JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Kuna hii habari nimeikuta kwenye vuombo vyetu vya habari Nchini, ni kuhusu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kutoa taarifa ya kutoa maagizo kwa vyombo vyenye mamlaka ya kusimamia sheria ikiwemo Mahakama.
Unaweza kuisoma habari yenyewe hapo chini, nakubali kweli hoja yake ni nzuri na inaweza kusaidia haki kupatikana haraka ili iwe funzo kwa watu wengine, lakini ninachojiuliza ni sahihi kwa Majaliwa kuipa maagizo Mahakama au alitakiwa kuishauri tu?
Hili lipoje kisiasa na kisheria kwa kuwa nafahamu Mahakama ni mhimili unaojitegemea...
-----------------------------------------------
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameviagiza vyombo vya sheria ikiwamo Jeshi la Polisi, Mahakama na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP), kufanyia kazi na kutoa uamuzi wa mashauri yote yanayohusu watoto ndani ya miezi sita na sio vinginevyo.
Pia, amezionya familia ambazo zimekuwa na tabia ya kumaliza kesi zinazohusu watoto zenyewe bila kufikisha mashauri katika vyombo vya sheria kuacha mara moja.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu wa Bunge, George Simbachawene, alibainisha hayo alipokuwa akifungua kongamano la kitaifa la malezi ya watoto na familia kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mei 15, 2022.
“Waziri Mkuu amenituma nitoe maagizo haya kwa vyombo vyote vya sheria nchini kuhakikisha kuwa mashauri yote yanayohusu watoto yanafanyiwa kazi na kutolewa maamuzi ndani ya miezi sita na sio vinginevyo,” alisema Simbachawene.
Alisema hivi sasa matukio ya ukatili kwa watoto yamekuwa yakiongezeka na wahusika wakuu ni wanafamilia wenyewe.
Aidha, alisema jamii inapaswa kupaza sauti ili kupinga matukio ya ukatili kwa watoto kwa kuripoti katika vyombo vya sheria badala ya kumalizana kifamilia.
Wakati huohuo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu wa Bunge, George Simbachawene amesema kesi za ukatili dhidi ya watoto zilizoripotiwa mwaka 2021 jumla ni 11,499.
Waziri Simbachawene amesema takwimu za Jeshi la Polisi zinaonesha kuwa kuanzia Januari hadi Desemba, 2021 kulikuwa na idadi hiyo ya kesi ambapo matukio makubwa ni ubakaji 5,899, mimba 1,677 na ulawiti ni 1,114.
Source: IPP Media