PreGE2025 Waziri Mkuu, Majaliwa atangaza kugombea tena Ubunge wa Ruangwa akiaga Bunge

PreGE2025 Waziri Mkuu, Majaliwa atangaza kugombea tena Ubunge wa Ruangwa akiaga Bunge

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Ni bora pia tusichague Marais wapya Ili kupunguza gharama maana wakistaafu watalipwa
Mara kadhaa nimeshauri miaka ya kukaa madarakani iongezwe at least iwe miaka 7. Mwaka wa kwanza kupanga safu yake ya Uongozi mwaka 2 mpaka 6 miaka ya kazi na mwaka wa Saba kujiandaa kukabidhi ama kuendelea kupewa imani na wananchi kwa kipindi kingine. Pia hii itatupunguzia gharama za uchaguzi...miaka....ndani ya miaka 15 uchaguzi mara 3 wakati mara mbili inatosha. Kwanza Umeona bajeti ya uchaguzi wa mwaka huu?

Sijapangilia vizuri maelezo lakini yachambue hivyo hivyo.
 
Tangu uliwe ndogo hujawahi kujitambua hata mamlaka hauzitambui.
Naongea ninachokijua, hakunaga mtu mwenye mihemko akawa na msimamo.
Hawa wa hivi wanayumbaga sana na mifumo mfano wake ni Makonda.
 
Mwambieni kabisaa ajue hakuna kupita bila kupigwa.
Na uchaguzi haupo kama reforms hakuna.
 
Waziri Mkuu wa JMT Mh Kassim Majaliwa amesema atarudi tena Jimboni Ruangwa Mkoani LINDI kuomba ridhaa tena kwa Wananchi wake kuliongoza tena Jimbo hilo kwa miaka mitano ijayo(2025/2030).

Kauli hiyo ya kishujaa ulipokelewa na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa vigeregere makofi na shangwe kubwa ndani ya UKUMBI wa Bunge Jiji Dodoma hivi karibuni!

Makofi hayo kutoka Kwa Wabunge yalitokana KAZI kubwa ambayo imefanywa na Serikali ya awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Mh Rais Samia Suluhu Hassan,Dr Philip Mpango,Makamu wa Rais,Mh Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu na Dr Dotto Biteko,Naibu Waziri Mkuu!

Katika hotuba yake ya kulifunga Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jana,Mh Rais Samia Suluhu Hassan alimsifia na kumshukuru Mh Waziri Mkuu Majaliwa kwa Weledi wake, Unyenyekevu na Uchapakazi wake katika kipindi chote cha miaka minne kama Msaidizi wake wa karibu katika kuendesha shughuli za Serikali ya awamu ya Sita!

Lakini pia,wakati wa hotuba yake ya kuhitimisha shughuli za Serikali Bungeni,Mh Waziri Mkuu Majaliwa alimshukuru SANA Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kufanya nae KAZI kwa ushirikiano mkubwa na kuifanya KAZI yake ya Uwaziri Mkuu kuwa nyepesi sana!

Mh Majaliwa alimsifu Mh Rais Samia kwa kupeleka Miradi mingi ya Maendeleo jimboni kwake na kusema wana-Ruangwa hawana sababu ya kutompambania Mama Samia katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu kutokana na mambo MAKUBWA aliyowafanyia!

Mradi mkubwa wa Maji kutoka pale Jimboni Ruangwa kwenda mpaka Wilaya ya Nachingwea,Mradi wa Barabara ya lami kutoka Ruangwa mjini mpaka Nanganga,mradi wa Barabara kutoka Ruangwa kwenda wilayani Nachingwea,Miradi ya Ujenzi wa Shule,Hospitali, ni miongoni mwa Miradi ambayo imeendelea kulifanya Jimbo la Ruangwa kuwa Jimbo la Mfano Mikoa ya Kusini kwa sasa!

Ni wazi kuwa hakuna wa kumzuia Mh Waziri Mkuu Majaliwa kuwa Mbunge wa Jimbo hilo kwani KAZI zake kwa Wananchi wa Jimbo la Ruangwa zinaonekana na zinaendelea kwa kasi kubwa sana!

Hongera Mh Waziri Mkuu kwa kuwa na mapenzi mema na Wananchi wako wa Jimbo la Ruangwa,Mkoani LINDI huku pia kwa wakati huo huo ukiwatumikia Watanzania wote kwa kipindi cha miaka 10!

Hakika umefanya KAZI ya kunisaidia Mh Rais Samia kwa nguvu kasi na akili kubwa ndio maana Nchi "ilikimbia"sana wakati wa awamu hii ya Sita!

George Michael Uledi!
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ametangaza kugombea tena Ubunge wa Jimbo la Ruangwa mkoani Lindi, amesema hayo akilihutubia Bunge kwa mara ya mwisho leo Juni 26, 2025 jijini Dodoma.

"Ninawashukuru sana wana Ruangwa kwa kuniunga mkono na kunipatia ushirikiano katika kipindi chote nilipokuwa nikitekeleza majukumu ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ninatambua wakati mwingi nimekuwa nje ya jimbo nikilitumikia taifa lakini wana Ruangwa wameendelea kuniunga mkono. Nitumie nafasi hii kusema asanteni sana na ninamuomba Mwenyezi Mungu azidi kuimarisha mshikamano uliopo kati yetu sote. Ninaomba kuwajulisha kuwa ninakuja kuchukua fomu ya kuomba ridhaa yenu tena."

Soma, Pia: Ruangwa wamlipia Fomu ya Urais Dkt. Samia na Ubunge Majaliwa

Ndimi mbili!
 
Back
Top Bottom