Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameliagiza Jeshi la Polisi kuhakikisha linamtafuta popote alipo mmiliki wa jengo la ghorofa lililoporomoka jijini Dar es Salaam na kusababisha vifo vya watu 15 na kujeruhi wengine zaidi ya 80.
Pia, amesema kuwa Serikali imeunda timu ya watu 19 kwa ajili ya kukagua ubora wa majengo yote yaliyopo eneo la Karakoo jijini Dar es Salaam, ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Samia Suluhu Hassan.
Soma Pia:
Majaliwa ameyasema hayo leo Novemba 18, 2024 wakati akiongoza waombolezaji kuaga miili ya watu waliofariki baada ya kudondokewa na jengo hilo kwenye tukio lililofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.