PreGE2025 Waziri Mkuu, Majaliwa atangaza kugombea tena Ubunge wa Ruangwa akiaga Bunge

PreGE2025 Waziri Mkuu, Majaliwa atangaza kugombea tena Ubunge wa Ruangwa akiaga Bunge

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Ila watu wa kusini sijui wana nini? Mbona aibu za reja reja zina epukika kabisa?

1St Lady kuwa mgonga meza.
PM anataka kuwa mgonga meza bila cheo. Lol

Ulafi wa madaraka ni Uraibu, kuliko neno lenyewe. Uwiiiih.
Wao kule hawajuwi hilo, ukiwajengea misikiti na madras TOSHA!
LIBRARY, shule, vyuo, maabara peleka kwingine!
 
Alikuwa na meno wakati wa JPM!
Kwa sasa? Hana meno, hana mvuto kisiasa, hana jpya, kawa chawa, hovyo hovyo, mchumia tumbo tu!
INASIKITISHA SANA SANA SANA!
 
Kweli kujiajiri ni kazi ngumu,yaani miaka yote kumi ya uwaziri mkuu haujamtosha?Anataka kurudi tena bungeni kugonga meza bila cheo.
 
Huyu bwana angekuwa jimboni kwangu ningetoka nje kupiga kura kwa sababu yake, anaitendea haki nafasi yake na tungebahatika kumpata rais wa hivyo tz ingefika mbali sana lkn ndio hivyo tena naona kama umri umesogea sana.
 
Mafao analipwa asilmia 80 ya mshahara wa waziri mkuu aliyepo na mkewe analipwa bado tu anataka ubunge baada ya kukaa miaka 10 uwaziri mkuu

Hapana hatutendei haki watanzania

Pinda mbona yupo anajishughulisha na kilimo?
Tz km ni mwl wengi Wana shida kichwani!
 
Dah! Angestaafu kulingana na wadhifa alio nao angeheshimika sana, tofauti na hapo tafsiri itakuwa haridhiki na alivyo navyo.
Mwacheni jamani, mbona Samia walieanza naye anagombea. Sasa kwanini yeye asigombee. Sio kwamba haridhiki ila awamu haijaisha. Bado ananafasi ya kuwa waziri mkuu. Mipango iliyopangwa awamu hii na yeye akiwepo bado inahitaji usimamizi wake. Hawezi kustaafu wakati awamu aliyomo haijamaliza muda wake.
 
Ridhikeni ndugu zangu, kwani hakuna kazi nyingine za kufanya ? Hamjajifunza kwa MPANGO?
Yuko pia waziri mkuu mstaafu Pinda yuko vizuri tu mbona.

Majawaliwa ataenda kupoteza hadhi na heshima kama Malecela na Sumaye ndiko anakoelekea akichukua fomu

Atabaki Pinda tu kama mheshimika kila eneo serikalini,bungeni nk

Sumaye na Malecela wakipita popote hakuna watu wa kuwashobokea

Huyu Majaliwa naye anataka kuunga tela

Maisha sio pesa aelewe hilo .Kuheshimiwa pia ni kitu muhimu.Wako watu huwa na pesa sana tu lakini hufa kwa presha kwa kukosa Kuheshimiwa tu
 
Na kulipwa mafao yote kama waziri mkuu mstaafu anataka tena ubunge alipwe pesa za ubunge tena

CCM kuweni na huruma mtu mmoja asibane nafasi za wengine pia kupata ajira bunge na kipato.

Hapo ina maana ajira za kipato za watu wawili anabeba zote yeye

Uwaziri mkuu mstaafu una kipato na ubunge una kipato.Katumika miska 10 uwaziri mkuu apumzike apishe wengine ale pension ya uwaziri mkuu mstaafu

Vijana chukueni form kwa wingi Rwangwa
Anataka afuate nyayo za Malecela

Cheo kama uwaziri mkuu ukifika ukatumika miaka 10 vizuri kwenda kupumzika

Maana ya maslahi ya viongozi wastaafu na wenza wao naona sasa inapoteza umaana kabisa.

