PreGE2025 Waziri Mkuu, Majaliwa atangaza kugombea tena Ubunge wa Ruangwa akiaga Bunge

PreGE2025 Waziri Mkuu, Majaliwa atangaza kugombea tena Ubunge wa Ruangwa akiaga Bunge

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Huyu angepumzika tu
Hivi hawa watu hawaoni
Aibu,maana akirudi atakuwa mbunge alafu hana uwaziri mkuu
Akiwa bungeni ataanza kuomba wajengewe sijui matundu ya choo,mara visima vya maji,mara anaomba madawati

Ova
Nimemdharau sana!
Tamaa kali sana...
Ina maana hawezi kufanya kitu kingine wakati ana resources zote na anatunzwa mpaka afe..duh..hahaha
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ametangaza kugombea tena Ubunge wa Jimbo la Ruangwa mkoani Lindi, amesema hayo akilihutubia Bunge kwa mara ya mwisho leo Juni 26, 2025 jijini Dodoma.

"Ninawashukuru sana wana Ruangwa kwa kuniunga mkono na kunipatia ushirikiano katika kipindi chote nilipokuwa nikitekeleza majukumu ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ninatambua wakati mwingi nimekuwa nje ya jimbo nikilitumikia taifa lakini wana Ruangwa wameendelea kuniunga mkono. Nitumie nafasi hii kusema asanteni sana na ninamuomba Mwenyezi Mungu azidi kuimarisha mshikamano uliopo kati yetu sote. Ninaomba kuwajulisha kuwa ninakuja kuchukua fomu ya kuomba ridhaa yenu tena."

Soma, Pia: Ruangwa wamlipia Fomu ya Urais Dkt. Samia na Ubunge Majaliwa
Njaa ni noma,
 
Dah! Angestaafu kulingana na wadhifa alio nao angeheshimika sana, tofauti na hapo tafsiri itakuwa haridhiki na alivyo navyo.
Kasema hapo alikuwa nje ya jimbo mda mrefu,kwahiyo sasa hivi ndio anaenda kufanya kazi....
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ametangaza kugombea tena Ubunge wa Jimbo la Ruangwa mkoani Lindi, amesema hayo akilihutubia Bunge kwa mara ya mwisho leo Juni 26, 2025 jijini Dodoma.

"Ninawashukuru sana wana Ruangwa kwa kuniunga mkono na kunipatia ushirikiano katika kipindi chote nilipokuwa nikitekeleza majukumu ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ninatambua wakati mwingi nimekuwa nje ya jimbo nikilitumikia taifa lakini wana Ruangwa wameendelea kuniunga mkono. Nitumie nafasi hii kusema asanteni sana na ninamuomba Mwenyezi Mungu azidi kuimarisha mshikamano uliopo kati yetu sote. Ninaomba kuwajulisha kuwa ninakuja kuchukua fomu ya kuomba ridhaa yenu tena."

Soma, Pia: Ruangwa wamlipia Fomu ya Urais Dkt. Samia na Ubunge Majaliwa
Na kulipwa mafao yote kama waziri mkuu mstaafu anataka tena ubunge alipwe pesa za ubunge tena

CCM kuweni na huruma mtu mmoja asibane nafasi za wengine pia kupata ajira bunge na kipato.

Hapo ina maana ajira za kipato za watu wawili anabeba zote yeye

Uwaziri mkuu mstaafu una kipato na ubunge una kipato.Katumika miska 10 uwaziri mkuu apumzike apishe wengine ale pension ya uwaziri mkuu mstaafu

Vijana chukueni form kwa wingi Rwangwa
Anataka afuate nyayo za Malecela

Cheo kama uwaziri mkuu ukifika ukatumika miaka 10 vizuri kwenda kupumzika

Maana ya maslahi ya viongozi wastaafu na wenza wao naona sasa inapoteza umaana kabisa.

Kwa mtindo huu heri yafutwe tu
 
Angestaafu, Kuna zile za kua balozi na Ofisi ya Raisi, Kua katibu Mkuu ni nyingi tu lkn sio ubunge
Mafao analipwa asilmia 80 ya mshahara wa waziri mkuu aliyepo na mkewe analipwa bado tu anataka ubunge baada ya kukaa miaka 10 uwaziri mkuu

Hapana hatutendei haki watanzania

Pinda mbona yupo anajishughulisha na kilimo?
 
Huyu angepumzika tu
Hivi hawa watu hawaoni
Aibu,maana akirudi atakuwa mbunge alafu hana uwaziri mkuu
Akiwa bungeni ataanza kuomba wajengewe sijui matundu ya choo,mara visima vya maji,mara anaomba madawati

Ova
Nadhani mama kamuhaidu kitu.
 
Back
Top Bottom