Waziri Mkuu Majaliwa: Serikali imekamilisha malipo ya ununuzi wa ndege mpya tatu

Waziri Mkuu Majaliwa: Serikali imekamilisha malipo ya ununuzi wa ndege mpya tatu

Husu Sumbawanga hata dalili ya kufyeka nyasi hakuna sijui ujenzi unaendelea wapi.

Huyu jamaa kwa uongo ni kiboko
 
Kwenye reli SGR naweza kuwaelewa maana itachochea ukuaji wa uchumi maana itagusa watu wengi saana though ni kosa kuijenga kwa kitumia fedha za ndani 12 Trilion. Kwa nini ukiumize kizazi hiki kwa kukibana wakati project itaishi zaidi ya miaka 100?

Huku kwenye ndege so afar ishafeli...tangu hiyo Dreamliner itue kwa mfano niambieni ishasafiri km ngapi angani hadi leo hii?

Mawazo yanaweza kuwa mazuri ila approach ndiyo bomu.
Kuna reli ya Tazara mpya,uliza kama imewahi chochea uchumi.

Kinachoongezeka hapo ni speed ya train lakini hakuna cha kusafirisha sgr ilikoelekezwa
 
Serikali inapenda ndege kuliko kuboresha hospitali kwa ajili ya matibabu ya wanyonge.
Nashangaa sana kusikiwa Waziri Mkuu akishadidia kuongeza ndege za ATCL hata pale CAG ameonesha udhaifu mkubwa wa shirika na kuwa na hasara ya uendeshaji ya kutisha. Sijui kama serikali inafahamu after effects za haya maamuzi kwa maendeleo ya nchi!!!

Hivi sasa shirika lina overcapacity katika ndege tulizonazo ukilinganisha na routes tunazokwenda; ndege zetu haziendi nje zaidi ya comoro kwa sababu ya madeni ambayo hayajalipwa!! Kuwa na overcapacity kwenye shirika la ndege ni hasara kubwa na kuongeza ndege nyingine hasara itakuwa kubwa zaidi!! Ndege Kubwa ya DRAMLINER Ndio inatia hasara sana kwani hii ni ndege ya masafa marefu hivyo kuitumia kwa domestic flights ni hasara tu!! Hizi nyimbo za kwenda China zimeimbwa toka siku nyingi na hata juzi Waziri Mkuu bado anaimba kuwa hizo safari za China zitaongeza biashara ikionesha kuwa toka hiyo ndege ifike nchini haijafanya hizo safari za china!!

Ikumbukwe kuwa ATCL inapokuwa na hasara mzigo wote unabebwa na mwananchi kwa kuongezewa kulipa kodi zaidi! Waziri Mkuu hana budi kujua hilo kuwa kuwaongezea mzigo wa kodi wananchi kwasababu ya maamuzi ya hovyo ya Serikali yanaathiri maendeleo na maisha ya wananchi. Inawezekana hana upeo huo kama inavyoonesha, lakini akili ya kawaida tu ingeonesha kuwa ingekuwa busara kama ile order ya ndege mpya ingesitishwa under the circumstances na fedha kutumika kwa sehemu nyingine za maendeleo. Pia kwa kusitisha ununuzi wa ndege hizo mpya kungelipunguzia shirika hasara zaidi itakayotokana na kuwa na overcapacity. Kumbuka ndege sio kama mabasi; hazitakiwi kuwa ardhini bali kuwa angani na zina faida zikiwa angani kama zimeeba abirai wa kutosha!! Zikiwa ardhini ni wakati wa kufanya matengenezo tu ama sivyo zitatengeneza hasara.

Kuongeza ndege mpya kwa shirika ni uamuzi usio kuwa na uzalendo hata kidogo kwani umezingatia maslahi ya watu wachache na sio wananchi walio wengi. Serikali inafumbia macho ukweli kuwa ATCL haina ROUTES nyingi zaidi ya LOCAL routes ; ndege za ATCL haziwezi kuruka kwenda South Africa kwa kuogopa ndege kukamatwa na hata hiyo route ya China kuna ushindani mkubwa sana kutoka kwa majirani zetu hivyo shirika linahitaji weledi mkubwa kulikwamua!
 