Kwa mtindo huu heri yafutwe tu
Msikalili mambo uwaziri mkuu sio kama urais hauna kikomo katika katiba yetu. Uwaziri mkuu sawa na ubunge.
 
Kutoka kwenye ajira hawataki Alafu wakishapita badae wanakuja kutuambia hakuna ajira na kutengeneza ajira sio kazi yao tukajiajiri huko
Tunaambiwa, 'VIJANA NI TAIFA LA KESHO'! Kama wazee ndio hawa, wanang'ang'ania hizo nafasi, hao vijana 'WATATAIFIKA' lini?
 
Mwacheni jamani, mbona Samia walieanza naye anagombea. Sasa kwanini yeye asigombee. Sio kwamba haridhiki ila awamu haijaisha. Bado ananafasi ya kuwa waziri mkuu. Mipango iliyopangwa awamu hii na yeye akiwepo bado inahitaji usimamizi wake. Hawezi kustaafu wakati awamu aliyomo haijamaliza muda wake.
Ujinga mtupu katumikia uwaziri mkuu miaka 10 aende zake huko

Raisi Samia hajatumikia miaka 10 ruksa kuendelea. Majaliwa hapana tafadhali.Pilau ni chakula kizuri sana tu lakini huwezi kuila kila siku mwaka mzima inakinaisha

Majaliwa hapana asirudi hata ubunge.Aende akale mafao ya mawaziri wakuu wastaafu na wenza wao
 
Kutoka kwenye ajira hawataki Alafu wakishapita badae wanakuja kutuambia hakuna ajira na kutengeneza ajira sio kazi yao tukajiajiri huko
Tunaambiwa, 'VIJANA NI TAIFA LA KESHO'! Kama wazee ndio hawa, wanang'ang'ania hizo nafasi, hao vijana 'WATATAIFIKA' lini?
 
Msikalili mambo uwaziri mkuu sio kama urais hauna kikomo katika katiba yetu. Uwaziri mkuu sawa na ubunge.
Waondolowe mafao ya ustaafu kama ni hivyo.Wamepewa ya nini kama wanataka kuendelea tu baada ya kutumikia miaka 10?

Nilikuwa namheshimu Majaliwa lakini akigombea sitamheshimu tena
 
Ila watu wa kusini sijui wana nini? Mbona aibu za reja reja zina epukika kabisa?

1St Lady kuwa mgonga meza.
PM anataka kuwa mgonga meza bila cheo. Lol

Ulafi wa madaraka ni Uraibu, kuliko neno lenyewe. Uwiiiih.
Mh!!!!!
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ametangaza kugombea tena Ubunge wa Jimbo la Ruangwa mkoani Lindi, amesema hayo akilihutubia Bunge kwa mara ya mwisho leo Juni 26, 2025 jijini Dodoma.

"Ninawashukuru sana wana Ruangwa kwa kuniunga mkono na kunipatia ushirikiano katika kipindi chote nilipokuwa nikitekeleza majukumu ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ninatambua wakati mwingi nimekuwa nje ya jimbo nikilitumikia taifa lakini wana Ruangwa wameendelea kuniunga mkono. Nitumie nafasi hii kusema asanteni sana na ninamuomba Mwenyezi Mungu azidi kuimarisha mshikamano uliopo kati yetu sote. Ninaomba kuwajulisha kuwa ninakuja kuchukua fomu ya kuomba ridhaa yenu tena."

Soma, Pia: Ruangwa wamlipia Fomu ya Urais Dkt. Samia na Ubunge Majaliwa

Sawa, mitano tena:KKomrade:
 
Na hii ndio kasumba ya ngozi nyeusi........issue ni kuridhika.........wanasahau kwamba uwezi kuzikwa na mali kaburini
Acha kujinyanyapaa wewe - Putin wa Urusi ana miaka mingapi? Trump wa USA ana miaka mingapi na wako madarakani!!!!

Kinachokushinda tulia anayekiweza akifanye
 
Back
Top Bottom