Waziri Mkuu Majaliwa: Serikali imekamilisha malipo ya ununuzi wa ndege mpya tatu

Waziri Mkuu Majaliwa: Serikali imekamilisha malipo ya ununuzi wa ndege mpya tatu

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema malipo ya ununuzi wa ndege mpya tatu yamekamilika, na zinatarajiwa kuwasili mwaka 2021/22.

Akiwa Bungeni Dodoma leo, Waziri Mkuu amesema ununuzi huo utawezesha Serikali kuwa na jumla ya Ndege 12. Aidha, amesema kuanzishwa kwa safari za Guangzhou (China) kutakuwa chachu ya kuimarisha Biashara, Utalii na Ajira.

Vilevile, Majaliwa amesema ujenzi na upanuzi wa Viwanja vya Ndege vya Shinyanga, Kigoma, Tabora na Sumbawanga vitakavyogharimu Tsh. Bilioni 176 unaendelea.

PM.jpg
 
Kwenye reli SGR naweza kuwaelewa maana itachochea ukuaji wa uchumi maana itagusa watu wengi saana though ni kosa kuijenga kwa kitumia fedha za ndani 12 Trilion. Kwa nini ukiumize kizazi hiki kwa kukibana wakati project itaishi zaidi ya miaka 100?

Huku kwenye ndege so afar ishafeli...tangu hiyo Dreamliner itue kwa mfano niambieni ishasafiri km ngapi angani hadi leo hii?

Mawazo yanaweza kuwa mazuri ila approach ndiyo bomu.
 
Asilimia kubwa ya watanzania hasa wapiga kura huona njee na si ndani... Ni ngumu kumuelewesha mtanzania ambae si mfatiliaji kuwa eti ndege zinaleta Hasara akakuelewa .

Na hii ndo ilipelekea Mzee mwendazake kueleweka au kusifika kwa ununuzi wa ndege kwa hao wanaoitwa wanyonge maana Impact yake hawaijui na hata ukajaribu muelezea anakuona mpingajii tuu .

Si kwamba nae mzee hajui ni hasara ila navyojua tamaduni za watu wa huko hupenda kuona mavitu makubwa makubwa ili apate sifa hata kama mnakufa njaa hapo ndani
 
Nawahurumia wanao dai Mafao NSSF
Kuhusu mafao ukishafika umri wa miaka 60 tutakupa 25% ya hayo then 75% tutakupa kidogo kidogo hadi ufe...hatutaki usumbue ndugu, mķeo na watoto wako kukuuguza na kukuzika..tunataka uwe na kipato chako kidogo kidogo mwenyewe.
Tunajua tukiwapa mnakula hela zote bila kujali mbeleni mtaishije ..mnazipa familia zenu mzigo wasiostahili.
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema malipo ya ununuzi wa ndege mpya tatu yamekamilika, na zinatarajiwa kuwasili mwaka 2021/22

Akiwa Bungeni Dodoma leo, Waziri Mkuu amesema ununuzi huo utawezesha Serikali kuwa na jumla ya Ndege 12. Aidha, amesema kuanzishwa kwa safari za Guangzhou (China) kutakuwa chachu ya kuimarisha Biashara, Utalii na Ajira

Vilevile, Majaliwa amesema ujenzi na upanuzi wa Viwanja vya Ndege vya Shinyanga, Kigoma, Tabora na Sumbawanga vitakavyogharimu Tsh. Bilioni 176 unaendelea
China tutakwisha na vovid
 
Kazi inaendelea...
 
CCM ni kichwa cha mwendawazimu kinachotembea!Hivi inawezekana vipi watu kama hawa wanaingia madarakani?
Watz ndiyo wanawachagua nyinyi bakini huku kwenye mitandao ya kijamii mnaandika udaku tu!! Kazi Inaendelea!!
 
Common sense tu tangia tuambiwe hizo ndege zimeshanunuliwa ni muda.

Manunuzi ya ndege mpya sio kama gari unaenda show room na kuondoka nalo.

Ndege unatoa order ndio unatengenezewa na serikali imesha commit by now sehemu kubwa ya deposit imeshalipwa.
 
Kwenye reli SGR naweza kuwaelewa maana itachochea ukuaji wa uchumi maana itagusa watu wengi saana though ni kosa kuijenga kwa kitumia fedha za ndani 12 Trilion. Kwa nini ukiumize kizazi hiki kwa kukibana wakati project itaishi zaidi ya miaka 100?

Huku kwenye ndege so afar ishafeli...tangu hiyo Dreamliner itue kwa mfano niambieni ishasafiri km ngapi angani hadi leo hii?

Mawazo yanaweza kuwa mazuri ila approach ndiyo bomu.
Dreamliner zipo 2 ndugu wala sio moja...na zinakusanya tu vumbi pale airport..mara moja au mbili kwa wiki zinaenda hapo india walau engine zipashwe pashwe...ila india kupeleka dreamliner ni ghali..route hiyo hata airbus zingeweza ila wanaishia kupeleka dreamliner ili zisije zikageuka mazalia ya popo
 
Back
Top Bottom