavyojisikia?!

Aina ya vita ambayo anapigana Israel tayari Russia alipigana nayo nchini kwake kwenye jimbo la Chechnia ambalo kwa sasa hivi lipo chini ya Ramdan Kadyrov na akashinda vita.

Brother, ipe heshima Russia.

Vita anayopigana Israel ni nyepesi sana! Akiwa na askari wabishi wenye kuhimili mapigano na wasiyo waoga anateka maeneo ya Lebanon na anaongeza mipaka. Ila askari wake wa ardhini waoga.

Changamoto ambayo ninayoiona kwa Israel kwa jeshi lake la ardhini asije akategeshewa mtego kama Ukraine anavyofanyiwa akasubiriwa aingie ndani zaidi.

Na wao hili wameshalitambua; na ndiyo maana wanasema ni operation ambayo itakuwa na mipaka. Kadri watakavyo faulu ndivyo kadri watakavyo tanua wigo.

Wakiona wanafeli siyo mbaya! Wanawapa makamanda wa anga wanacheka nao unakuwa ni mwendo wa vifusi tu.
 
Umeandika maneno mengi sana huku point zikiwa chache, hivyo vyote Urusi ameiacha mbali sana Ukraine kuanzia idadi ya wanajeshi hadi vifaa vya kijeshi, Ukraine inapigana kwa kupewa visilaha Tena vya kupimiwa tu, pamoja na hayo imepigana na kukomboa miji kama Kherson japo si yote!, snake island pamoja na Lyman huko kote Urusi imefurushwa, imagine Ukraine iwe na idadi ya wanajeshi au silaha ilizonazo Urusi uwanja ungekuwaje?

Kingine umesema wanajeshi wa Israel ni waoga sio? Hamas wanakambi zao sio? wana sare sio? Kaka ushahidi upo mwingi humu wa video za Hamas wakipigana bila sare, sasa kati ya Israel na Hamas nani waoga?
 
Tatizo lako Adiosamigo huwa unajibu kimihemko saana! Kichaka chako cha wanawake na watoto ndiyo unachokimbilia kila siku! Hamas ni magaidi hawapigani kama professional soldiers siku zote gaidi huwa hajitokezi hadharani anavizia vizia tu! Hata uniform rasmi hawana wanajidisguise na wananchi wa kawaida ndiyo maana zayuni anachanganya wote.
 

Waziri Mkuu wa Lebanon akili hana, hopeless, sio kiongozi kabisa, hakuna lolote watafanya, all the time magaidi ya Hezbollaah yanafanya kazi za kigaidi nchini Lebanon against Israel, yeye alikuwa amekaa kimya akichekelea tu, tena anawa support hao magaidi, leo anaona magaidi wanauawa na kupigwa vibaya anajidai kuleta Jeshi mpakani, hao wote ni moja, yaani Hezbollaah na Jeshi la Lebanon ndio hao hao, dawa yao ni kufyeka wote hata huyo Waziri Mkuu wa Lebanon ajichunge sana myahudi ataondoka nae soon..!!
 
Uwezo wa kijeshi wa Ukraine kabla ya kuvamiwa na Russia ulkidunia ulikuwaje?

Na uwezo wake kwa bara la Ulaya ukipimwa kwa nchi moja moja ulikuwa namba ngapi?
Kingine umesema wanajeshi wa Israel ni waoga sio? Hamas wanakambi zao sio? wana sare sio? Kaka ushahidi upo mwingi humu wa video za Hamas wakipigana bila sare, sasa kati ya Israel na Hamas nani waoga?
Maelzo ya juu ili upate picha ya vita jinsi inavyopiganwa. Kwa bahati mbaya hukuelewa.

Ninachokiona hapa nazungumza na mtu ambaye hajui vita zinapiganwa vipi! Hata nikikutolea mifano 1000 hutoweza kuelewa.

Hamas ni kama wale waasi wa Kibiti! Kipindi cha Mabeyo alipeleka vijana kadhaa ndani ya miezi kadhaa wote wakaondolewa. Israel mpaka sasa bado anapambana nao.

Vijana wa Hamas ni kama vijana wale wa mapangoni Tanga waliyoleta fujo. Kipindi cha Mwamunyange wamepelekwa vijana kadhaa ndani ya masaa kadhaa operation ilienda vizuri. Israel mpaka sasa bado anapambana nao.

Kwa ufahamu wako vijana kama hawa ambao hawana chochote zaidi ya SMG na RPG unaipa credit Israel kuwa ni jeshi bora na bado anapambana nao takribani mwaka sasa?

Halafu unaidogesha Russia kwa kupigana na Ukraine ambayo kamandi ya ardhini wana independent tank, mechanized and artillery units, but also Army aviation and Air Defense.

Bravo brother! Bravo!
 
Kwa hiyo Kura unahamisha Kwa Hezbollah sio?
 
Unaona sasa yani unafananisha Hamas na vibaka wa kibiti dar aise hii nchi kweli ina vilaza, alafu kumbe wewe ni mtaalamu wa kivita kiasi Cha kuniona mimi sielewi kitu, kwamba unajua namna vita vinavyopiganwa kuliko waliopo vitani wenyewe, ukiwa front line mambo yanakuwa tofauti na hii essay unayoiandika hapa.
 
Kwa hiyo Kura unahamisha Kwa Hezbollah sio?
Ukiwa kama kiongozi wa kijeshi ni lazima ufahamu nguvu yako na udhaifu wako.

Israel airforce ipo vizuri na Hizbullah hawana hii nguvu.

Hapa Israel kapatumia vizuri na kaleta maafa makubwa kwa Hizbullah na Israel ameshinda kwenye.

Kwa kamandi ya ardhini ni mapungufu kwa Israel na ndiyo maana hajakurupuka kwa sababu anafahamu nguvu ya adui wake kwani kwenye vita hutakiwi kumdharau adui yako.

Kwa msingi huo operation yake huko South Lebanon kaifanya kuwa ni limited hakutaka iwe full.

Ikiwa successful atatanua wigo zaidi. Ikiwa kashindwa atarudi nyuma na kuangalia afanye nini zaidi.

Kura sijaihamisha popote ila nazungumzia uhalisia.
 
Bro! Wewe hufahamu chochote mambo ya kijeshi na mambo ya kivita.

Wewe baki hivyo hivyo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…