Waziri Mkuu Majaliwa na uhalali wa maamuzi hadharani


Majaliwa ni msanii sana !
 
Makosa ya kiserikali,na kuteua makada wa chama kuwapa nafasi za kiutendaji imedhoofisha ufanisi wa taasisi zinazosimamia hizi Mamlaka za Serikali.

Taarifa za ndani za Serikali zinajadiliwa mbele ya kamera,hii ni kuidhofisha Serikali mbele ya wananchi bila kujua.

Viongozi wafanyiwe mafunzo ya kiutawala na uendeshaji na maadili, bila kuzingatia na kurekebisha haya siku ya uchaguzi huru na haki hakuna atayechaguliwa sio mfanya kiki wala chama.
 
Lazima ajikite kwa watu wa chini kwa sababu huku ndiko Kuna miradi ambayo watu wa kawaida wanaiona na pia ndiko anaweza kukutana naonkwa kiki n...
Sawa. Ila yeye kwa cheo chake alitakiwa awabane hao wa juu ili kuleta Uwajibikaji kwa wale wa chini. Tanzania ni nchi kubwa sana.

Hata afanyeje hataweza kugusa kila mahali. Kama siyo kutafuta kiki basi ajikite kwenye report ya CAG atuonyeshe huo uchapakazi wake. Madudu yanayoibuliwa na CAG pia yana audit report.
 
Leadership style hii ya kutumbua majipu hadharani, iltamalaki kipindi cha Serikali ya awamu ya tano.

-Waziri Mkuu ni zao la Serikali ya awamu ya tano,kwa hiyo anaendeleza leadership style ya awamu iliyopita.
-Leadership style hii haikuwa fair wakati ule na sasa hivi.

-Sina uhakika Kama watumishi wote walioadhirika na leadership style hii wamepata relief baada ya kufanya uchunguzi na kuonekana hawana hatia. -watendaji wetu,wawe Wazalendo,na watumie rasilimali chake tulizo nazo.

-wanaotumbuliwa ni wachache tu , asilimia kubwa ya watendaji wa Serikalini na mashirika ya umma siyo wasafi.

-Waziri Mkuu anachofanya,mara nyingi,ni kuwasimamisha kazi watuhumiwa,ili kupisha uchunguzi,kwa mfano leo,amewasimamisha kazi Mhasibu na Mkurugenzi huko Sumbawanga, baada ya wahusika kutuhumiwa kwa kuungua nyaraka nyeti za mradi katika mazingira ya kutatanisha.

Ushauri
1. Serikali iweke mifumo sahihi na endelevu wa kufanya kazi.

2. Mawaziri wa kisekta watimize majukumu yao kuondoa muhali.

3. Mahakama ifanye kazi kwa weledi,itoe haki bila upendeleo.

4. Vyombo vya uchunguzi vifanye kazi kwa weledi na kwa muda mfupi.

5. Watuhumiwa wawekwe pembeni kupisha uchunguzi.Lakini ifanyike kwa wahalifu wote,pasiwe na double standard.

6. Serikali na vyombo vyake vya uchunguzi ,viwe vinawasafisha watuhumiwa wote, ambao wamebainika hawana makosa,kwa maana kuna waadhirika wengi wa maamuzi haya ambao hawajui hatima yao toka awamu tano na wengine wamefariki

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo la wabongo lipo palepale,hamtaki waovu,walarushwa washughurikiwe.Wasiposhughurikiwa mnakuja hoo serikali hii chovu sana.Hamueleweki.
 
Wcha ufisadi utafungwa

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Acheni kumnanga majaliwa ni bora mara mia huyu majLiwa kuliko

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Kuwataja kuna faida zake pia,inakuwa ni alert kwa wengine kujua kwamba ufuatiliaji upo na hatua zinachukuliwa hivyo wengine kuogopa kufanya matendo hayo
 
Mama yako anaupiga mwingi endelea kukenua meno yote,acha ukigeugeu
 
Kwahiyo mnafurahia watu wanapora mali ya umma kisha wanachoma nyaraka?[emoji706][emoji706]
 
At least yeye kaonesha njia ya kufanya watu kuwajibika na hawawezi kujisahau. Kukosea kupo tuu, Magufuli alisema acha tukosee tutarekebisha mbele kwa mbele
 
Huyu mwamba usipomtaja account yako haisomi?[emoji706][emoji706]
 
Wengine ni wateule wa mkubwa wake,anachofanya ni kumpa taarifa na kumshauri,hilo linabaki kwa anayeupiga mwingi,kuubeba ushauri au kuupotezea
 
SIO KWA LICHAMA CCM ! Majizi Hayo hayataki udhibiti ! Hakuna mwana ccm hata mmoja asiye mwizi! Japokua na wale wa vyama vingine wanaweza kua wezi pia maana pia ni wa TZ
Wabongo wezi ila CCM nayo ni majizi yaliyokubuhu. Yametunyonya sana watanzania
 
Huyu mwamba usipomtaja account yako haisomi?[emoji706][emoji706]
Hawezi kwepa haya ya ufisadi maana Miaka 6 amekuwepo Madarakani na hii miradi mingi aliiacha.
Hakuna mradi hata mmja ambao pm kakagua huko Rukwa ambao Umeanza awamu hii,na hiyo miradi Pesa zilikuwa na haikukamilika..

Zama za Mwendazake aliyeaminisha watu kwamba Serikali take hainaufisadi Hakuna mtu angethubutu kusema Kuna ufisadi ili amuaibishe bwana mkubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…