Waziri Mkuu Majaliwa aagiza uhakiki wa vibao vya majina ya mitaa katika anwani za makazi ili kuepuka makosa ya maandishi

Waziri Mkuu Majaliwa aagiza uhakiki wa vibao vya majina ya mitaa katika anwani za makazi ili kuepuka makosa ya maandishi

Basi mimi niliposikia zoezi la anuani za makazi nikajua ni project ambayo ingepelekea kutengenezwa kwa barabara za mitaa pale ambapo nyumba zimejengwa kiholela kiasi kwamba hata ukozuka ajali ya moto gari ya zimamoto haiwezi kupita.

Nikajua zoezi hilo lingeboresha mitaa na kuondoa ile hali ya wananchi kupaki gari kuliko na ofisi ya CCM n.k

Kumbe si Simba si yanga [emoji2357][emoji848][emoji848]
 
View attachment 2214584

Majaliwa ameyasema leo Ijumaa Mei 6, 2022 wakati akizindua mradi wa Afya yangu unaofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Marekani (USAID).

Amesema kazi ya maandalizi ya sensa ya watu na makazi inaendelea nchini ambayo inaenda sambamba na anwani za makazi.

Majaliwa amewataka Watanzania kushiriki katika sensa ya watu na makazi na kwamba haitakuwa faida kwa Watanzania tu pekee bali na taasisi zote zinazofanya kazi na Serikali ya Tanzania.

Amesema kazi hiyo inaendelea na imefikia asilimia 86 katika kuikamilisha uwekaji wa anwani za makazi na kwamba kazi iliyobaki ni kuchomeka vibao kuonyesha mitaa.

“Ingawa vibao vingine vimeandikwa kimakosa lakini najua yatarekebishwa. Juzi nilikuwa natembea nikaona bango moja limeandikwa Mahakama load badala ya Road (barabara) imeandikwa load,”amesema.

Majaliwa amewataka makatibu tawala kuangalia usahihi wa majina ya mitaa hiyo.

“Wanapoandika majina haya mhakiki mara mbili mbili. Msikubali kwenda kubandika kibao kikiwa kimekosewa. Yapo majina ya watu yahakikiwe vizuri,”amesema.

Amesema kuna bango moja limeandikwa kimakosa Feed Force badala ya Field Force na lingine lilikuwa likiandikwa jina lake lakini limekosewa pia.

Chanzo: Mwananchi

vitapanda elikopta mara ya pili
IMG_6678.jpg
 
Back
Top Bottom