Hatuna namna kwasasa maana ndiyo brand au equipment zilizopo kwenye fleet ya ATCL. Kwasasa tuendeleze hizohizo ila tusitafute zingine tofauti tena.
So far tuna marubani na huenda tumetrain wahandisi wa aina hizo za Ndege.
Mm nimeona at least hizo equipment ziko tailored kwa mazingira yetu kidogo, kuliko zingeongezwa Dreamliner tena zine kubanikwa juani..
Habari nzima ya kuongeza kununua ndege wakati zilizopo zinaleta hasara na hatuna business plan inayoeleweka kubadili biashara ni sawa na kusema hatuna jinsi hili kaburi tushaanza kujichimbia, tumefikia nusu, ni bora tumalize tu kuchimba lote tuzikwe.
This is what psychologists call "cognitive dissonance".
Yani unataka kwenda Kariakoo kwa njia fupi kabisa, umetoka Mwenge, unaelekea Mbezi kaskazini uelekeo tofauti na wa Kariakoo.
Unafika Africana, unaanza kustuka huku ninakoenda si Kariakoo.
Lakini unasema nishakwenda mbali sana, ngoja niendelee huko mbele Tegeta mpaka Bagamoyo labda kuna shortcut ya kunifikisha Kariakoo haraka.
Unaendelea kwenda kaskazini, muelekeo tofauti na Kariakoo, kwani Kariakoo iko kusini kwako.
Serikali ilitakiwa ijitoe kwenye biashara ya usafiri wa ndege na kujikita katika kujenga viwanja vya ndege na kukusanya kodi.
Kwa kuongeza idadi ya ndege bila ya business plan ya kueleweka, kitakachotokea ni ile hasara tuliyopata mpaka sasa tunaenda kuiongeza.
It's just simple common sense.