Ameshindwa kusema kuwa order zilishawekwa tangu enzi za jpm na possibly wanakabwa na vifungu vya order cancelation, wazilete tu baba CAG atatuambia mwakani zimeingiza nini. Kazi iendelee.
Penalties za cancellation ya order ndiyo inayowafanya, wajitoe ufahamu, ni wajinga tu wanaoweza kununua midege huku wakijua inaleta hasara zisizopimika.

Nimemdharau PM kuliko maelezo. Ila mwendazake ndiyo kawaweka kwenye tight corner! Akisaidiwa na huyo speaker.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Asilimia kubwa ya watanzania hasa wapiga kura huona njee na si ndani... Ni ngumu kumuelewesha mtanzania ambae si mfatiliaji kuwa eti ndege zinaleta Hasara akakuelewa .

Na hii ndo ilipelekea Mzee mwendazake kueleweka au kusifika kwa ununuzi wa ndege kwa hao wanaoitwa wanyonge maana Impact yake hawaijui na hata ukajaribu muelezea anakuona mpingajii tuu .

Si kwamba nae mzee hajui ni hasara ila navyojua tamaduni za watu wa huko hupenda kuona mavitu makubwa makubwa ili apate sifa hata kama mnakufa njaa hapo ndani
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Wakubwa tuoneeni huruma watoto wenu wadogo zenu. Hizi pesa wekeni hata kwenye ajira tujikwamue na tukwamue familia zetu wakubwa..
 
Penalties za cancellation ya order ndiyo inayowafanya, wajitoe ufahamu, ni wajinga tu wanaoweza kununua midege huku wakijua inaleta hasara zisizopimika.

HILI SUALA LA CANCELLATION YA ORDER COULD HAVE BEEN SOLVED DIPOLATICALLY KWA KUMTUMIA MAMA MWANADIPLOMASIA BALOZI MULAMULA; LAKINI KWASABAU CHAMLIHO AMEKULA 10% YAKE NDIO ATAWASHAWISHI KUWA HAIWEZEKANI!!! HILO LINGEWEZA KUZUNGUMZIKA NA BOEING WANGEWEZA KUWAIVE HIZO PENALTIES.
 
Asante sana PM Majaliwa,nina6amini kabisa 2025 wewe ndo rais wetu,naomba iwe hivyo ,Mungu akubariki sana
Huyo muongo analeta porojo tu, hela hawana za kununua ndege, na kama ni kulipwa basi zilishalipwa na yule dhalimu hapo kabla.
 
Wameshasema "ATCL inatoa huduma", kama vile madaraja na barabara na huduma hiyo inasaidia "kuchochea ukuaji wa biashara na sekta nyingine". Hawa jamaa hawana mpango wa kufanya biashara

WAMEBADILISHA LINI SHERIA ILIYOUNDA ATCL NA KULIFANYA SHIRIKA LA KUTOA HUDUMA?
 
Akizungumzia maendeleo ya Miradi Mbalimbali inayoendelea kutekelezwa na wakati Bajeti ya ofisi yake Ikipitishwa. Waziri Mkuu Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania amesema Ndege Zingine Tatu ziko mbioni kuja Nchi wakati wowote kutekeleza ahadi ya Serikari katika uboreshaji wa Usafiri wa Anga Nchi.

Una neno gani Mdau juu ya Uamuzi huu mzuri unaoonesha ustawi chanya wa Nchi yetu.

Mbarikiwe sana.
 
Ungemalizia kwa kusema aina ya Ndege zinazokuja ingefaa zaidi.
Kwa kutaja aina tungejua kama zitafanya kazi au ni za kukaa kwenye eneo la maegesho kama ilivyo kwa zile kubwa mbili zinazootea jua.
 
Ungemalizia kwa kusema aina ya Ndege zinazokuja ingefaa zaidi.
Kwa kutaja aina tungejua kama zitafanya kazi au ni za kukaa kwenye eneo la maegesho kama ilivyo kwa zile kubwa mbili zinazootea jua.
Ni Airbus A220-300 mbili na Dash Q-400 De-Havilland moja.

Kwa nini tunanunua ndege kampuni tofauti tofauti ? Boeing, Bombardier, Airbus, De- Havilland.

Hapo tunaingia gharama sana mikataba tofauti, maintenance, mafunzo etc.
 
Back
Top Bottom